Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 10

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 10

Katika makala haya, tuna angazia ukuaji na hatua muhimu katika mtoto wa miaka 6 miezi 10. Tazama iwapo mtoto wako anakua ipasavyo.

Je, mtoto wako mdogo tayari ameanza kufanya majukumu ya mtoto mkubwa. Anapokaribia kufikisha umri wa miaka 7, mtoto wako wa miaka 6 miezi 10 ana ujasiri mwingi na hamu ya kufanya mambo tofauti. Mbali na hayo, ana hamu isiyo isha ya kupata maarifa zaidi.

Utaanza kuona kuwa mtoto wako anakuelezea kwa furaha mambo ambayo yalitendeka shuleni, na kuonyesha kiburi hata kwa mafanikio machache zaidi. Je, una hamu ya kujua zaidi kuhusu unayo yatarajia kutoka kwa mtoto wako katika umri huu? Tupo hapa kwa sababu yako.

Tuna jadili ukuaji wa kijumla wa mtoto wako wa miaka 6 miezi 10, unashauriwa kukumbuka kuwa kila mtoto ni tofauti na atadhihirisha hatua muhimu za ukuaji katika mwendo wake. Una shauriwa kuwasiliana na mtaalum wa afya ya watoto iwapo una shaka zozote.

Ukuaji Na Hatua Muhimu, Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 10: Je, Mtoto Wako Anakua Ipasavyo?

6 years 10 months old child development

Ukuaji wa Kifizikia

Katika umri wa miaka 6 miezi 10, ukuaji wa kifizikia wa mtoto wako (wote wa jumla na hasa) utaendelea kuimarika na kuzidi kuwa bora. Wakati ambapo huenda kukawa na ukuaji katika pande tofauti, urefu wa inchi 2 unatarajiwa kushuhudiwa katika mwaka wote.

Wazazi wanahimizwa kuwasaidia watoto kujihusisha katika shughuli za kijamii na kufanya shughuli za familia kuwa jambo la maisha. Una shauriwa kuwa ni vyema kwa watoto kuhusika katika mchezo maalum. Kwani watoto walio hai huwa bora zaidi katika uwezo wa kifizikia ikilinganishwa na wale wasio jihusisha na michezo.

Watoto wa umri huu wanapaswa kuwa hai kifizikia kwa angalau dakika 6o kila siku kwa siku 5 kila wiki.

Urefu na uzito wa mtoto wako* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 121.0 cm (47.6 inchi)
  – Uzito: 22.8 kg (50.2 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 120.7 cm (47.5 inchi)
  – Uzito: 22.4 kg (49.5 lb)

Mbali na hayo, unapaswa kujua kuwa mtoto wako ana:

 • Usawa bora wa mwili na kutangamana.
 • Uwezo wa kujivalisha nguo na kufunga kamba za viatu zake
 • Kuwa na hali ya utu unao endelea kukua.
 • Meno machache ya uzima.
 • Uwezo ulio imarika wa kuchora na kuandika.
Vidokezo
 • Mpatie mtoto wako majukumu mepesi ya nyumba (kama vile kukusaidia unapo anika nguo kwenye kamba) ambayo yatamsaidia kuimarisha mwendo wake hasa na kumfanya awajibike wakati unapo zidi kupita.
 • Mhimize mtoto wako acheze nje na kuanzisha michezo na majirani na wanarika wake.
 • Kuendesha baiskeli ni njia mwafaka ya kukuza misuli ya mtoto wako na kujenga ujasiri wake wakati huo huo, anapo zidi kuhitimu hadi kwa baiskeli yenye migurudumu miwili. Usisahau kofia ya kumlinda kichwa!
 • Iwapo huja mwanzishia mtoto wako darasa za kuogelea, huja chelewa bado. Uwezo wa kuogelea ni muhimu sana katika maisha yake na ni muhimu zaidi katika kuimarisha uwezo wake wa mwendo wa kijumla.
Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako wa miaka 6 miezi 10,

 • Anapoteza uwezo ambao alikuwa nao hapo awali.
 • Anashindwa kujivalisha nguo peke yake.
 • Hako makini akifanya mambo.
 • Kutatizika anapo soma ama kuwa na uwezo wa chini wa kuona.
Ukuaji wa Kiakili

Katika umri wa miaka 6 miezi 10, akili za mtoto wako zinakaribia kuwa zimekua asilimia 100. Ni muhimu kumpatia mtoto wako lishe zilizo na virutubisho muhimu ili adumishe ukuaji wake wa kifizikia na kiakili.

Katika umri huu, mtoto wako mdogo anaendelea kuwa na hamu zaidi ya kujua zaidi kuhusu dunia inayo mzingira. Mtoto wako anajivunia kuonyesha umaarifa wake na ataongea kwa ujasiri kuhusu mambo anayo yajua na alicho soma shuleni.

Uhuru ni alama ya nguvu katika umri huu. Wakati ambapo ni vyema kukuza uhuru huu kwenye mtoto wako, hakikisha kuwa unakuwa mwangalivu kwani na viwango vilivyo ongezeka vya ujasiri, huenda akajaribu kufanya mambo hatari.

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 10 ana,

 • Uwezo wa hesabu na kusoma unao zidi kuimarika.
 • Kufahamu kuhusu wakati, kuelewa sekundu, dakika, masaa, siku, wiki, miezi na miaka.
 • Kuelewa kuongeza, kutoanisha, na kutumia mambo haya anapofanya hesabu.
 • Uwezo ulio imarika wa kusoma, vitabu vinavyomfaa kwa umri wake.
Vidokezo
 • Endelea kujibu maswali mengi ya mtoto wako, kumhimiza kufikiria kwa umakini uwezapo.
 • Msaidie mtoto wako kutumia umaarifa wake wa kihesabu katika shughuli zake za kila siku. Kwa mfano, unaweza mruhusu mtoto wako kujilipia vitu vichache anavyo nunua sokoni na kuhakikisha anarudishiwa pesa zinazo baki.
 • Mpe mtoto wako vidoli vya STEAM (Science, Tech, Engineering, Arts, Math) kuimarisha ukuaji wake wa kiakili.
 • Mawazo na ubunifu ni njia bora za kuimarisha uwezo wake wa kiakili. Kwa hivyo, endelea na umhimize aanze mradi wa kisanaa ama umwanzishie mtoto wako darasa za kusakata densi.
Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako wa miaka 6 miezi 10,

 • Anashindwa kuwa makini kwa jambo kwa angalau dakika 10.
 • Anatatizika kusoma sentensi rahisi.
 • Anashindwa kufanya hesabu za kimsingi.
 • Anashindwa kufuata ama kuelewa maagizo rahisi ya pande tatu, kama vile, "Tafadhali weka vitabu vyako mbali, kisha unawe mikono na uje tule chajio."
Children at this age are quite sensitive to the feelings and emotions of others
Ukuaji wa Kijamii/Muingiliano na Hisia

Watoto katika umri huu huwa na hisia nyeti na hisia za wengine. Utagundua kuwa mtoto wakoa anakufariji unapo jiumiza. Atafanya juhudi za kuto kuumiza ama wengine.

Anakosa uwoga kuhusu mambo ambayo hapo awali yalikuwa yanamsumbua. Wanaonekana wakifanya urafiki mpya na kupata marafiki wapya mbio. Urafiki na wanarika wao huenda ukawa muhimu zaidi na watoto wa umri huu hupata marafiki wa jinsia sawa. Mtoto wako mdogo anapenda kufurahisha, utamuona akifanya juhudi za kukufurahisha na watu wazima wengine na walimu walio "muhimu."

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 10 ata.

 • Chagua kucheza kwa vikundi vikubwa vya wanarika wake.
 • Kasirika sana unapo mtenganisha na wengine ama kumwadhibu.
 • Kuwa na rafiki wa dhati mmoja ama zaidi.
Vidokezo
 • Mhimize mtoto wako kueleza hisia zake, hasa anapo onyesha ishara za kuwa na hisia hasi kama vile uwoga.
 • Hakikisha kuwa una ukarimu na sifa zako kwa mtoto wako na wakati wote kumhimiza na kupatia ujumbe chanya.
 • Ongoza kwa mfano. Watoto wa umri huu wana uwezo wa kuangalia kwa makini na kufuata tabia zako.
 • Endelea kumsifu mtoto wako kwa mambo mepesi anayofanya vyema, kama vile kuweka vitu mahali panapo faa, kuchukua vidoli vyake na vinginevyo.

Iwapo mtoto wako wa miaka 6 miezi 10,

 • Anakataa kucheza na watoto wengine.
 • Anaonyesha ishara za wasiwasi, kama vile kukataa kuenda shuleni ama kuenda haja ndogo kitandani.
 • Ana ukatili mwingi anapo cheza na watoto wengine.
Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Huu ni wakati ambapo ukuaji wa kasi wa uwezo wa kuongea hukua. Kwa maneno mengine, mtoto wa miaka 6 miezi 10 hukuza matamshi yake na uwezo wa kusoma na kuongeza umaarifa wake wa maneno.

Mtoto wako ataanza kudhihirisha mawazo, ubunifu na uwezo wake wa kuandika maneno magumu.

Utagundua kuwa mtoto wako ana uwezo wa kuunda sentensi ndefu zilizo ngumu kidogo zenye maneno makubwa. Huenda akajaribu kutumia maneno aliyo yasoma.

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 10 ana uwezo wa,

 • Kukwambia wakati na kutaja siku na miezi vizuri.
 • Kueleza usawa kati ya vyombo viwili.
 • Kueleza matukio yaliyo tendeka hapo awali kwa kufuata yalivyo tendeka.
 • Kuwa na mjadala na sababu mwafaka.
Vidokezo
 • Mwanzishe mtoto wako kwenye vilabu vya maktaba na vya kusoma.
 • Mhimize kusoma kwa kumwanzishia mtoto wako vitabu vinavyo mfurahisha kisha vya utafiti.
 • Tenga wakati zaidi msome pamoja.
 • Mpatie fursa za kuandika hadithi za kubuni na umhimize atie mawazo yake anapo andika.
Wakati wa kumwona daktari

Huenda ukahitajika kuongea na daktari wako iwapo mtoto wako wa miaka 6 miezi 10 ana,

 • Dhihirisha matatizo ya mazungumzo kama vile kugugumaa.
 • Hawezi tumia sentensi iliyo kamili kuelezea matukio.
 • Anakataa kuandika ama kusoma.
Afya na Lishe

health and nutrition

Huu ni umri ambao uwezo wa kifiziki, kijamii na kiakili wa mtoto wako hukua. Ni muhimu kuhimiza ukuaji huu na virutubisho mwafaka zaidi. Na anuwai ya chaguo zilizoko kwenye soko leo, kuchagua chakula kinacho faa kwa ukuaji wa mtoto wako ni muhimu.

Katika umri wa miaka 6 miezi 10, mtoto wakoa anahitaji kalori 1700 ama 1830 kwa siku kumpatia nishati mwafaka za ukuaji na maendeleo.

 • Wavulana: 1,826 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,714 Kcal/kwa siku

Hapa chini kuna mwongozo wa kukusaidia kusambaza virutubisho hivi kwa kuongeza aina ya vyakula hivi kwenye lishe ya mtoto wako.

Nafaka

Kama vile oats, barley na mchele na vyakula vinavyo tengenezwa kutokana na vitu hivi kama vile mkate. Hakikisha kuwa unakula nafaka nzima  ili kuboresha mfumo mwema wa utumbo.

Mtoto wako anahitaji angalau ounsi 4 za chakula zinazo hitaji nafaka kila siku, kama vile mkate kipande kimoja ama kikombe cha pasta, cereal ama mchele. Angalau nusu ya vyakula vya nafaka vya mtoto wako vinapaswa kuwa kutokana na nafaka nzima.

Matunda na mboga

Habari njema ni kuwa mtoto wako hakasiriki kula mboga na matunda kama mwaka uliopita. Mpe anuwai ya vitamini na madini yanayo hitajika kwa ukuaji wa afya wa mtoto wako. Ni muhimu kuhakikisha kuwa mtoto wako anakula mchanganyiko wa matunda na mboga kila siku.

Mtoto wako mdogo anahitaji kuwa akila angalau mboga ya machungwa, ya rangi ya kijani na yenye matawi mengi kila siku.

Mtoto wako anahitaji kula angalau matunda na mboga mara mbili kwa siku, kila mara ikiwa angalau nusu kikombe.

Maziwa

Vyanzo vya maziwa na vyakula vinavyo tengenezwa kutokana na maziwa viko katika familia hii. Ni vyema kumpatia mtoto wako bidhaa zilizo na ufuta wa chini na vyenye viwango vya juu vya kalisi.

Mtoto wako anahitaji angalau ounsi 17 hadi 20 za maziwa kila siku, vinapaswa kuwa ifuatavyo: maziwa- kikombe kimoja, cheese- gramu 50, maziwa ya bururu- 3/4 kikombe ama saizi ya mpira wa tenisi.

Protini

Mtoto wako anayekua anahitaji protini kumsaidia kukuza na kutengeneza celi na homoni na pia kumpa nashati.

Vyanzo bora vya protini ni kama vile nyama, samaki, njugu, kunde na maharagwe. Hakikisha unaziongeza kwenye lishe ya mtoto wako.

Katika umri huu, mtoto wako anahitaji gramu 36 za protini kila siku, kwa mfano: saizi ya mkono wa kike wa kipande cha kuku, nyama ya ng'ombe, ama samaki na mayai mawili, tofu  na maharagwe.

Vidokezo
 • Mpatie mtoto fursa ya kukusaidia kutengeneza lishe kwa kuhusisha maoni yake.
 • Mhusishe mtoto wako katika kutayarisha na kutengeneza vyakula.
 • Weka chakula mezani na sio mbele ya televisheni ama vifaa vyoyote vitakavyo mfanya kuto kuwa makini na chakula chake. Wanajamii wanapokuwa nyumbani, hakikisha mnakula kama familia wakati wote.
 • Punguza vyakula vilivyo chakatwa ama vya sukari wakati wote.
 • Mhimize mtoto wako kunywa maji mengi siku yote.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mwanao ya kila siku:

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 36 kwa wavulana; gramu 36 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)
Wakati wa kumwona daktari

Mtembelee daktari wako iwapo mtoto wako,

 • Ana onyesha ishara za mzio kama vile kufura ama kutoa machozi.
 • Kuendesha zaidi ya siku mbili.
 • Kuumwa na tumbo mara kwa mara.
 • Kuongeza ama kupoteza kilo kusiko kwa kawaida.

Chanjo na Maradhi ya Kawaida: Mtoto wako wa miaka 6 miezi 10

Nyingi kati ya chanjo za mwanao zinapaswa kuwa zimeisha katika umri huu. Walakini, hakikisha kuwa ratiba ya chanjo za mtoto wako zimeafikiana. Ratibisha chanjo zijazo kwenye kalenda yako ya kibinafsi. Ni muhimu kuweka kumbukumbu za tarehe hizi.

Wakati ambapo homa, joto jingi na kikohozi huwa kawaida katika watoto wa umri huu, una shauriwa kuwasiliana na daktari wako kwa chanjo za kawaida ambazo mtoto wako anahitaji kwa sana, kama vile chanjo dhidi ya flu.

Iwapo unapanga kusafiri, ni muhimu kuangalia mahitaji ya chanjo na pia kuangalia taarifa za afya kuhusu nchi unazo panga kutembelea.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kutibu matatizo ya kiafya yaliyo kawaida sana kwenye watoto- joto jingi, kukohoa na homa - fuata maagizo haya:

 • Kutibu joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto jingi hadi 38°C (100.4°F), unaweza jaribu matibabu machache ya kinyumbani. Mpake mtoto wako maji ya vuguvugu kwenye kichwa chake, sehemu za siri na makwapa kushusha joto mwilini wake. Iwapo joto ya mtoto wako inapanda zaidi ya 38 degrees unapaswa kumpeleka kwa daktari na ufuate ushauri wa daktari ili kudhibiti afya ya mtoto wako.
 • Kutibu kikohozi: Wakati ambapo kukohoa ni njia ya mwili ya kusafisha koo, iki andamana na homa na kuchemua. Unapaswa kujaribu matibabu ya kinyumbani kama vile tangawizi na asali na uchanganye na maji ya vugu vugu. Mwulize mtoto wako kunywa angalau glasi nane za maji kila siku. Iwapo mtoto wako anakohoa na kuendelea zaidi ya siku tatu ama tano, ama kuanza kuuma anapo kohoa, mpeleke kwa daktari atibiwe na upate ushauri wa kudhibiti hali yake.
 • Kutibu homa: Kwa kawaida, homa inapaswa kuisha baada ya siku chache. Madawa ya kununua ni sawa kukubana na tatizo hili. Homa inasababishwa na virusi na madawa ya kununua hayatasaidia. Iwapo mtoto wako ana homa ama joto jingi, huenda ikawa influenza. Unapaswa kuleta mtoto wako aone daktari.

Ni muhimu kufahamu kuwa iwapo baadhi ya matibabu huenda yakanunuliwa bila ushauri wa daktari, chaguo lako la kwanza kwa matatizo mepesi ya kiafya ni matibabu ya kinyumbani.

Kwa mfano, mtoto aliye na homa ama kikohozi anapaswa kupatiwa maji ya vuguvugu. Anapaswa kuweka maji yaliyo pashwa joto na chumvi kisha kutema kabla ya kumeza. Maji yaliyo na chumvi ni bora kusafisha mfumo wa mapua.

Ni muhimu kumhimiza mtoto wako na kumtia nguvu kuzingatia usafi, hasa kunawa mikono ambayo huenda ikasaidia kuepuka kusambazwa kwa maradhi.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius.
 • Ana upele, vidonda ama kugwaruzwa kusiko kwa kawaida.
 • Ana uzito mwingi zaidi ama mdogo zaidi wa umri wake.
 • Anakataa kukula ama kupoteza hamu yake mara kwa mara.

Mwezi uliopita: 6 years 9 months

Mwezi ujao: 6 years 11 months

Vyanzo: Mayo ClinicCDC, Web MD , Alberta Health Services

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio