Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 miezi 8

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 miezi 8

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 anakaribia sana kufikisha miaka 7! Ni kipi kinacho endelea katika ukuaji na hatua muhimu za mtoto wako unazo tarajia kuona?

Kipenda roho chako sasa kinafikisha miaka 6 miezi 8, na kwa saa hii unaona kuwa miaka 7 inakaribia. Kwa kiasili, huenda utafurahikia jambo hili kama upasavyo. Katika hatua hii, utagundua kuwa mtoto wako anaweza andika majina yake kwa kirahisi. Kifungu chako cha furaha kinapenda kuwa hai sana wakati wote.

Hatua hii pia ni ya kufurahisha sana kwa mtoto wako kwani anajaribu kufanya majukumu mapya ambayo huenda yakawa hatari zaidi kwako kumkubalisha. Ila, kwa usalama wake, ni muhimu kuhakikisha usalama nyumbani.

Kadri mtoto wako anavyo anza kuelewa tofauti kati ya mambo-ya kuamini na ukweli, bado atazidi kufurahikia michezo ya kujifanya mara kwa mara.

Tuangazie kwa kina ukuaji na hatua muhimu ambazo mtoto wako anapaswa kuwa akifikisha katika miaka 6 miezi 8.

Miaka 6 miezi 8, Ukuaji na Hatua Muhimu: Je, Mtoto Wako Anakua Ipasavyo?

6 Years 8 Months Old Development and Milestones

Ukuaji wa Kifizikia

Katika umri wa miaka 6 miezi 8, mtoto wako atapata uwezo mwingi wa kifizikia. Kutoka kwa Tae Kwon Do hadi kadanda, kurusha na kushika mpira, mtoto wako anahusika sana. Hii ni kwa sababu ako hai kifizikia.

Uwezo wa mwendo wa kijumla na mwendo hasa utakuwa umeimarika sana katika hatua hii. Kwa sasa, mwendo wa kuanguka anguka ni historia. Mtoto wako anaweza kuruka, kurusha na kushika mpira na hata kutembea. Kwa hivyo unaweza endelea kumpatia mtoto wako fursa ya kujihusisha katika shughuli za kifizikia.

Urefu na uzito wa mtoto wako* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 119.9 cm (47.2 inchi)
  – Uzito: 22.4 kg (49.3 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 119.6 cm (47.1 inchi)
  – Uzito: 22.0 kg (48.5 lb)

Utagundua kuwa mtoto wako anatumia kamba ya kurukia. Huenda hata hata akaweza kujirusha ndani ya mistari ya kuruka. Kadri mtoto wako anavyo zidi kufanya mazoezi ya kutangamanisha mwendo wake, ndivyo anavyokuwa stadi zaidi. Kwa hivyo, usimkubalishe mtoto wako kukata tamaa. Kwa upole, mhimize hadi utakapoona akikuwa bora zaidi.

Katika umri huu mtoto wa miaka 6 miezi 8, anapaswa kuwa na uwezo wa:

 • Kujenga ngazi kwa kukumbuka kutumia maumbo ya kujenga.
 • Kuchora almasi na maombo mengine.
 • Kuandika majina yake, la kwanza na la mwisho.
 • Kuenda na mwendo wa muziki anaosikiza.
 • Kuimarika kwa mwendo wa macho na mikono.
 • Kufuata maagizo ya michezo ya nje kwa makini.
 • Kujivalisha nguo na kufunga kamba za viatu.
 • Kuangalia njia zote mbili mtaani.
 • Kukumbuka kubeba virago vyake anapo toka nje.

Vidokezo

 • Hakikisha kuwa mtoto wako anapata angalau lisaa limoja la michezo ya kifizikia kila siku.
 • Himiza mazoezi kama shughuli ya kifamilia. Kwa sasa, mtoto wako anaweza ruka na anataka kuruka mara kwa mara. Unaweza fanya jambo hili liwe la kupendaza zaidi kwa kuruka pamoja naye.
 • Mhimize mtoto wako kuandika mara kwa mara. Unaweza mhimiza aandike hadithi fupi fupi.
 • Endelea kumsomea mtoto wako na akusomee pia. Unamsaidia kujenga matamshi yake na kuimarisha kutangamana kwa macho na mikono na kukuza mwendo wake hasa.
 • Lingekuwa jambo nzuri pia kupanga herufi baada ya kipindi cha kusoma.
 • Usisahau kumlinda mtoto wako kutokana na ajali kwa kumweka mbali na vifaa vya nyumbani ambavyo ni hatari.
 • Watoto katika umri huu bado wanasoma kuhusu sauti, umbali na spidi. Kwa hivyo, waweke mbali na mitaa. Hawajui hatari za magari na lori.
 • Huu ni wakati muhimu kwa mtoto wako kukuza ujasiri wake katika pande tofauti za maisha yake. Atafanya hivi kwa kupitia marafiki wake, kazi za shuleni na michezo. Unaweza msaidia unapo msifu kwa kufanya jambo.
 • Fanya juhudi za kuenda shuleni ambapo mtoto wako anasomea na kujihusisha katika michezo yake. Ni muhimu kwao kuonyesha kufanikiwa kwao.
Wakati wa Kumwona daktari

Zifuatazo ni ishara kuwa kuna jambo linalo enda mrama katika maisha ya mtoto wako wa miaka 6 miezi 8. Utahitaji kumjulisha mtoto wako iwapo unagundua mambo haya:

 • Bado anakojoa kitandani mara kwa mara, wakati wa mchana ama usiku.
 • Anashindwa kufanya mambo hakuwa anatatizika hapo awali.
 • Haonyeshi hamu ya kuandika majina yake.
Ukuaji wa Kiakili
Your 6 years 8 months old child has an ever-increasing attention span

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 anaendelea kuongeza wakati wake wa kuwa makini. Ana uwezo wa kufikiria kwa umakini, kwa hivyo kuwa tayari kuulizwa maswali mengi. Mtoto wako mara kwa mara anakueleza jinsi anavyohisi kuhusu mada fulani.

Hii ni kwa sababu mtoto wako anaimarisha uwezo wake wa kujieleza. Pia tunaweza sema kuwa mtoto wako anaweza uwezo wa kufikiria sana. Mtoto wako anaanza kuelewa jinsi watu wengine wanavyo maanisha. Huku kunamsaidia kupata marafiki na kupatana na watu wapya.

Na iwapo mtoto wako anakuwa 'mjua yote,' hawako peke yako! Kama mwaka wake wa kwanza wa shule ya msingi unaendelea kuisha, mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 anapaswa kujua:

 • Anaelewa chanzo na athari za uhusiano. Kufikiria kwa kina, hii ni kawaida kwa watoto ila huisha katika umri huu.
 • Anachora mtu wa viungo 12- 14.
 • Kutunga na kuandika hadithi fupi.
 • Kuelewa nambari na kuzisema hadi 20.
 • Anakuza uwezo wake wa kufikiria.
 • Anatoka kusoma kwakuangalia na kushuhudia hadi kwa lugha na kufikiria.
 • Anayataka yote na huenda akatatizika kufanya uamuzi.
 • Kusoma maneno 200.
Vidokezo

Ni muhimu kwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 kuwa na uwezo wa kufikiria ipasavyo katika umri huu.

 • Mhimize mtoto wako kueleza hisia na fikira zake. Unaweza uliza maswali kama vile "Unahisi vipi?" ama "Unafikiria aje?"
 • Mfunze mtoto wako kuwa anapaswa kuheshimu hisia za watu wengine hata anapo zidi kujieleza.
 • Mtoto wako anahitaji kuelewa kuwa hawezi pata mambo yote na anapaswa kujifunza kuchagua. Unaweza mfunza kuhusu kufanya uamuzi mwema.
 • Mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 ana maswali pia, na jambo hili huenda likakufanya ukose utulivu. Ila, kuwa mtulivu na umhusishe kwa kumjibu.
Wakati wa kumwona daktari

Tafadhali tembelea daktari wako unapo gundua kuwa mtoto wako anaonyesha ishara zifuatazo:

 • Ana tatizika kusoma ama ishara za kuwa na ulemavu.
 • Ana onyesha tabia za kikatili kama vile kugonga, kurusha mateke na kuwagwara watu.
 • Ana matatizo ya afya ya kiakili ama kukwazwa.
 • Kutatizika mnapo achana.
 • Anapenda kukaa peke yake wakati wa kucheza.
 • Anajitenga wakati wa shughuli za watu wengi.
Ukuaji wa Kijamii/ Muingiliano na Hisia

 

Play, play play! Group play is a vital part of your child's social development

Cheza, cheza cheza! Michezo ya kimakundi ni muhimu zaidi kwa kila mtoto wa miaka 6 miezi 8 kwa ukuaji wa kijamii wa mtoto wako. Huku ndiko urafiki na utangamano na watu wengine una tengenezwa. Kwa wakati huu, mtoto wako huenda akawa na rafiki wa dhati, kwa wakati mwingi wa jinsia moja.

Kujiamini kwake kunakua, anapozidi kujua zaidi kuhusu urafiki. Tarajia mtoto wako kuhisi ufanikio mkubwa baada ya kushinda mchezo mara ya pili na marafiki wake.

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 pia ata:

 • Anafurahikia kuwa shuleni sana, kwa sababu ya marafiki wake.
 • Anataka kupendeza marafiki wake ili apate kibali chao.
 • Anakua kipekee, ila anahisi hako salama sana.
 • Anataka kusikizwa na walimu na wazazi wake.
 • Ana onyesha wanarika wake upande wake usio mwema, ila ana omba msamaha haraka.
 • Anahitaji kushinda na huenda akageuza maagizo ili yamfurahishe.
 • Anaumizwa na kutokubaliwa, kulaumiwa na kuadhibiwa.
 • Anajua kuwa watu wengine huenda wakawa na hisia tofauti.

Vidokezo

 • Mhusishe mtoto wako katika michezo tofauti. Mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 anapaswa kufurahikia michezo kama vile Nyoka na Ngazi na michezo mingineyo.
 • Unapaswa kufanya urafiki na wazazi wa marafiki wa watoto wako. Kwa njia hiyo, mnaweza kupanga siku za kulala kwa watoto wengine ili kufanya urafiki huu uendelee kupata mizizi.
 • Mhimize mtoto wako kufanya uamuzi kivyake. Jaribu wakati wote kutomfanyia uamuzi.
 • Endelea kumsomea mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 na umhimize akusomee pia.
 • Weka dhibiti kwa kompyuta na runinga.
 • Usiwe na uwoga kuongea na mtoto wako kuhusu mada ngumu kama vile shinikizo la wanarika, utumiaji wa madawa, jinsia. Tafuta njia zinazofaa umri wake kujibu maswali yake bila ya kuongeza uwoga,
 • Mwanzishe mtoto wako darasa za kuogelea na kumfunza mtoto wako usalama wa moto.
 • Mhimize mtoto wako kuona mambo kutoka kwa mtazamo wa watu wengine. Jaribu kuuliza maswali, "Je, unafikiria Yohanna anahisi vipi kuhusu jambo hilo?"
 • Msifu mtoto wako kwa mafunikio yake.
 • Saidia kuimarisha kujiamini na ujasiri wa mtoto wako. Kunasaidia kuwa makini kwa nguvu zake na mambo chanya na kuyatambua.
 • Ibua kufanya mambo kwa kufuata njia mwafaka badala ya kumpuuza. Kama vile, geuza mada badala ya kungoja mada ifike mahali pasipo furahisha.
Wakati wa kumwona daktari

Lazima umtembelee daktari wako iwapo mtoto wako:

 • Anakumbana na matatizo kufuata maagizo.
 • Ana tatizika kufanya urafiki mpya.
 • Ana ukatili na watoto wengine.

your child is quite the little talkative

Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Katika umri wa miaka 6 miezi 8, mtoto wako anaongea sana. Utagundua kuwa anaweza fuata maagizo ya pande tatu. La kufurahisha ni kuwa atabaki kuwa na uwezo wa kufikiria kwa kina. Mtoto wakoa anaweza ongea kuhusu mada ya mazungumzo na kuchukua fursa kuongea.

Mtoto wako wa miaka 6 meizi 8 anauwezo wa kukuangalia usoni bila kuogopa. Anatumia lugha na lengo tofauti kama vile ili kupata ujumbe zaidi, kufurahikia ama kuwafanya wengine waamue. Watoto wa umri huu wana uwezo wa kudhibiti ngeli tofauti (iliyopita, ijayo na ngeli ya sasa).

Utagundua kwamba mtoto wako anaweza kuhadithi ama kupanusha hadithi na kutabiri yatakayo tendeka baada ya hapo. Anafahamu zaidi kuhusu kueleza mhusika fulani ama video ama kujua chanzo na athari za tukio.

Kwa kuongeza, mtoto wako anatambua na kutamka maneno mengi! Matamshi ya jina huenda yakalingana na sauti ambazo maneno hayo huwa nayo. Haya yana tarajiwa na ni sawa.

Mtoto wako anaweza kurudia sentensi 8 hadi 10. Amejua kutofautisha kati ya 'r' na 'l'. Kukufanya umfurahikie zaidi, mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 anajua siku zote za wiki!

Vidokezo
 • Endelea kumsomea mtoto wako. Ni njia bora zaidi ya kukuza matamshi yake na kuongeza idadi ya maneno aliyo nayo.
 • Mara kwa mara, mhimize mtoto wako kukusomea. Mkubalishe akuandikie majina yanayo mfurahisha.
 • Cheza mchezo wa kujua tofauti na umkubalishe mtoto wako aseme tofauti aonayo.
 • Tamka maneno ipasavyo, badala ya kumrekebisha mtoto wako anapokosea kutamka maneno ipasavyo.
 • Himiza ubunifu wa mtoto wako na uwezo wake wa kuandika kwa kusisitiza mchakato huu na sababu ya kuandika badala ya kukazana na kuandika ipasavyo na matamshi.
Wakati wa kumwona daktari

Ongea na daktari iwapo mtoto wako:

 • Ana tatizika kufuata maagizo ya pande mbili, kama vile "Weka mkoba wako mbali kisha uniletee sare yako ya kadanda."
 • Hana hamu yoyote ya kuandika jina lake.
 • Anakataa kusoma.
 • Kuonyesha tabia nyingi zinazo mtatiza.
 • Kushindwa kutofautisha kati ya kushoto na kulia.
 • Anashindwa kutamka hata maneno rahisi.

Eating family meals together will encourage him/her to enjoy a variety of foods.

 Afya na Lishe

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 anahitaji kula vyakula vya afya mara kwa mara kumpatia nishati na virutubisho ili akue na kupigana na magonjwa. Kula lishe kama familia kutamhimiza kufurahikia anuwai kubwa ya vyakula.

Mwanao wa miaka 6 miezi 8 anahitaji angalau kalori 1800 kwa siku. Kula vitamu tamu siku yote badala ya lishe yenye afya kunamfanya kutosawaisha lishe yake. Kuhimiza tabia bora za kula, jaribu kukaa chini na mkule vyakula kama familia. Jaribu kufanya hivi bila usumbufu kama vile televisheni ama michezo ya kompyuta.

Usisahau michezo ya kifizikia. Mtoto wako anahitaji angalau dakika 60 za mazoezi kila siku. Jaribu kuhusisha mazoezi kwenye shughuli za kila siku kama vile kutembea shuleni ama dukani.

Kutembeza mbwa ama kucheza shambani huenda ikawa rahisi zaidi ikilinganisha na kuenda kwa sherehe ama mahali pa kujivinjari. Haya hitaji kujipanga sana na pia ni bure!

Kwa ujumla, kalori zinazo hitajika kwa wavulana na wasichana wa umri huu ni:

 • Wavulana: 1,812 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,700 Kcal/kwa siku

Lishe yao inapaswa kuwa na yafuatayo:

Familia ya maziwa

Mhimize mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 kula na kunywa vyakula vya maziwa vilivyo na idadi ya ufuta wa chini kama vile maziwa ya ng'ombe, maziwa ya bururu (yoghurt), na cheese.

Vyakula hivi vyote vilivyo na calcium ni muhimu kwa lishe ya mtoto wako. Vina saidia kusitiri mifupa na ukuaji wa meno. Vinasaidia mtoto wako anapaswa kunywa angalau ounsi 17 ama 20 za maziwa kila siku.

Familia ya protini

Vyakula vya majini, nyama laini, ndege wa nyumbani, mayai, na njugu. Vyote hivi ni vyakula vya protini na ni muhimu sana katika kuwasaidia watoto wakue na kutengeneza misuli.

Jaribu kuongeza aina tofauti za vyakula vilivyo na protini kwenye lishe ya mtoto wako. Anahitaji angalau granu 36 za protini kila siku.

Familia ya mboga na matunda

Mhimize mtoto wako kukula anuwai ya matunda yaliyo hifadhiwa, kukaushwa ama makopo- badala ya maji ya sharubati. Iwapo mtoto wako anakunywa maji ya sharubati, hakikisha kuwa asilimia 100 bila kuongezwa sukari ama kupunguza idadi unayo mpatia. Mtoto wako wa miaka 6 miezi 8 anahitaji vikombe 3 vya matunda na vikombe 2 vya mboga kila siku.

Mpatie anuwai ya mboga kama vile mboga za kijani, nyekundu na rangi ya machungwa. Husisha maharagwe, kunde na wanga kila wiki.

Nafaka

Unapaswa kumwanzishia mtoto wako nafaka vyema. Unaweza mpatia ounsi 4 za nafaka kila siku. Huenda ikawa ni kikombe kimoja cha cereal zilizo tayari kuliwa, kipande kimoja cha mkate ama nusu kikombe cha pasta ama cereal zilizo pikwa. Hizi zote mara nne kwa siku.

Unaweza chagua nafaka, kama vile oatmeal, quinoa, mkate wa wimbi mzima, popcorn, mchele wa hudhurungi. Ila, hakikisha kuwa unapunguza nafaka zilizo tengenezwa kama vile wali, pasta ama mkate mweupe.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mwanao ya kila siku (tazama hapo juu kuona viwango vinavyo hitajika):

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 32.4 kwa wavulana; gramu 32.4 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Vidokezo: 

 • Weka matundwa yakiwa yameoshwa, kukatwa na kuonekana kwa urahisi kwenye friji.
 • Tengeneza saladi nyingi mara kwa mara. Ikiwezekana kila lishe mbili kwa siku.
 • Jaribu kutengeneza vyakula tofauti vya mboga ama kuongeza mboga kwenye chakula chako.
 • Mara kwa mara, pika mboga badala ya kuweka nyama kwenye chakula chako.
Wakati wa kumwona daktari

Mtembelee daktari wako iwapo mtoto wako,

 • Ana uzito wa chini ama mwingi kupindukia
 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius
 • Ana upele, vidonda ama kugwaruzwa kusiko kwa kawaida
 • Anatapika mara kwa mara baada ya kula

Chanjo na Maradhi ya Kawaida

Nyingi kati ya chanjo za mwanao zinapaswa kuwa zimeisha katika umri huu. Wasiliana na daktari wako kwa chanjo za kawaida ambazo mtoto wako anahitaji kwa sana, kama vile flu shot.

Kadri mtoto wako anavyo kuwa shuleni kwa wakati mwingi, huenda akaugua ama akakosa maradhi ya kawaida kama homa na mafua. Pia, kuwa makini kuona upele unao ibuka kwenye mwili wa mwanao. Na cha muhimu zaidi, mtie moyo akwambie iwapo anahisi kujikuna mwili ama anahisi hayuko sawa.

Ni muhimu kwa wazazi kukumbuka kuwa watoto wote hushuhudia ukuaji tofauti. Kila mtoto ni wa kipekee. Inapofika kwa hatua muhimu, hii ni miongozo tu ila haipaswi kufuatwa kwa umakini.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kutibu matatizo ya kiafya yaliyo kawaida sana kwenye watoto- joto jingi, kukohoa na homa - fuata maagizo haya:

 • Kutibu joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto jingi hadi 38°C (100.4°F), unaweza jaribu matibabu machache ya kinyumbani. Mpake mtoto wako maji ya vuguvugu kwenye kichwa chake, sehemu za siri na makwapa kushusha joto mwilini wake. Iwapo joto ya mtoto wako inapanda zaidi ya 38 degrees unapaswa kumpeleka kwa daktari na ufuate ushauri wa daktari ili kudhibiti afya ya mtoto wako.
 • Kutibu kikohozi: Wakati ambapo kukohoa ni njia ya mwili ya kusafisha koo, iki andamana na homa na kuchemua. Unapaswa kujaribu matibabu ya kinyumbani kama vile tangawizi na asali na uchanganye na maji ya vugu vugu. Mwulize mtoto wako kunywa angalau glasi nane za maji kila siku. Iwapo mtoto wako anakohoa na kuendelea zaidi ya siku tatu ama tano, ama kuanza kuuma anapo kohoa, mpeleke kwa daktari atibiwe na upate ushauri wa kudhibiti hali yake.
 • Kutibu homa: Kwa kawaida, homa inapaswa kuisha baada ya siku chache. Madawa ya kununua ni sawa kukubana na tatizo hili. Homa inasababishwa na virusi na madawa ya kununua hayatasaidia. Iwapo mtoto wako ana homa ama joto jingi, huenda ikawa influenza. Unapaswa kuleta mtoto wako aone daktari.

Ni muhimu kufahamu kuwa iwapo baadhi ya matibabu huenda yakanunuliwa bila ushauri wa daktari, chaguo lako la kwanza kwa matatizo mepesi ya kiafya ni matibabu ya kinyumbani. Kwa mfano, mtoto aliye na homa ama kikohozi anapaswa kupatiwa maji ya vuguvugu. Anapaswa kuweka maji yaliyo pashwa joto na chumvi kisha kutema kabla ya kumeza. Maji yaliyo na chumvi ni bora kusafisha mfumo wa mapua.

Ni muhimu kumhimiza mtoto wako na kumtia nguvu kuzingatia usafi, hasa kunawa mikono ambayo huenda ikasaidia kuepuka kusambazwa kwa maradhi.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius
 • Ana upele, vidonda ama kugwaruzwa kusiko kwa kawaida
 • Kulia mara kwa mara kuhusu kuumwa na mwili ama kichwa
 • Amekuwa akitapika ama kuendesha zaidi ya siku mbili

Mwezi uliopita: 6 years 7 months

Mwezi ujao: 6 years 9 months

Vyanzo: Web MDCDC

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio