Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Na Miezi 2

Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Na Miezi 2

In this article, we look at common 6 years 2 months old child developmental milestones. Check if your child is on track with this information.

Kipenzi mtoto wako kwa sasa yu 6 years 2 months old child ni mwanafunzi anayependa kujifanyia mambo, ambaye kwa wakati mwingi, anapenda kupatana na watu wengi na kufanya marafiki wapya.

Mtoto wako kwa sasa anaelekea kuwa binafasi wa kiakili na kihisia. Kwa hivyo, huenda ukagundua kuwa mtoto wako huenda akakosa kuomba usaidizi wako anapo fanya mambo yake.

Iwapo unashangaa nini kingine unacho tarajia kutoka kwa 6 years 2 months child, tunakupatia orodha kamili ya ukuaji na hatua muhimu za kutarajia.

Tunapo kuelezea zaidi kuhusu ukuaji huu muhimu, tafadhali kumbuka na utie akilini kuwa kila mtoto ni tofauti na kila mmoja hukua kwa mwendo wake. Iwapo una shaka ama maswali zidi, una shauriwa kumtembelea mtaalum wa afya ya watoto.

6 Years 2 Months Old Ukuaji na Hatua Muhimu: Je, Mtoto Wako Anakua Ipasavyo?

child development and milestones

Ukuaji wa Kifizikia- 6 Years 2 Months Old

Katika hatua hii, urefu na uzito wa mtoto wako* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 116.73 cm (46 inchi)
  – Uzito: 21.17 kg (46.7 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 116.2 cm (45.7 inchi)
  – uzito: 20.7 kg (45.7 lb)

6 years 2 months old child kwa sasa anaimarisha uwezo wake wa kifizikia kama vile kuruka, kurusha mateke na kushika.

Kwa hivyo, mhimize mtoto wako kuenda nje kupata wakati wa kucheza ili kuongeza uwezo wake.

Mtoto wako huenda pia akafanya vyema katika michezo ya makundi kama vile kadanda, mpira wa vikapu na uwezo wake wa kuelewa na kufuata maagizo mepesi kwa urahisi.

Kujihusisha kwa michezo kama hii kutamfunza mambo muhimu kama vile kutangamana na watu, uongozi, na nidhamu -  yote ambayo ni muhimu kwa miaka yake ya shule - ila pia ni msingi maalum wa maendeleo ya usoni.

Kando na hayo, idadi kuu ya shughuli za kifizikia ni muhimu kwa ukuaji kiakili wa mtoto wako, kwani una imarisha kumbukumbu zake na kuimarisha uwezo wake wa mwendo.

Unapaswa kuweza kuona ukuaji ufuatao kwenye mtoto wako.

 • Ana kuwa stadi wa shughuli za kifizikia kama vile, kuruka, kutupa, kurusha mateke na kushika.
 • Kusoma jinsi ya kuogelea.
 • Anaonyesha kusawasisha bora zaidi na kutangamanisha.
 • Kusimama kwa mguu mmoja kwa zaidi ya sekunde 9.
 • Kurusha na kushika mpira mdogo vyema.
 • Anajua na kufuata mpigo wa muziki.

Vidokezo:

 • Mhimize apate wakati mwingi nje ya nyumba na darasa za michezo.
 • Hakikisha kuwa mtoto wako anapata lisaa limoja ama zaidi ya shughuli za kifizikia kila siku.
 • Hakikisha kuwa mtoto wako ana nyoosha ipasavyo kabla ya mazoezi ya kifizikia.
 • Mfunze mtoto wako kuhusu lishe na umhusishe katika kununua vyakula vya jikoni.
 • Punguza wakati wa mtoto wako wa kutazama runinga hadi lisaa limoja ama mawili kwa siku.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mtoto wako,

 • Anashindwa kutangamanisha mikono na macho na uwezo wake wa mwendo wa umri wake hauja afikiana.
 • Anashindwa kufanya mambo ya kikawaida kama vile kuvalia viatu ama kufunga viatu.
 • Anapoteza uwezo ambao alikua nao hapo awali.

child development and milestones

Ukuaji wa Kiakili - 6 Years 2 Months Old Child

6 years 2 months child ana akili inayo kua kwa kasi kwani anaendelea kupata uwezo wa kiakili na kujua mambo mengi kila siku.

Uwezo wao wa kusoma pia hukua kutokana na kuona na kuyashuhudia. Huku kuna maana kuwa mtoto katika umri huu atasoma vyema kupitia kwa uzoefu wake wa kucheza ama kutazama wanao wachunga.

Mtoto wako ana taka kujua zaidi kuhusu mazingira yake, na huenda atakuwa na maswali kuhusu mambo yote ayaonayo, kuyasikia ama kuya zoea.

Kwa hivyo mzazi, tarajia kupata maswali mengi kutoka kwa mtoto wako mchanga, na kuweka akilini kuwa kuuliza maswali ni njia ya mwanao ya kusoma kuhusu dunia.

Kando na hayo, mtoto wako ataonyesha hamu zaidi katika kusuluhisha matatizo peke yake, hasa anapokuwa kwenye mazingara yaliyo na mfumo (ambayo ni shuleni) bila ya kuwepo kwako.

Hapa ni baadhi ya ukuaji zaidi unaotarajia kuona kutoka kwa mtoto wako katika upande huu. Mtoto wako:

 • Anasoma kuuliza maswali kuhusu mambo tofauti.
 • Anaonyesha umakini ulio ongezeka.
 • Kuonyesha kutaka kujua zaidi kuhusu mazingira yake.
 • Uwezo wa kufanya kazi ngumu kidogo shuleni na nyumbani.
 • Kupendezwa na kutatizika kwa michezo na puzzles.

Vidokezo:

 • Jibu maswali ya mwanao kwa utulivu na upole.
 • Fanya hesabu kwenye shughuli zenu za kila siku.
 • Tengeneza mahali palipo tulia pa kufanya kazi ya ziada ya mwanao.
 • Usimlazimishe mtoto wako kusoma ama kufanya marudio kusipo faa.
 • Himiza kucheza kulio bunika.
 • Mpeleke mtoto wako mahali kunako himiza masomo kama vile mbuga.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Ana epuka kufanya shughuli nyepesi kama vile kujivalisha nguo.
 • Hajui jina lake anapo itwa.
 • Ana tatizika kuongea na wengine.
 • Hawezi kuhesabu hadi 10.
 • Kushindwa kusoma majina ya maneno mawili.

kids and their cognitive development at 6 years 2 months old

Ukuaji wa Hisia na Muingiliano - 6 Years 2 Months child

6 years 2 months old child anakuwa mwenye umaarifa zaidi wa kupata na kutunza urafiki mpya anapo endelea kujua zaidi kuhusu kuingiliana na marafiki wake.

Mtoto wako atasoma mambo muhimu kama vile kugawa na kuwa na shukrani, kwa hivyo, usiwe na shaka unapo ona kuwa mtoto wako ako tayari kugawa vidoli vyake na marafiki ama jamii yake.

Kando na hayo, mtoto wako pia anakuwa stadi wa kueleza hisia na fikira zake.

Hapa ni baadhi ya ukuaji unaokusudia kuona katika pande hii kwa 6 year 2 month child. Ana:

 • Kwa ufasaha anasema anacho hisi ama kufikiria.
 • Hamu ya kupata marafiki wapya.
 • Anaelewa umuhimu wa kufanya kazi kama kikundi.
 • Ana umakini kwa urafiki.
 • Ana woga kidogo anapo patana na watu wapya.

Vidokezo

 • Uliza maswali kila siku kuhusu anavyo hisi.
 • Mtie mwanao moyo kueleza hisia zake.
 • Mfunze mtoto wako kuhusu kunyanyaswa.
 • Mfunze kuhusu shukrani na heshima.
 • Sisitiza na umsifu anapo fanya mema.
 • Mfunze mwanao kuhusu "hatari ya watu wageni" na "kuguswa kwema, na kubaya."
 • Kua mfano mwema inapofika kwa tabia njema na nidhamu.

 Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Anakataa kutenganishwa nawe.
 • Anachukia kucheza ama kuongea na watoto wa rika lake.
 • Hataki kugawa vitu vyake na marafiki wake.
 • Ana aibu nyingi kupindukia ama ukatili mwingi kwa wengine.

Children and their language development

Ukuaji wa Lugha na Mazungumzo - 6 Years 2 Months Child

6 years 2 months old child ni chiriku kwa sasa na anaongea kwa ujasiri kwa kutumia sentensi kamili, mufti yenye maneno hadi 7.

Ana paswa kuwa na uwezo wa kusema neno la heru 3 ama 4 kama vile "mnyama" ama "spaghetti" na kutamka majina kama "mwenyewe" na "yangu" bila tatizo lolote.

Mbali na hayo, mtoto wako huenda akadhihirisha hamu kuu ya kuandika ama kusoma.

Tuangazie ukuaji zaidi katika upande huu: 6 years 2 months child

 • Amekuza uwezo wake wa kuongea, na kumsaidia kujieleza hasa anacho taka, mawazo na hisia zake kwa njia kuu.
 • Amejua herufi vyema hasa consonants.
 • Uwezo wa kutumia ngeli ya sasa na iliyopita kwa sentensi zake.
 • Kutambua mfumo kwenye maneno.
 • Anauliza maana ya jina ama sentensi.

Vidokezo: 

 • Ongea kwa upole unapo muongelesha mtoto wako
 • Tumia muziki kama njia ya kuimarisha uwezo wake wa kuongea
 • Uliza mtoto wako akwambie kuhusu siku yako. Hii ni njia mwafaka ya kumtia nguvu kukuza uwezo wake wa kujieleza na pia uweze kujua iwapo mtoto wako anakumbana na matatizo yoyote shuleni
 • Mwanzishie mtoto wako majina mapya kadri uwezavyo, na kumbuka kumwelezea unacho maanisha
 • Mwulize mwanao maswali mengi ili kuimarisha uwezo wake wa kupiga ngumzo

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Anaepuka kusoma vitabu kabisa.
 • Ana tatizika kufuata maagizo mepesi.
 • Kigugumizi zaidi.
 • Kusema "huh?" ama "nini" hata baada ya kujirudia mara nyingi.
 • Ana tatizika kukumbuka vitu vidogo kuhusu mazungumzo.

what they are eating at this age

Afya na Lishe - 6 Years 2 Months child

6 years 2 months old child kwa sasa amekua orodha kamili ya vitu avipendavyo na asivyo vipenda hasa kwa mambo ya lishe.

Huku kuna maana kuwa kama mzazi, huenda ikawa vigumu kumfanya mtoto akubali chakula asicho kipenda.

Walakini, haijalishi chakula wanacho kipenda, watoto wa umri huu bado wanahitaji lishe bora na yenye afya ili kukimu mahitaji ya nishati wanayo hitaji, ukuaji na maendeleo.

Watoto wa umri huu wanapaswa kuvila vyakula vifuatavyo kila siku:

Kwa ujumla, kalori za wavulana na wasichana katika umri huu ni ifuatavyo:

 • Wavulana: 1,766 Kcal/kila siku
 • Wasichana: 1,657 Kcal/kila siku

Familia ya maziwa

Hakikisha kuwa mtoto wako anakunywa hadi vikombe viwili ama vitatu vya maziwa kila siku. Ila usipitishe viwango kwani huenda kukapelekea viwango vya chini vya vitamin d. Kiwango kizuri cha vyakula hivi vina hakikisha mtoto wako ana kua na afueni na mwenye nguvu.

Familia ya protini

Kulingana na Taasisi ya Dawa huko Umerikani, protini ni mojawapo ya vitu vinavyo itunga seli na kwa hivyo ni muhimu kwenye lishe ya watoto wako. Wazazi wanapaswa kuhakikisha wanawalisha watoto wao angalau protini mara mbili kwa siku. Kwa hivyo hakikisha kuwa unaijaza nyumba yako na mayai, tuna, lentils na ndengu na pia nyama.

Familia ya matunda na mboga

Wazazi wanapaswa kuhakikisha kuwa 6 years 2 months child anapata viwango sawa vya matunda na mboga. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa wazazi hawa wapatii watoto wao mboga nyingi kama matunda.

Vyakula hivi viwili ni muhimu kwa kukabiliana na magonjwa na matatizo ya kiafya kama vile kukosa maji tosha mwilini. Hakikisha kuwa mtoto wako anapata vikombe viwili vya matunda na mboga kila siku. Jaribu mboga tamu, na uziweke kwenye chakula chako ukipendacho zaidi ama pizza iliyo tengenezewa nyumbani.

Nafaka

Hakikisha una tia ndani ounsi 4 za nafaka kwenye lishe ya mtoto wako ya kila siku. Fanya jaribio na kiasi kidogo cha oatmeal ama pasta zilizo pikwa.

Kwa ujumla, unapaswa kuchagua nafaka mzima kama vile oatmeal, oatmeal, quinoa, whole-wheat bread, popcorn, ama wali wa hudhurungi. Ila, hakikisha kuwa unapunguza kiwango cha wali ama mkate unao mlisha mtoto wako.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mwanao ya kila siku (tazama hapo juu kuona viwango vinavyo hitajika):

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 36 kwa wavulana; gramu 36 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Vidokezo:

 • Mpatie vyakula vingi kutoka kwa familia tofauti
 • Unda mfumo dhabiti wa kumlisha
 • Iwapo mtoto wako amepata chakula cha kutosha, usimlazimishe kukula zaidi
 • Epuka kumnunulia vinywaji vyenye sukari nyingi ama vyakula vyenye ufuta mwingi
 • Kula lishe bora na mtoto wako atafuata

Chanjo na Maradhi ya kawaida

Watoto wengi wa 6 years 2 months huwa wamepata chanjo zile nyingi katika umri huu. Ila, ni jambo la busara kuwasiliana na daktari wako.

Kadri mtoto wako anavyo kuwa shuleni kwa wakati mwingi, huenda akaugua ama akakosa maradhi ya kawaida kama homa na mafua. Pia, kuwa makini kuona upele unao ibuka kwenye mwili wa mwanao. Na cha muhimu zaidi, mtie moyo akwambie iwapo anahisi kujikuna mwili ama anahisi hayuko sawa.

Kama kumbusho, mtoto wako wa 6 years 2 months child anapaswa kuwa amepata chanjo zifutazo katika umri huu:

 • DTaP, chanjo ya kulinda dhidi ya diphtheria, tetanus, na pertussis
 • IPV, chanjo inayo linda dhidi ya polio
 • MMR, chanjo inayo linda dhidi ya measles, mumps, na rubella
 • Varicella, chanjo inayo linda dhidi ya chickenpox
 • Flu shot inayo hudumiwa kila mwaka

Wasiliana na daktari kujua iwapo rekodi za chanjo za mtoto wako zina afikiana na tarehe.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Walakini, baadhi ya wakati hata na rekodi kamili ya chanjo, mtoto wako huenda bado akapata homa, mafua ama magonjwa mengine kama vile Hand Foot and Mouth. Iwapo mtoto wako anaonyesha ishara za kutokuwa na starehe, ama hata kutapika na kuendesha ama joto jingi (zaidi ya 38°C/100.4°F) wasiliana na daktari.

  • Kutibu joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto ya hadi 38.5°C , ni salama kumpatia mtoto wako paracetamol baada ya kila masaa 4 hadi 6 ama ibuprofen. Ila, suluhu lako la kwanza linapaswa kuwa matibabu ya kinyumbani kama vile kupaka maji ya vugu vugu kwenye uso wake, makwapa ama sehemu nyeti ili kuishusha joto yake. Iwapo hii haipunguzi joto yake, mpeleke aone daktari.
  • Kutibu kikohozi: Iwapo kukohoa ni njia ya mwili kuosha koo, huenda ikasumbua iwapo inaandamana na homa na kupiga chafya. Kwa kawaida, tumia matibabu ya kinyumbani kama vile tangawizi na asali kisha uchanganye na maji ya vuguvugu. Kukunywa maji kwa wiki angalau glasi nane za maji kwa siku. Nunua madawa kama vile decongestants, antihistamines, cough suppressants (antitussives), mucolytics and expectorants. Hizi ni salama kwa mtoto, ila tuna kushauri, uwasiliane na mtaalum wa afya ya watoto kabla ya kuzinunua.
  • Kutibu homa: Isipokuwa ikikuliwaza zaidi, epuka kuchukua madawa za kununua kutibu homa. Homa husababishwa na viini na madawa hayatasaidia. Iwapo mtoto wako pia anahisi kuumwa na mwili na joto jingi, huenda akawa na influenza. Unapaswa kumpeleka hospitalini atibiwe.

Kwa magonjwa mengine ya kawaida kama vile colic, madaktari hawawezi kushauri ununue dawa bila ya kushauriwa na mtaalum. Ila badala yake, wange kushauri utumie matibabu ya naturopathic ama homeopathic. Kwa chickenpox, iwapo mtoto wako ameugua maradhi haya, usimpe aspirin, huenda ikamletea matatizo ya Reye's syndrome. Huenda ikahatarisha ama kuharibu figo na ubongo. Badala yake, hakikisha kuwa mtoto wako amepata dosi ya chanjo ya chickenpox.

Kwa kuendesha kusiko kuwa kwingi, epuka kumpatia mwanao dawa kama vile Pepto-Bismol na Kaopectate zinazo kuwa na bismuth, magnesium, ama aluminium. Ni hatari kwa watoto wadogo. Badala yake, hakikisha kuwa umempatia mtoto wako maji na oral rehydration (ORS) kuhakikisha kuwa hakosi maji mwilini.

Ni muhimu kufahamu kuwa iwapo joto ya mtoto inapanda zaidi ya 38 degress ama dalili zinaonekana kuwa zinaendelea kuwa mbaya zaidi, mpeleke kwa daktari wako bila kusita.

Wakati wa kumwona daktari:

Wasiliana na daktari wako ama mtaalum wa afya ya watoto iwapo mtoto wako:

 • Ana uzito mwingi ama mdogo zaidi
 • Ana upele, uvimbe, vidonda na kufura kusio kwa kawaida
 • Ana uzito wa chini ama juu zaidi
 • Ana harisha ama kutapika sana na joto jingi (zaidi ya 39 degree celsius), unapaswa kumtembelea daktari wako kwa kasi

Mwezi uliopita: 6 years 1 month old 

Mwezi ujao: 6 years 3 months old 

Vyanzo: Mayo ClinicCDC, Web MD  

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio