Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 9

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 9

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 9 anaanza kuichunguza dunia na ubongo ulio na hamu ya maarifa! Jua zaidi kuhusu hatua muhimu za mtoto wako katika hatua hii.

Katika umri huu wa miaka 6 miezi 9, mtoto wako huenda akawa ni mwanga wa shule ya msingi, kwa kuifanya alama yake ya kimasomo. Ni hatua kubwa katika ukuaji wa mtoto wako. Ako huru kuliko hapo awali na huenda akaonekana kama mtoto mkubwa tayari. Ila, mtoto wako anahitaji usaidizi wako katika kuujenga ujasiri na utu wake sasa kuliko hapo awali.

Tuangazie kwa kina mafanikio ambayo bado hayajafunguliwa katika hatua hii kwenye maisha ya mtoto wako.

Ila, kumbuka kuwa kila mtoto ni tofauti. Sio watoto wanaokua uwezo fulani wakati sawa. Hatua hizi muhimu ni mwongozo tu, ila si maagizo dhabiti ya ukuaji.

Ukuaji na Hatua Muhimu, Mtoto Wako Wa Miaka 6 miezi 9: Je, mtoto wako anakua ipasavyo?

6 years 9 months

Image courtesy: Stock

Ukuaji wa Kifizikia

Katika wakati, huu mtoto wako ana uwezo wa kufanya mambo mengi – mengine huenda yakawa hatari kwa afya yake! Kwa hivyo fanya hatua ya kumkumbusha awe mwangalifu anapo enda mahali pa uma na uwe mwangalifu hata unapokuwa kwa starehe zako nyumbani mwako.

Katika mwezi wa tisa wa mwaka wa sita wa maisha ya mtoto wako, anapaswa kuwa na urefu na uzito wa**.

 • Wavulana
  • Urefu: 120.5 cm (47.4 in)
  • Uzito: 22.6 kg (49.7 lb)
 • Wasichana
  • Urefu: 120.1 cm (47.3 in)
  • Uzito: 22.2 kg (49 lb)

Kadri mtoto wako anavyo zidi kukua, uhitaji wake wa kuwa huru unazidi. Epuka haja ya kumfanyia mtoto wako wa miaka sita kila kitu! Unapo mruhusu mtoto wako kujifanyia mambo kipekee, utamruhusu kwa kuitikia mwito wa kushindana. Atapata uwezo wa kuvalia vyema, kujifunga kamba za viatu zake bila usaidizi na kuendesha baiskeli bila kuendesha migurudumu.

Na mwendo hasa ulio imarika kama vile kupanda, kukimbia na kurukaruka, huenda ukaanza kumhusisha mtoto wako katika darasa za kusakata densi ama kucheza kadanda. Yeye pia huenda akaanza darasa za kuogelea katika wakati huu. Siku njema zijazo!

Vidokezo
 • Mhimize mtoto wako kujaribu vitu vipya na kujaribu shughuli zinazo mfurahisha.
 • Katika umri huu, watoto wengi hudhihirisha hamu ya kuonyeshwa kwa vitendo. Nunua vifaa vingi na uhakikishe kuwa una hifadhi vilivyo bora zaidi kumpongeza mtoto wako anapo fanya jambo nzuri!
 • Kadri mtoto wako anavyo zidi kupata hamu zaidi ya michezo, ajali nyingi za kawaida huenda zikafanyika, kama vile kuanguka akiendesha baiskeli ama kugwarwa miguu. Hakikisha unajua matibabu ya kwanza.
 • Iwapo mtoto wako anajifunza kuendesha baiskeli isiyo kuwa na migurudumu, nunua nguo za usalama kuepuka ajali mbaya. Kofia ni lazima!
Wakati wa kumwona daktari
 • Wakati ambapo mtoto wako anatatizika kushika penseli ama kushindwa kushika kifaa cha sanaa.
 • Iwapo mtoto wako wa miaka karibia saba ana wakati mgumu kucheza na wanarika wake.
 • Iwapo ana wakati mgumu kutangamanisha mikono na macho kama vile kushika mpira.
Ukuaji wa Kiakili

Your little one has officially entered the primary school years at 6 years 9 months old

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 9 kwa rasmi amejiunga na miaka ya shule ya msingi. Atakuwa na mengi ya kusoma katika umri huu na shule itakuwa sehemu kubwa ya maisha yake. Ni muhimu kwa mtoto wako kufanya mabadiliko haya makubwa hadi shule hadi shule kubwa. Mtoto wako anapofikiria kuhusu shule kwa njia chanya, kusoma kutakuwa jambo la kufurahikia na rahisi.

Habari njema ni kuwa unaweza tarajia mtoto aliye na umakini zaidi katika umri huu. Mtoto wako kwa sasa anapaswa kuchukua angalau dakika 15 anapofanya jambo ulilo mwagiza ama hata kazi yake ya ziada.

Uwezo wa mtoto wako wa kiakili unaendelea kukua kadri siku zinavyo zidi kupita, kwa hivyo, mtarajie aelewe mambo zaidi kuhusu dunia, hata ucheshi na vicheko. Huenda ukaona mcheshi mdogo akikua!

Uwezo wa mtoto wako wa kusoma, kusema wakati na kuelewa nambari umeimarika sana kwa sasa.

Vidokezo
 • Anapokaribia umri wa miaka 7, mtoto wako bado anakuza kuelewa kwa umbali. Wakati wote, mshike mkono anapopita mitaani kuepuka ajali.
 • Kumfunza usalama wa moto ni muhimu sana katika umri huu kwani mtoto wako ana uwezo wa kuelewa maagizo. Weka kengele za moshi nyumbani mwako na umfunze mtoto wako anacho hitajika kufanya wakati ambapo hatari ya moto inapotokea.
Wakati wa kumwona daktari
 • Iwapo mtoto wako anashindwa kufuata maagizo mepesi.
 • Iwapo mtoto wako anapoteza uwezo ambao alikuwa nao hapo awali.
Ukuaji wa Hisia na Kijamii/ Muingiliano

The apple of your eye is exploring the world in his or her own little way

Kipenda roho chako kinazidi kujua zaidi kuhusu dunia kwa njia yake ya kipekee. Kumtegemeza kwako ni muhimu katika hatua hii kwa sababu mtoto wako anajenge ujasiri wake na pia kukuza njia za kujiegemeza wakati mgumu unapofika.

Katika hatua hii, mtoto wako aanza kuwa huru na kuto tegemea wanajamii, kwa hivyo usipatwe na butwaa unapo ona anaanza kujitolea kufanya kazi nyepesi nyumbani. Hatimaye, mpatie mtoto wako majukumu, na usikasirike mtoto wako mdogo mwenye bidii anapo vunja kikombe ama sahani. Ajali hutendeka.

Mtoto wako anaanza kujua ishara za kijamii ambazo zinapelekea kupata kibali kutoka kwa wazazi na wanarika wake. Mtoto wako ataanza kuwa makini zaidi kwa urafiki na kufanya mambo kwa vikundi.

Vidokezo
 • Kuza ujasiri na kujiamini kwa mtoto wako kwa kujua mafanikio yake, kumsifu na kumwosha mapenzi kila mara.
 • Mkubalishe mtoto wako kujua kuwa uko tayari wakati wote kusikiza matatizo yake. Jaribu kumwuliza mtoto wako kuhusu shule, marafiki na pia mambo yanayo mtatiza.
 • Watoto katika umri huu huenda wakawa na uongo mwingi, kudanganya ama kuiba. Tabia hizi ni kawaida. Unapomshika mtoto wako akidanganya, tumia kama fursa ya kumfunza tabia nzuri. Mkumbushe umuhimu wa kuchukua fursa yake na athari za vitendo hivi.
 • Mhimize mtoto wako kujiunga na vikundi na kujihusisha katika kazi za kijamii. Muunge mkono kukabiliana na changamotokukuza uwezo wake wa kukabiliana na matatizo na kufanya uamuzi.
 • Mfunze mtoto wako kufanya uamuzi wa mambo mepesi. Mwache afanye uamuzi wa vidoli anavyotaka kucheza navyo ama michezo ya kucheza.
Wakati wa kumwona daktari
 • Iwapo mtoto wako anaepuka muingiliano wa kijamii.
 • Unapo ona ishara za nishati ya chini, kukwazwa ama kuwa na wasiwasi.
Ukuaji wa Lugha n Mazungumzo

 

Your child will even be able to make purchases at the store

Mtoto wako anawaambiwa watu wote mambo muhimu aliyo yagundua, jambo la kupendeza zaidi!

Katika umri wa miaka 6, mtoto wako anapaswa kuwa na uwezo wa kueleweka na wageni, asilimia 90-100 ya wakati, kuwa na uwezo wa kufanya ucheshi, na pia kuahidi. Mtoto wako atakuwa na uwezo wa kununua vitu dukani- na uangalivu wa mtu mzima bila shaka. Mtoto wa miaka 6 husahau kuchukua pesa zilizo baki wakati mwingi!

Matamshi ya mtoto wako yameongezeka – huenda yakawa na maneno 2,600-2,700. Ataanza kutumia maneno ya kulinganisha kama ndogo, ndogo zaidi.

Maarifa ya lugha imekuwa kwa kiwango cha juu. Mtoto wako anatumia alama za kilugha kama ngeli na mengineyo.

Vidokezo
 • Hakuna kitu kama kusoma zaidi! Jaribu kumsomea mtoto wako vitabu vinavyo faa umri wake kukuza matamshi yake zaidi.
 • Kusoma pia kuna imarisha ubunifu wake. Kunasaidia watoto kujua mambo anayo yapenda zaidi. Kutasaidia kukuza na kujenga msingi wa kufikia malengo yake maishani.
 • Hata kama huenda kuka kuchokesha kusikiza hadithi za mtoto wako ni muhimu sana. Mazungumzo hukuza kuwa huru, kufunguka na kuongea na hakuna uhusiano bora zaidi kuliko ule ulio na imani.
 • Fuatilia mwendo na maneno ya mtoto wako. Sehemu kubwa ya ukuaji wa mtoto wako ni kusoma kutoka kwako.
Wakati wa Kumwona daktari
 • Iwapo mtoto wako ana matatizo kujibu kwa kutumia sentensi zilizo kamilika.
 • Iwapo mtoto wako amejitenga na haongei maneno mengi.
 • Haelewi nambari ama wakati.
Afya na Lishe

His or her baby teeth may now begin to fall out and get replaced by permanent teeth

Hakuna kumkataza mtoto wako kukua. Meno yake ya utotoni huenda ikaanza kung’oka na akapata meno ya watu wazima. Hakikisha kuwa una mwanzishia mtoto wako kwa hadithi za meno!

Wakati mwema unakuja kwa sababu ya watu wote wake wapya anao patana nao shuleni. Kwa sababu anaanza anaanza kuunda mwili wake na utu wake anapokuwa miaka 6 miezi 9. Ni muhimu kudhibiti mazungumzo wazi. Hii ni njia bora zaidi kwa kuhakikisha afya yake ya kiakili imekua.

Unaweza tarajia kuwa mtoto wako anakua kwa kasi katika hatua hii ya ukuaji. Atakua anaongeza kilo 2 ama 3 kila mwaka na kukua inchi 2.5 kila siku.

Kwa ujumla, mtoto wako anahitaji vyakula aina tatu kupata lishe bora zaidi — maziwa, protini na matunda na mboga.

Kwa hayo yote, kalori zinazo hitajika kwa siku ni:

 • Wavulana: 1,819 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,707 Kcal/kwa siku

Lishe ya kila siku ya vyakula vya mtoto wako inapaswa kuwa na:

Protini

Kadri mtoto wako anavyozidi kukua, anahitaji virutubisho vinavyofaa kujenga misuli na kudumisha nguvu zake. Protini zinasaidia kujenga na ukarabati wa tishu. Kuna maana kuwa mtoto wako anapata nguvu za kupona mbio! Kwa hivyo hakikisha kuwa unajaza sahani yake na mayai, maharagwe na ama na nyama!

Mboga

Matunda ni vyanzo vya vitamini na madini ya kiasili. Pia, ni muhimu kujua kuwa rangi tofauti huwa na umuhimu tofauti. kwa hivyo hakikisha kuwa unatumia mbadala ya mboga za kijani, majano na nyekundu ili kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata vyote anavyo taka!

Mboga

Kama matunda, mboga hukuwa zimejazwa na enzymes ambazo zina fanya mwili kuwa na nguvu na afya zaidi. Na kusaidia kuepuka kupata magonjwa sugu na kupata uzito mwingi zaidi. Hakikisha kuwa mtoto wako anapata faida za mbadala ya rangi zako pia.

Nafaka

Karibia miaka 7, watoto wako wanataka kujua zaidi kuhusu dunia inayo wazingira. Ili kufanya jambo hili litendeke, unapaswa kuwapatia nishati na chanzo kimoja cha nafaka. Kimejazwa na wanga kuhakikisha mwili wako unafanya kazi zake. Hakikisha kuwa unapata nafaka zifaazo badala ya vyakula vilivyo tengenezwa vyenye virutubisho vya viwango vya chini.

Maziwa

Katika umri huu, mtoto wako anaanza kupata meno yake ya ukubwani. Kalisi inapaswa kuwa mojawapo ya madini bora zaidi. Kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata vya kutosha , unahitaji, viwango vya afya vya maziwa, cheese na maziwa ya bururu. Huenda hata ukatengeneza dessert iliyo na viwango vya juu vya kalisi. Ila, kuwa makini, huenda vyakula hivi vikawa na viwango vya juu vya sukari.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mtoto wako wa miaka 6 miezi 9 ya kila siku ni:

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 36 kwa wavulana; gramu 36 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)
Vidokezo
 • Mhusishe mtoto wako katika michezo kuhakikisha kuwa anapata angalau lisaa limoja la michezo ya kifizikia.
 • Zingatia maadili mema ya kukula unapokuwa nyumbani na uzingatie kukula lishe bora. Ni vyema kwa mtoto wako na kwako pia.
 • Mtoto wako anahitaji angalau masaa 9 hadi 12 ya usingizi, kwa hivyo hakikisha kuwa anaenda kulala wakati unaofaa.
 • Hata kama tunaishi kwa enzi za simu mahiri, televisheni na vifaa vingine vya kisasa, wakati mwingi wa kutazama runinga huwa na athari hasi kwa ukuaji wa mtoto wako. Kifanye chumba cha mtoto wako kutokuwa na vifaa vyovyote vya mawasiliano.
 • Weka mwili wa mtoto wako na afya kwa kuwa na ziara za mara kwa mara kumuona mtaalum wa afya ya meno.
Wakati wa kumwona daktari
 • Iwapo mtoto wako hapati usingizi tosha ama analala zaidi ya masaa 9 ama 12 kwa siku.
 • Iwapo ukuaji wa mtoto wako umedidimia.

Chanjo na Maradhi ya kawaida

Katika wakati huu wa miaka 6 miezi 9, mtoto wako anapaswa kuwa amepata chanjo zote. Ili kuwa upande salama, wasiliana na daktari wako iwapo ana habari zozote kuhusu chanjo. Angalia kwa makini, unaweza angalia fungo hili.

Weka akilini kuwa that iwapo rekodi za mtoto wako za chanjo huenda zikawa zimekamilika, huenda bado akaugua magonjwa ya kawaida. Habari njema ni kuwa kuna njia za kutibu maradhi haya nyumbani.

Kutibu Magonjwa ya Kawaida

Katika hatua hii ya maisha ya mtoto wako, ni kawaida kupata homa na kukohoa mara kwa mara ama hata kuumwa na koo. Ila, kama ilivyo desturi, unapaswa kuwa makini na fungo lako la nishati kabla ya jambo lolote la dharura kutokea. Iwapo joto yake inapanda zaidi ya 38ºC, hakikisha kuwa unampeleka kuona daktari bila kusita. Kwa magonjwa ya kawaida, hapa ni baadhi ya matibabu ya kinyumbani ya kufuata:

 • Joto jingi: Hata ongezeko chache la joto huenda likasababisha kupoteza kwa nishati na kuvunja moyo. Kwa hivyo, hakikisha kuwa mtoto wako mdogo anapata mapumziko tosha. Unaweza paka maji ya vuguvugu kwenye sehemu zake nyeti, makwapa ama kwenye utosi wake. Huku kutasaidia kupunguza joto mwilini mwake.
 • Kukohoa: Wakati mwingine, kukohoa kidogo huenda kukawa ni kusafisha koo. Wakati mwingine, huenda kukawa ni jambo la kuwa na wasiwasi. Wakati ambapo kikohozi hiki kina zidi, hakikisha kuwa mtoto wako anakunywa vinywaji vingi. Matibabu ya kinyumbani kama vile kuchanganya tangawizi na asali na maji ya vuguvugu. Kuwa mwangalifu kutoa kikohozi cha rangi ya majano huenda kukawa ni maambukizo.
 • Homa: Kwa homa za kawaida, hakikisha kuwa mtoto wako ana maji tosha mwilini na anapumzika ipasavyo. Mfanyie mtoto wako vipimo kudhibiti iwapo homa hii inatangamana na kuumwa na mwili na joto jingi kwani huenda kukawa ni ishara ya influenza. Kadri iwezekanavyo, epuka kununua madawa bila kushauriwa na daktari.

Katika umri huu, ni muhimu uhakikishe kuwa mtoto wako anazingatia usafi. Kunawa mikono huenda kuka kusaidia kuepukana na kulipa gharama ya juu ya hospitalini na kupata matibabu. Kumbuka kuwa kuepuka ni vyema kuliko matibabu!

Mwezi uliopita: 6 years 8 months

Mwezi ujao: 6 years 10 months

Vyanzo: WebMD, CDC

(*Tahadhari: Hiki ni kipimo cha kimo cha urefu na uzito kulingana na Shirika La Afya Duniani)

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio