Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 7

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 7

Bila shaka kulea mtoto wako ni jambo la kufurahikia. Ila, kuwa tayari kwani mtoto wako wa miaka 6 miezi saba ana nishati zaidi.

Mwaka wa kwanza  wa mtoto wako shuleni huwa na matukio mengi sana sio kwake pekee mbali kwako pia. Itabidi umezoea kuwa mbali na yeye kwa masaa mengi . Lakini katika miaka 6 miezi 7 ushazoea hili.

Wataalam hukitambua hiki kipindi katika maisha ya mtoto kama “kipindi cha kati cha utotoni”. Mdogo wako wa miaka sita miezi saba anaanza kutaka kuwa huru kwa upande mmoja. Lakini kwa upande mwingine bado anahitaji usalama kutoka kwa huu ulimwengu mkubwa. Hiki ni kitu ambacho wewe pekee ndio unaweza kumpa.

Michezo anayojihusisha nayo sasa ni ya utata. Hiki kipindi kikilinganishwa na vingine ndio huiga mambo anayoyaona kwa vitabu ama televesheni. Kwa mfano wakati wa mchana atamwiga ninja na wakati wa jioni atakuwa mwimbaji wa nyimbo za injili.

Ana nishati nyingi na hujihusisha kwa michezo yenye ucheshi kila siku. Itakuwa jukumu lako kuhakikisha kuwa mwili wake unabakia wenye nguvu na afya bora. Wacha tuangazie hatua zingine unafaa kutarajia katika huu mwaka.

Ukuaji na Hatua Muhimu Za Mtoto Wa Miaka 6 Miezi 7: Je, Mtoto Wako Anakua Ipasavyo?

 

miaka 6 miezi 7

Ukuaji wa Kifizikia

Inaonekana kwa usiku mmoja tu mtoto wako amegeuka kutoka kwa mtoto mchanga kuwa anayeenda shule mwenye nishati na nguvu nyingi. Mikono na miguu ya mtoto wako inaonekana kuwa inakua kwa haraka sana. Anakua kwa kiasi cha inchi 2.5 ama sentimeta 6 kila mwaka na pia anaongeza uzani wa kilo 3 kila mwaka.

Katika miaka sita miezi saba urefu wa wastani wa mtoto wako* na uzani wake unafaa kuwa hivi:

 • Wavulana
  – Urefu: 119.4 cm (47.0 inchi)
  – Uzito: 22.2 kg (48.9 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 119.0 cm (46.9 inchi)
  – Uzito: 21.8 kg (41.0 lb)

Katika huu umri, mtoto wako anaweza furahia kujipima uwezo wake  kama vile,  kukimbia kwa njia iliyo na kigezo, kuruka kwenye ngazi ama kufanya mapindu.

Pia utaweza kugundua anakuwa sawa katika kujumuisha mambo yanayohusisha kukimbia kama vile kukimbia kugonga mpira ama kuruka kama anapinda kamba.  Haya maarifa ya kimwili yatategemea uzeofu wake katika kuyafanya.  Michezo iliyo na mtindo kama vile madarasa ya densi, tenisi, na mpira wa miguu yote inaweza kusaidia. Lakini fursa nyingi za kukimbia, kupiga, kurusha , kufanya mapindu na mengineo pia ni muhimu.

Maarifa ya mtoto wako ya kutembea imekua vizuri sasa.  Anaweza kuyasugua meno yake na kufanya mambo mengine ya usafi wake bila usaidizi wako. Pia utagundua mtoto wako anaweza kukata vipande vya karatasi visivyo na umbo shwari  na kuandika herufi ndogo katikati ya nafasi katika vitabu vyake vya shuleni.

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 7 pia atakuwa anashuhudia haya:

 • Ataanza kuwa makini kwa sura yake
 • Meno ya kwanza itangoka ikijitayarisha kwa mengine kumea
 • Anaonyesha uwezo katika maarifa nyingi ya kimwili
 • Misuli itaongezeka mizani na itaonekana kwa ujumla katika uzito wake
 • Anaweza kuwa na uwezo wa kuona wa 20/20
 • Ana nguvu nyingi kupita kiasi
 • Anaweza kuzingatia kanuni za michezo kwa urahisi
Vidokezo
 • Mtoto wako atahitaji michezo mingi sana
 • Himiza mtoto wako kucheza uwanjani
 • Cheza naye pia. Jihusishe na kuruka , kugonga na kurusha. Sio tu mazoezi kwako mbali wakati wa kujenga uhusiano wewe na yeye. Kwa kufanya vile pia utamsaidia kujenga imani yake
 • Mwangalie mtoto wako anapojihusisha kwenye michezo hatari kama vile kupanda.
 • Zungumza na mtoto wako jinsi ya kuitisha usaidizi anapouhitaji
 • Weka vitu vya nyumbani, vifaa na bunduki vinavyoweza kumdhuru mbali na yeye.

Wakati Wa Kumwona Daktari

Kuwa mwangalifu kwa ishara hizi. Zinaweza kuwa zinaashiria jambo lisilo sawa. Katika kutokea kwa jambo kama lile tafadhali ona daktari wako haraka iwezekanavyo.

 • Iwapo mtoto wako ataanza kuonyesha dalili za kurudi nyuma katika mazoezi yake hio ni bendera nyekundu.
 • Mtoto wako anapata shida kulala usiku.
 • Kuongezeka kwa mazoezi mengi ya kimwili huweka mtoto kwenye hatari ya kuanguka na ajali zingine. Tembelea hospitali iwapo hilo litatokea
 • Iwapo mtoto wako anakojoa kitandani kwa mara nyingi sana

miaka 6 miezi 7

Ukuaji wa Kiakili

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 7 anaendelea kutofautisha kwa kasi kati ya sawa na mbaya. Yeye anaweza waambia rafiki zake ambao anafikiria hawafanyi sawa.

Katika huu umri, uwezo wa mtoto wako kuzingatia kitu kimoja unaongezeka na ataweza kufanya mambo yenye utata shuleni na pia nyumbani. Pia utaweza kugundua mtoto wako anaweza kufanya haya:

 • Kukuambia umri wake
 • Kuhesabu na kuelewa dhana ya nambari kumi. Kwa mfano, wanaweza kuhesabu vipindi kumi vya chokoleti
 • Wanaweza kujieleza vizuri wakitumia maneno
 • Aanze kuelewa mahusiano ya chanzo na sababu. Mawazo ya sihiri ambayo ni dalili ya wale bado hawajaingia shule huanza kudidimia haraka katika huu umri.
 • Anaweza kusoma na kuandika vizuri
 • Anaweza kuelewa dhana ya wakati
 • Anaweza kukuambia wakati
Vidokezo

Lazima umfunze mtoto wako kuwa ni sawa kufanya makosa. Mwache mtoto wako akuone ukijaribu mambo mapya na ukifeli. Hili litamwezesha kuelewa kuwa kusoma na kukua yote huhusisha kufanya makosa,  lakini cha muhimu ni kutokata  tamaa. Hivi vidokezo zaidi zitakusaidia wewe mzazi wa mtoto wa miaka sita miezi saba.

 • Onyesha mtoto wako mapenzi. Tambua jitihada zake
 • Msaidie mtoto wako kukuza hekima ya kuwajibika – muulize mtoto wako akusaidie katika kufanya mambo nyumbani kama vile kuandaa meza.
 • Zungumza na mtoto wako kuhusu shule, marafiki na mambo anayoyatarajia katika maisha ya usoni.
 • Zungumza na mtoto wako kuhusu kuwaheshimu wengine. Mhimize kuwasaidia watu wanaohitaji msaada
 • Msaidie mtoto wako kuwa na malengo anayoweza kutimiza. Hili litamwezesha kujivuna anapozitimiza na kutegemea kwa umbali idhini na tuzo kutoka kwa watu
Wakati wa kumwona daktari

Lazima umwone daktari wa watoto iwapo mtoto wako ataonyesha dalili hizi:

 • Ugumu katika kusoma ama dalili zingine za ulemavu
 • Kitu kinachomsumbua mtoto wako kama vile kunyanyaswa
 • Jambo linalogusia afya ya kiakili ama mkazo wa mawazo
 • Anakataa kukaa mbali na wewe
 • Anafurahia kucheza akiwa peke yake
 • Anakaa kukwepa mambo mengi
Ukuaji wa Muingiliano/jamii na Hisia

 

miaka 6 miezi 7

Katika miaka 6 miezi 7, mtoto wako ataendelea kujenga urafiki na kuelewa mahusiano. Si jambo lisilo la kawaida kuwa na vita katika mahusiano haya. Watoto wanajaribu kutambua hizi hisia kama vile wivu. Pumzika ukijua hivi vita vitapotea haraka tu jinsi vilivyoanza.

Jinsi mtoto wako anamudu haya mahusiano, ataweza kupata nguvu na usalama kutoka kwa wale ana uhusiano wa karibu sana. Kukubalika katika vikundi linakuwa jambo la muhimu kuliko hapo awali, na mtoto wako anajifunza kukaa na watu na kushirikiana.

Jinsi mtoto wako wa miaka sita miezi saba anavyozidi kuwa huru, yeye kwa mara nyingi atataka kujihusisha kwenye michezo yenye hatari.

Maarifa ya mtoto wako ya kuongea inavyozidi kukua, utagundua kuwa ataweza kuwa shwari katika kueleza kilichotokea, anachohisi na anachofikiria.  Mtoto wako ataweza kuongeza juu ya maarifa au tabia yake - kama vile, ‘naweza kula hamburger kumi kwa mara moja!’

Tarajia udanganyifu, maongo na wizi katika huu umri, mtoto wako anapojaribu kufikiria ni wapi anatoshea na nini kinachokubalika.

Vidokezo

Katika umri huu ni jambo la busara kuwa makini kwa haya ili kuwa mzazi mzuri kwa mtoto wako wa miaka sita miezi saba:

 • Mwache mtoto wako afanye uchaguzi juu ya michezo na vichezeo vyake. Mpe mifano mingi ili aweza kufanya uchaguzi mwafaka
 • Kuwa na wakati kwenye michezo ya video, matumizi ya kompyuta na televisheni. Hakikisha kuwa wakati wake kwenye televisheni hauzuii yeye kucheza nje, kulala vizuri ama kuwa na familia
 • Msomea mdogo wako vitabu na ata wewe aweza kukusomea pia
 • Weka vipimo vya mzazi kwenye runinga na kompyuta
 • Usiwe na aibu kuzungumza na mtoto wako kuhusu mada ngumu kama vile msongo – rika, vita, matumizi ya dawa na mapenzi. Tafuta njia kulingana na miaka za kujibu maswali bila kuongeza utata ama woga.
 • Fikiria juu ya mafunzo ya kuogelea na kufunza juu ya usalama wa moto
 • Mfunze mtoto wako kuwa ni sawa kufanya makosa. Mwache mtoto wako akuone ukifanya mambo mapya na ukifanya makosa. Hili linamsaidia mtoto wako kujua kuwa kusoma na kukua yote huhusisha kufanya makosa lakini na muhimu ni kutokata tamaa.
 • Mhimize mtoto wako kujua athari ya matendo yake na kuweza kuzingatia maoni na fikira za watu wengine. Unaweza kufanya hivi kwa kuuliza maswali kama vile, ‘unafikiria Jane anahisi nini unapofanya hivyo?’
 • Tumia nidhamu kumwongoza mtoto wako na kumkinga badala ya adhabu kumfanya kuhisi vibaya juu ya kitendo chake. Fuatia kila mazungumzo juu ya kile si cha kufanya na kile ambacho anafaa kufanya
Wakati wa kumwona daktari

Hakikisha umemtembelea daktari wako iwapo:

 • Ana kigugumizi anapozungumza
 • Ana kipindi kigumu kuzingatia maelekezo
 • Huwa na kipindi kigumu kufanya marafiki
 • Hutumia nguvu kupita kiasi na watoto wengine
Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

 

miaka 6 miezi 7

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 7 anaweza kuongea katika sentensi kamili! Hili lazima linakufurahisha sana. Yeye anajifunza maneno kumi mapya kila siku na anazidi kuongeza msamiati wake. Si jambo la kushangaza mtoto wako wa miaka sita miezi saba anazungumza sana. Yeye kwa mara nyingi ana ucheshi mwingi na anakuza hisia zake za kufurahisha.

Mtoto wako anaweza kuelewa lengo na manufaa ya kunena. Sentensi zake ni rahisi na mara nyingi huwa na maneno saba ama zaidi. Katika huu umri, mitindo mingi ya sauti imeumbika ata kama mtoto wako anaweza kuwa na shida kutamka “r’s” ama anaweza kusema maneno kama vile ‘pisgetti’ badala ya spaghetti. Katika huu umri mtoto wako anafaa:

 • Kuwa na uwezo wa kufuata maelekezo matatu kwenye mfululizo
 • Ameanza kuona kuwa maneno mengine yana maana zaidi ya moja
 • Anza kuzungumza kwa ucheshi
 • Onyesha dalili ya kukua sana kwa uwezo wa kiakili
 • Kuanza kusoma vitabu vilivyo sawa kwa umri wake
 • Kusema ama kutambua maneno asiyoyajua
 • Uwezo wa kutofautisha kati ya mchana na usiku na kushoto na kulia
 • Uwezo wa kujua wakati
 • Uwezo wa kurudia nambari tano kwenda nyuma
Vidokezo

Kadri iwezekanavyo, endelea kumsomea mtoto wako hadithi. Ndio njia bora zaidi ya kujenga msamiati wake na kuongeza katika benki yake ya maneno. Kwa mara nyingine mhimize mtoto wako akusomee pia. Mhimize aandike chini maneno yaliyomfurahisha na pia unaweza kuratibisha wakati wa kunakiri chini maneno na mtoto wako.

Utagundua kuwa mtoto wako wa miaka sita miezi saba huzungumza sana na mazungumzo yake mengi yana husisha maswali. Kuwa mtulivu na ujaribu kuyajibu maswali yote.

Katika huu umri, ana uwezo wa kuzungumza  kama mtu mzima. Usiwe na hofu kuzungumza naye. Cheza naye michezo tofauti na umwache mtoto wako azungumze anachokiona. Mfunze jinsi ya kutamka maneno badala ya kumsahihi  mtoto wako anapofanya makosa katika kuzungumza.

Wakati wa kumwona daktari

Zungumza na daktari iwapo mtoto wako:

 • Ana wakati mgumu kufuata maagizo yenye pande mbili kama vile, “weka mkoba wako mbali na kisha uniletee sare yako ya kucheza mpira
 • Haonyeshi mvuto katika kuandika jina lake
 • Anakataa kusoma
 • Anaonyesha ugumu katika kufanya mambo mengi
 • Hawezi kutofautisha kushoto kutoka kulia
 • Hawezi kutamka ata maneno rahisi kabisa
Afya na Lishe

 

miaka 6 miezi 7

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 7 anahitaji kalori 1800 kila siku. Huu pia ndio wakati mwafaka wa kumfunza mtoto wako lishe bora. Hili ni la muhimu sio tu kwa kukua na kuendelea kwake mbali pia kwa uwezo wake wa kusoma

Kwa sababu mtoto wako anajihusisha sana kwa mazoezi ya kimwili katika huu umri, anafaa kuwa anakula chakula chenye lishe bora ili kuafikia nguvu anayotumia. Pia jaribu kuhimiza mazoezi kwenye mtoto wako. Ikiwa ni michezo shuleni ama kama familia mazoezi ni muhimu na  pia usingizi.

Vyakula kama vilivyotengenezwa kutokana na maziwa, protini, nafaka, matunda, na mboga vyote ni muhimu kwa kukua na kuendelea kwa mtoto wako. Ebu tazama hii orodha ya vyakula vyenye lishe bora zitakavyosaidia mtoto wako kuongeza mizani na kunawirisha mwili wake unaokua.

Kwa kawaida, kiwango cha kalori kwa watoto wa kike na wale wa kiume ni kama ifuatavyo:

 • Wavulana: 1,805 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,693 Kcal/kwa siku

Chakula chao kinafaa kuwa na hivi:

Vyakula vinavyotokana na maziwa

Vyakula vinavyotokana na maziwa ya bururu na maziwa huwa na lishe bora kwa mdogo wako wa miaka sita miezi saba. Mtoto wako atahitaji vikombe vitatu vya maziwa ama maziwa ya mgando katika chakula chake cha kila siku.

Kwa kawaida mtoto huhitaji vikombe 2.5 vya maziwa ama maziwa ya mgando  katika chakula chake cha kila siku. Hakikisha tu kuchagua vilivyo na vipimo vidogo vya mafuta.

Iwapo mtoto wako hapendi bidhaa za maziwa unaweza kutafuta mbinu ya kuongeza hivi katika vinywaji vyake, nafaka, mboga ama chakula kingine kitamu

Kundi la Protini

Kwa watoto katika umri wa miaka 6, CDC inapendekeza gram 36 za protini kila siku. Iwapo mtoto wako husumbua wakati wa chakula sio shida. Ni kama kila watoto hufurahia mayai, maziwa ya mgando, matunda na kuku.

Kundi la Matunda na Mboga

Matunda na mboga hukupa fursa ya kuwa mbunifu. Watoto kwa kawaida huhitaji vikombe vitatu vya matunda  na vikombe viwili vya mboga kila siku. Kwa hivyo wazo lako bora litakuwa kumpa kama vyakula vitamu na kuchanganya na vyakula vingine kwa wingi iwezekanavyo.

Nafaka

Ongeza kiwango cha vikombe vinne katika chakula cha mtoto wako. Kiwango kimoja cha nafaka ni kama Kipande kimoja  cha mkate, kikombe kimoja cha nafaka ama nusu ya kikombe cha mchele uliyopikwa ama nafaka iliopikwa.

Chagua nafaka  kama vile mkate wa kahawia, oti, bisi, quinoa ama pilau. Punguza  nafaka iliyopitishwa  viwandani kama vile mkate mweupe, pasta na mchele.

Kwa kifupi, anachohitaji mtoto wako kila siku (angalia hapa juu ili kujua viwango anavyohitaji vinafanana aje):

 • Matunda: vikombe vitatu kwa vijana wa kiume na vikombe vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana na vikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka : vipimo vinne kwa vijana na vinne kwa wasichana
 • Protini: gramu 36 kwa vijana na 36 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 kwa vijana na 17-20 kwa wasichana
 • Maji: mililita 1500 kwa vijana na 1500 kwa wasichana (vikombe sita)

Vidokezo:

 • Weka matunda yako yakiwa safi, imekatwa na mahali inaonekana kwenye fringe
 • Mpakulie mtoto wako salads mara nyingi, ikiwezekana kwa vyakula viwili kila siku
 • Jaribu mlo ulio na mboga ama ongeza kiwango cha mboga kwenye lishe lililo na nyama
 • Mara kwa mara badilisha protini za nyama na zile za shambani
Wakati wa Kumwona daktari

Mwone daktari wako mara unapotambua hizi ishara katika mtoto wako:

 • Ana uzani wa chini ama zaidi
 • Ana upele usiyo wa kawaida ama uvimbe ama kuchibuka
 • Joto la zaidi ya digrii 39
 • Hutapika mara anapokula chakula.
Chanjo na madawa ya kawaida

Nyingi ya chanjo za mtoto wako zimekamilika katika huu umri. Lakini iwapo hili sio sawa kwako tunaweza kupendekeza kuzungumza na daktari wako juu ya zile zimebakia kwa mara kwa mara.

Vile mtoto wako anavyozidi kukaa shuleni kwa vipindi virefu, anaweza ama kosa kuambukizwa baridi na homa. Kwa hivyo kuwa mwangalifu kwa upele ama joto, kujikuna ama kuumwa na mwili. Himiza mtoto wako kuzungumza iwapo anahisi maumuvi na umpeleke hospitalini kama huelewi chanzo cha maumivu.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Ili kuweza kudhibiti mambo matatu ya kitabibu kwa watoto – joto, kikohozi na mafua jaribu yafuatayo:

 • Joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto hadi digrii 38(100.4F), mpe mtoto wako maji mengi na uhimize apumzike. Pia unaweza kutumia maji ya vuguvugu na kumtila usoni , chini ya mikono na kwenye nyonga ili kusaidia kususha joto chini. Iwapo vipimo vya joto vitazidi digrii 38(100.4F) ni vizuri kumplekea kwa daktari na kufuata ushauri utakaopewa kudhiti afya ya mtoto wako.
 • Kukohoa: Ingawa kukohoa ni jambo ambalo husafisha koo linaweza kuwa la kusumbua kama litajumuika na makasi na chafya. Ni vyema kwanza kujaribu njia mbadala za nyumbani kama vile tangawizi na asali zilizochanganywa kwenye maji ya vuguvugu. Pia muulize mtoto wako kunywa glasi nane za maji kwa siku kumsiadia kurejesha utulivu. Kama kukohoa kutazidi ata baada ya siku tatu ama tano mpeleke kuona daktari kwa matibabu na ushauri.
 • Homa: Iwapo haisumbui sana jiepushe na kunywa dawa za OTC kupigana na baridi ya kawaida. Baridi husababishwa na virusi na kwa hivyo dawa hazitasidia. Kama homa ya mtoto wako ina kuumwa na mwili na joto kiwango cha juu inaweza kuwa influenza. Utahitajika kumpeleka mtoto wako kwa daktari ili kupata ushauri unaofaa.

Ni vyema kugusia hapa kuwa ata kama ni kwaida kununua dawa zingine bila maagizo, wazo lako la kwanza linafaa kuwa njia mbadala zinazoweza patikana nyumbani.

Kwa mfano, mtoto aliye na mafua na anakohoa anafaa kunywa maji iliyo na joto. Yeye anaweza kutumia maji ya chumvi iliyo vuguvugu kutibu maumivu ya koo. Vivyo hivyo maji ya chumvi itasaidai kufungua mapua yake iwapo yamefungika.

Pia ni jambo la muhimu kumfunza mtoto wako kuzingatia usafi wa mwili, haswa kuoga mikono ili kuzuia kuenea kwa magonjwa.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Ana kipimo cha juu cha joto zaidi ya 39 degrees
 • Amekwaruzwa ama ana upele
 • Anateta sana juu ya maumivu kwenye kichwa na maumivu mahali kwingine
 • Amekuwa akitapika na kuendesha kwa zaidi ya siku mbili

Mwezi uliopita: 6 years 6 months
Mwezi ujao: 6 years 8 months

Vyanzo: Web MD, CDC

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio