Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 11: Ukuaji Na Hatua Muhimu

Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 11: Ukuaji Na Hatua Muhimu

Katika umri wa miaka 6 miezi 11, mtoto wako mchanga anaendelea kusoma mambo mapya kuhusu dunia anayo ishi. Ni jukumu lako kumlinda katika ukuaji huu.

Hongera mama! Mtoto wako mdogo kwa sasa ana miaka 6 miezi 11, na kuna uwezekano mkubwa unafurahikia wazo la kusherehekea kuzaliwa kwake kwa mwaka wa saba! Katika hatua hii, mtoto wako amesoma mambo mengi na ana uwezo wa kuyatenda mengi.

Mtoto wako mdogo atakuwa makini sana kuyaangalia mazingira yake na kusoma zaidi kuhusu dunia. Huku kuna maana kuwa unapaswa kuwa mwangalifu zaidi na usalama wa mtoto wako.

Tuna angazia kwa kina ukuaji na maendeleo muhimu katika mtoto wako wa miaka 6 miezi 11.

Ukuaji na Maendeleo muhimu kwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 11: Mtoto wako anakua ipasavyo?

miaka 6 miezi 11

Ukuaji wa Kifizikia

Katika umri wa miaka 6 miezi 11, mtoto wako ameshuhudia ukuaji mwingi katika fizikia yake. Huenda akawa na hamu ya kujiunga na michezo tofauti kwani uwezo wake wa mwendo umeimarika katika hatua hii.

Katika wakati huu, mtoto wako mchanga anakua urefu wa inchi 2.5 ama sentimita 6-7 kila mwaka. Kwa upande wa uzito, mtoto wako ataongeza kilo 2-3 kila mwaka hadi atakapo fikisha ujana wake.

Huenda ukagundua kuwa kwa sasa, mwendo wake umeimarika sana, anaweza kushika mpira bila tatizo lolote. Katika mwaka huu, baadhi ya watoto hujua jinsi ya kuendesha baiskeli kwani wana uwezo wa kusawasisha vitu!

Uwezo huu wote wa kifizikia unawezekana kwa sababu ya mwili wa mtoto wako unao endelea kukua. Katika hatua hii, urefu na uzito wa mtoto wako* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  - Urefu: 121.5 cm (47.8 inchi)
  - Uzito: 23 kg (50lb)
 • Wasichana
  - Urefu: 121.2 cm (47.7 inchi)
  - Uzito: 22.7 kg (49.9lb)

Huu pia ni wakati mzuri kumhusisha mtoto wako katika kazi za kifizikia. Hii ni hatua muhimu, na kuhusika na kumhimiza mtoto wako kwenda nje na kucheza kunaweza msaidia kuwa na uzito ulio sawa na kuwa na afya.

Katika umri huu, mtoto wako wa miaka 6 miezi 11 anapaswa kufanya:

 • Kushika mpira kwa urahisi na utangamano mwema kati ya mikono na macho.
 • Kusawasisha vitu kwa urahisi na ana uwezo wa kujua mambo kama kuendesha baiskeli.
 • Kusakata densi kulingana na muziki.
 • Kukimbia kwa urahisi, kuruka na kupanda.
 • Kujifunza jinsi ya kuogelea bila kutatizika.
 • Kuruka kamba.
 • Kuandika jina lake wa njia inayo someka, na kuchora kwa urahisi.
Vidokezo
 • Make physical activity a top priority not just for your little one, but also for the family. This is a crucial stage in your child's life, and exercising with the family can establish good healthy habits in your child.
 • Hakikisha kuwa unaweka shughuli za kifizikia sio kwa mtoto wako mdogo tu, ila kwa familia kwa ujumla. Hii ni hatua muhimu kwenye maisha ya mtoto wako.
 • Mhimize mwanao ajiunge na michezo shuleni kuimarisha kutangamana na watu wengine.
 • Hakikisha unamlisha mtoto wako vyakula vya afya kama vile matunda na mboga na protini ili kukuza ukuaji na maendeleo ya misuli yake.
 • Jaribu kupunguza wakati wa mtoto wako wa kutazama runinga na uhakikishe kuwa hauingilii wakati wa familia ama wa kufanya mazoezi.
 • Mkubalishe mwanao achezee nje na pia kucheza na marafiki wake.
Wakati wa Kumwona Daktari

Zifuatazo ni ishara katika mtoto wako wa miaka 6 miezi 11 kudhihirisha kuwa huenda akawa na tatizo. Iwapo utagundua kuwa mtoto wako ana mojawapo ya yafuatayo, usisite kuongea na daktari wako kuhusu jambo hilo.

 • Kutatizika kushika kalamu ama kuandika jina lake vyema.
 • Matatizo ya kutangamanisha mikono na macho.
 • Ana matatizo na kazi za kifizikia ama kutatizika kujihusisha na michezo
Ukuaji wa Kiakili

 

miaka 6 miezi 11

Katika hatua hii, ukuaji wa akili wa mtoto wako unaanza kuwa wa kasi zaidi. Huenda ukagundua kuwa uangalifu wake umeongezeka sana, na kuna maana kuwa mtoto wako ataanza kuwa makini na kazi tofauti bila ya kupoteza umakini wake.

Kwa umri wa miaka 6 miezi 11, mtoto wako ni mwangalifu kwa kila kitu na huenda atapendezwa sana na mambo madogo. Huku pia kuna maana kuwa utaulizwa maswali mengi kila wakati, wa hivyo, kuwa tayari kuyajibu!

Atakuwa na uwezo mwema zaidi wa kujieleza, na hutakosa kuwaona watoto wa umri huu wakijieleza na kusema kilicho akilini mwao kila mara. Ni wakati huu pia ambao mtoto wako anapata marafiki wengi na pia kuongea na watu kwa u-huru.

Kama mwaka wake wa kwanza katika shule ya msingi unakaribia kuisha, mtoto wako wa miaka 6 miezi 11 anapaswa kuwa na uwezo wa:

 • Kuingiliana vyema na watu na kufanya urafiki.
 • Kukwambia wakati.
 • Anaweza soma sentensi rahisi.
 • Uwezo wa kuelewa mambo kama maisha na kifo.
 • Ana anza kuwa mwangalifu kwa mazingira yake.
 • Uwezo wa kumaliza puzzle rahisi.
 • Anaanza kuuliza maswali kuhusu vitu tofauti na kueleza hisia zake kuhusu mada tofauti.
Vidokezo

Katika umri wa miaka 6 miezi 11, ni muhimu kuhimiza uwezo wa kufikiria kwa makini kwa mtoto wako. Hapa ni baadhi ya njia za kufanya hivi:

 • Mhimize mtoto wako kueleza hisia na maoni yake kuhusu dunia.
 • Kuwa msikilivu anapo kuhadithia kuhusu siku yake shuleni, mwulize maswali ili kuhimiza kufikiria kwa umakini.
 • Mtoto wako wa miaka 6 miezi 11 atakuwa anakuuliza maswali mara kwa mara. Kwa hivyo kuwa na uhakika kutulia na kujaribu kuelewa kuwa hii ni njia yake ya kuelewa dunia inayo mzingira.
 • Ana uwezo wa kuongeza na kutoanisha hadi 20 kwa urahisi.
 • Ongea na walimu wa watoto wako ili ujue jinsi anavyo kuwa anapokuwa shuleni, na ili upate sehemu ambazo unapaswa kufanyia kazi na mtoto wako.
Wakati wa kumwona daktari

Tafadhali tembelea daktari wako iwapo unagundua kuwa mtoto wako anadhihirisha dalili zifuatazo:

 • Iwapo mtoto wako anatatizika kuhesabu, ama anashindwa kusema wakati.
 • Anadhihirisha kukosa hamu ya kujua, ama kuonekana hana hamu ya kujua mazingira yake.
 • Ana matatizo kuelewa baadhi ya vitu.
 • Kushindwa kujieleza kwa kutumia maneno ama kutatizika kuongea.
 • Ukuaji wake bado hauja imarika kutoka alipokuwa miaka 6.
 • Bado ana matatizo ya kuongeza ama kutoanisha nambari ndogo.
Ukuaji wa Kijamii na Hisia

 

miaka 6 miezi 11

Huenda ukagundua kuwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 11, anataka kuwa huru zaidi. Ameanza kuwa huru zaidi na marafiki wake. Sio jambo lisilo la kawaida kuona mtoto wako akitaka kutumia wakati mwingi akicheza peke yake ama kutaka muda wa kuwa peke yake.

Ujasiri wake unaongezeka katika umri huu, na anaanza kuwa hai katika kufanya marafiki wapya shuleni na nyumbani. Wakati mwingi, wavulana watapenda kuwa miongoni mwa wavulana na wasichana watataka kuwa na wasichana wengine, ila sio jambo lisilo la kawaida kuona vikundi vya watoto walio ingiliana wakicheza pamoja.

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 11 anapaswa kuwa na uwezo ufuatao:

 • Kuwa na uwezo wa kufanya kazi vyema na watoto wengine, na kucheza na watoto wengine kutakuwa na furaha zaidi kuliko kucheza peke yake.
 • Ataongea mara kwa mara na wanarika wake, na ataanza kujua jinsi ya kuingiliana na kuishi na watu wengine.
 • Anataka kuwa huru zaidi, kwa hivyo ni wakati mwema kumruhusu kujua zaidi kuhusu dunia na kusoma mambo kwa kipekee.
Vidokezo
 • Mruhusu mtoto wako kufanya uamuzi wake, kwa hivyo asome jinsi ya kufanya uamuzi na kuchukua majukumu kwa uamuzi alio fanya.
 • Mhimize mtoto wako kuongea na watoto wengine. Usimkataze kuingiliana na watoto wa jinsia tofauti kwani kuwa na kundi la jinsia tofauti ni vyema kwa ukuaji wa muingiliano na kijamii wa mtoto wako.
 • Weka mazungumzo yaliyo huru na mtoto wako. Huenda mtoto wako akawa huru, ila, bado atahitaji mapenzi na uangalifu wako.
 • Watoto katika umri huu huenda wakaanza kuongea uongo, kudanganya ama kuiba. Kuwa na uhakika wakuwajulisha tofauti kati ya mbaya na nzuri na kuwa kuna adhabu ya matendo yao.
 • Kuwa hakika kumpa mtoto wako wakati tosha wa kupumzika na usimtie mkazo mwingi inapofika wakati wa kufanya kazi yake ya ziada.
Wakati wa kumwona daktari

Lazima umtembelee daktari wako iwapo mtoto wako:

 • Ana matatizo kuingiliana, ama ana wakati mgumu kupata marafiki.
 • Hataki kuwa huru, ama wakati wote anapenda kukaa kwenye upande wako.
 • Anatatizika kueleza hisia zake ama ana wakati mgumu kusema kuhusu hisia zake.
Ukuaji wa Lugha na Mazungumzo

 

miaka 6 miezi 11

Katika miaka 6 miezi 11, sio jambo lisilo la kawaida kusikia mtoto mara nyingi akiongea kuhusu mambo tofauti. Huenda akaongea kuhusu shule, michezo ama kucheza ama anafikiria kuhusu runinga anayo tazama.

Mtoto wako pia ana uwezo wa kuongea vyema katika hatua hii, na kueleza hisia tofauti. Huenda ukajipata ukitaka amani na kunyamaza kwa sababu mtoto wako anaongea sana!

Uwezo wake wa kusema maneno umeimarika kwa sana katika wakati huu, na anapaswa kuweza kuandika sentensi rahisi bila kutatizika sana.

Hapa ni baadhi ya mambo ambayo mtoto wako wa miaka 6 miezi 11 anapaswa kuwa anafanya:

 • Anaweza elewa na kusema ucheshi.
 • Anaweza zungumza kwa urahisi, na wakati wote ana hamu ya kupeana hadithi mpya.
 • Hamu ya kusoma maneno mapya, na wakati wote ana kuza matamshi yake.
 • Anaelewa maagizo, na hana taabu kufanya anacho ambiwa afanye.
Vidokezo
 • Msomee mtoto wako vitabu mara kwa mara. Vitabu ni marafiki wa dhati wa mtoto wako, na ni wazo njema kumfanya apende kusoma.
 • Mhimize kutumia maneno mapya na usi aibike kumwanzishia mtoto wako majina magumu.
 • Watoto wa umri huu huenda wakaanza kuuliza majina "mabaya" kwa hivyo kuwa tayari kuongea na mtoto wako kuhusu kwa nini maneno haya yana paswa kuepukwa.
 • Unaweza mfunza mtoto wako mdogo kuanza kitabu chake (diary), na kuimarisha uwezo wake wa kuandika, ubunifu na kumbukumbu.
Wakati wa kumwona daktari

Ongea na daktari iwapo mtoto wako:

 • Ana tatizika kufuata maagizo mepesi.
 • Ana matatizo kuongea ama kusema maneno mepesi.
 • Kutatizika kusoma, ama anapo soma maneno mepesi.
 • Anabaki nyuma shuleni.
Lishe na Afya

 

miaka 6 miezi 11

Katika umri wa miaka 6 miezi 11, lishe ya mtoto wako mdogo inapaswa kuwa imejaa vyakula vyenye afya. Kukula vyakula vyenye afya kuna imarisha ukuaji na maendeleo katika mtoto wako na kuuweka katika mwendo unaofaa.

Wavulana na wasichana katika umri huu wanapaswa kuchukua viango vifuatavyo vya kalori:

 • Wavulana: 1,835 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,721 Kcal/kwa siku

Hii ndiyo sababu kwa nini ni vyema kuhakikisha kuwa lishe ya mtoto wako imejazwa na vitamu tamu vya afya. Walakini, hakikisha kuwa kumlishi vitamu tamu vingi kwani huenda vikaharibu hamu yake ya kula.

Kama kawaida, mazoezi ni muhimu sana katika ukuaji wa mtoto wako. Kuna saidia mtoto wako kuwa na afya na nguvu.

Inapofika kwa lishe ya mwanao, hapa ni vitu unavyo hitaji:

Kikundi cha maziwa

Bidhaa za maziwa ni muhimu katika ukuaji wa mtoto wako kwani ina kalisi inayo saidia katika ukuaji wa mifupa na meno. Walakini, baadhi ya bidhaa za maziwa zina ufuta mwingi ambao huenda ukawa mbya kwa afya ya mtoto wako.

Kuwa haki kumpa mwanao maziwa yenye ufuta mdogo, cheese na vyakula vingine vya maziwa vilivyo na afya. Katika hatua hii, mtoto wako anahitaji angalau ounsi 17 ama 22 za maziwa kila siku.

Mtoto wako anahitaji vikombe 2 vya maziwa, ounsi 1 ya cheese ama kikombe 1 cha maziwa ya bururu.

Kikundi cha protini

Protini ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto wako kwani zina saidia katika ukuaji wa misuli na kuitengeneza. Vyakula kama cheese, njugu, nyama, samaki na maharagwe ni vyanzo vyema vya protini vya ukuaji wa mtoto wako.

Mtoto wako anahitaji chaula chenye protini angalau mara mbili kwa siku kila lishe ikiwa na ounsi 2-3 za nyama, 1/2 kikombe cha maharagwe iliyopikwa, 1-2 mayai kwa kila lishe.

Kikundi cha mboga na matunda

Mlishe mwanao vikombe 3 vya matunda na yaliyo safi ni bora kwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 11. Matunda yaliyo toka shambani yana fiber nyingi inayo msaidia anapokula. Ina vitamini na virutubisho vingi vinavyo saidia kuimarisha afya ya mtoto wako na mfumo wake wa kinga.

Mboga ni muhimu katika ukuaji wa mtoto wako na lishe za mtoto wako zinapaswa kuwa na mboga nyingi. Mtoto wako anahitaji vikombe viwili vya mboga angalau mara 3 kila siku na kiwango kikubwa cha mboga zilizo pikwa, kikombe 1 cha salad katika kila lishe.

Nafaka

Katika hatua hii, mtoto wako anapaswa kula ounsi 4 za nafaka kila siku. Huenda ikawa ni kikombe kimoja cha cereal zilizo tayari kuliwa, kipande kimoja cha mkate ama nusu kikombe cha pasta ama cereal zilizo pikwa. Hizi zote mara nne kwa siku.

Unaweza chagua nafaka, kama vile oatmeal, quinoa, mkate wa wimbi mzima, popcorn, mchele wa hudhurungi. Ila, hakikisha kuwa unapunguza nafaka zilizo tengenezwa kama vile wali, pasta ama mkate mweupe.

Vidokezo
 • Weka matunda mengi kwa nyumba ili umpatie mtoto wako badala ya vitamu tamu.
 • Mboga zinapaswa kuwa nyingi kwenye lishe ya mtoto wako.
 • Mara kwa mara, tumia protini za mimea kuliko za wanyama unapo kitengeneza chakula kama vile maharagwe ama njugu.
 • Kuza tabia nzuri za kukula katika hatua hii, ili mtoto wako aige tabia hizi hata ukubwani wake.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mwanao ya kila siku:

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 36 kwa wavulana; gramu 36 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)
Chanjo na Magonjwa ya kawaida

Mtoto wako atakuwa amepata nyingi kati ya chanjo zake katika umri huu. Ila, iwapo kisa ni tofauti na haya, tunge kushauri kuwasiliana na daktari wako ili mtoto wako apate zilizo baki kwa kawaida.

Japo mtoto wako anapokuwa shuleni wakati mwingi, huenda akaugua homa ya kawaida ama mafua. Kwa hivyo, kuwa mwangalifu kuona upele, joto jingi ama kujikuna ambako huenda kukaongezeka na kuwa kuumwa na mwili. Mhimize mtoto wako kukueleza anacho hisi na ikiwa hahisi vyema, mpeleke hospitalini iwapo hauna uhakika kuhusu chanzo.

Kama kumbusho, hizi ni chanjo ambazo mtoto wako anapaswa kuwa amepata katika umri huu:

Walakini, hata na rekodi zilizo kamilika, mtoto wako huenda bado akapata homa, mafua ama magonjwa ya kawaida kama Hand and Mouth disease. Iwapo mtoto wako anadhihirisha ishara za kuto kuwa na starehe, kutapika na kuendesha ama joto jingi ( zaidi ya 38°C/100.4°F), wasiliana na daktari wako.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kutibu matatizo ya kiafya yaliyo kawaida sana kwenye watoto- joto jingi, kukohoa na homa - fuata maagizo haya:

 • Kutibu joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto jingi hadi 38°C (100.4°F), unaweza jaribu matibabu machache ya kinyumbani. Mpake mtoto wako maji ya vuguvugu kwenye kichwa chake, sehemu za siri na makwapa kushusha joto mwilini wake. Iwapo joto ya mtoto wako inapanda zaidi ya 38 degrees unapaswa kumpeleka kwa daktari na ufuate ushauri wa daktari ili kudhibiti afya ya mtoto wako.
 • Kutibu kikohozi: Wakati ambapo kukohoa ni njia ya mwili ya kusafisha koo, iki andamana na homa na kuchemua. Unapaswa kujaribu matibabu ya kinyumbani kama vile tangawizi na asali na uchanganye na maji ya vugu vugu. Mwulize mtoto wako kunywa angalau glasi nane za maji kila siku. Iwapo mtoto wako anakohoa na kuendelea zaidi ya siku tatu ama tano, ama kuanza kuuma anapo kohoa, mpeleke kwa daktari atibiwe na upate ushauri wa kudhibiti hali yake.
 • Kutibu homa: Kwa kawaida, homa inapaswa kuisha baada ya siku chache. Madawa ya kununua ni sawa kukubana na tatizo hili. Homa inasababishwa na virusi na madawa ya kununua hayatasaidia. Iwapo mtoto wako ana homa ama joto jingi, huenda ikawa influenza. Unapaswa kuleta mtoto wako aone daktari.

Ni muhimu kufahamu kuwa iwapo baadhi ya matibabu huenda yakanunuliwa bila ushauri wa daktari, chaguo lako la kwanza kwa matatizo mepesi ya kiafya ni matibabu ya kinyumbani.

Kwa mfano, mtoto aliye na homa ama kikohozi anapaswa kupatiwa maji ya vuguvugu. Anapaswa kuweka maji yaliyo pashwa joto na chumvi kisha kutema kabla ya kumeza. Maji yaliyo na chumvi ni bora kusafisha mfumo wa mapua.

Ni muhimu kumhimiza mtoto wako na kumtia nguvu kuzingatia usafi, hasa kunawa mikono ambayo huenda ikasaidia kuepuka kusambazwa kwa maradhi.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius ama joto jingi zaidi ya wiki moja.
 • Ana upele, vidonda ama kugwaruzwa kusiko kwa kawaida.
 • Ana uzito mwingi zaidi ama mdogo zaidi wa umri wake.
 • Anakataa kukula ama kupoteza hamu yake mara kwa mara.

Mwezi uliopita: Child development and milestones: Your 6-years-10-months-old

Vyanzo: Web MDCDC, Kid Central TN

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio