Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: Mtoto wako wa miaka mitano

Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: Mtoto wako wa miaka mitano

Find out what your feisty five-year-old is going to amaze you with this month!

Mwangalie mtoto wako mchanga! Amekuwa mkubwa sana, La! Mtoto huyu wako wa miaka mitano ana uwezo wa kujitegemea zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita. Kwa sasa amekuwa chiriku na kipepeo wa kuingiliana na anakushangaza kwa ukuaji wake wa kifizikia na kiakili.

Tuna angazia hatua muhimu za ukuaji unazo paswa kutarajia kwa mtoto wako wa miaka mitano.

*Tafadhali kumbuka kuwa hatua hizi muhimu za ukuaji si lazima kwa kila mtoto kwani kila mtoto anakua katika mwendo wake. Iwapo unashaka kuhusu kipengele chochote cha ukuaji wake, pata ushauri wa daktari bila kupoteza wasaa.*

mtoto wako wa miaka mitano

Ukuaji na Hatua Muhimu za Mtoto wa Miaka Mitano: Je, mtoto wako anakua ipasavyo?

Ukuaji wa kifizikia

Sio mtoto tena anaye chafua kila mahali na kuangusha kila kitu. Mtoto wako wa miaka mitano anaonyesha ukuaji wa kasi, hasa anapo kimbia uwanjana ama ndani ya nyumba! Kwa sasa, uwezo wake wa kuona u-shwari 20/20. Ataongeza karibu kilo mbili mwaka huu na kuongezeka kwa urefu kwa sentimita sita.

Sio uwezo wa kijumla wa mwenendo wa mwanao unao kuwa, ila pia mwenendo wake haswa wa mwenendo. Tuna angazia kwa karibu ukuaji wa kifizikia wa mtoto wako wa miaka tano na ishara dhibiti mwezi huu.

 • Anaweza kuandamanisha vyema- mikono yake na mwili wake wote
 • Anaruka ruka na kuudhibiti mwili wake vyema
 • Anaendesha baiskeli
 • Anaudbiti mguu mmoja huku amefunga macho
 • Huenda akaanza kukua meno ya watu wazima
 • Anaweza kutumia vyombo vya kula kwa urahisi zaidi
 • Ana ishika penseli vyema na anaweza chora muundo wa pembetatu
 • Anaweza kitumia kisu kupaka siagi kwa mkate
Katika hatua hii, urefu na uzito wa mwanao* unapaswa kuwa ifuatavyo:
 • Wavulana
  - Urefu: 109.2 cm (43 inchi)
  - Uzito: 18.4 kg (40.5lb)
 • Wasichana
  - Urefu: 107.9 cm (42.5 inchi)
  - Uzito: 17.9 kg (39.5lb)

Vidokezo: 

 • Mlete mtoto wako kwenye uwanja ama kwenye pwani na umkubalishe akimbie na acheze. Hii ni shughuli bora zaidi ya kifizikia ya kuimarisha ukuaji mwema na afya.
 • Mhimize mtoto wako ajivalishe nguo peke yake. Kazi kama kukaza vifungo na kuvuta nyororo husaidia uwezo wake wa mwenendo.
 • Mfunze mtoto wako njia bora ya kusugua meno yake. Mhimize ajaribu kwa kipekee chini ya uangalifu wako.
 • Punguza masaa ya kutazama televisheni hadi lisaa limoja na uhimize shughuli za kifizikia zaidi.
 • Mhimize mtoto wako kutumia vifaa vipya vilivyoko uwanjani. Jambo hili linaisaidia kumpa vikundi vya misuli na kufanya zoezi. Na pia, inasaidia kumpa ujasiri mwingi.
 • Imarisha uwezo wake wa kifizikia kwa mtoto wako kwa kutumia michezo ya kufurahisha. Kwa mfano, mwulize mtoto wako auinue mguu mmoja kwa sekunde 20 iwapo ana uwezo wa kuuinua kwa sekundu kumi tu.
 • Iwapo hujamwanzisisha mtoto wako darasa za kuogelea, hakikisha unamwandikisha. Kuogelea ni mchezo unao mfunza kipawa muhimu cha kujitegemea na kinafanya zoezi mwili wote.
 • Hakikisha kuwa mtoto wako anapata usingizi tosha. Ni muhimu katika ukuaji wake wa kifizikia. Anahitaji masaa nane hadi 10 ya usingizi usiku.

Wakati wa kumwona daktari: 

Iwapo mtoto wako:

 • Hawezi uinua mguu mmoja kwa sekunde zaidi ya kumi
 • Ana matatizo ya kuona ama kusikia
 • Anategwa na kuanguka anapo kimbia
 • Hawezi shika penseli ama chombo kinginecho
 • Hana hamu ya kukimbia ama kujihusisha na michezo ya kifizikia

mtoto wako wa miaka mitano

Ukuaji wa kiakili

Mtoto wako wa miaka mitano ana maswali mengi kuhusu karibu kila kitu. Hamu hii ya kusoma na kujua ni ishara ya ukuaji wa kiakili wa mtoto wako wa kustaajabisha.

Mtoto wako pia atataka kujua jinsi mambo yanafanya kazi. Ataanza kuvitawanya vitu kulingana na muundo, saizi ama rangi, inayoonyesha jinsi akili yake inavyo chakata mambo tofauti kulingana na ishara zake.

Hapa ni baadhi ya ukuaji wa kiakili utakao shuhudia katika mtoto wako wa miaka mitano:

 • Anaelewa ujumla wa wakati
 • Anaweza kuwa makini kwa shughuli ya kufurahisha kwa dakika zisizo punguka 10.
 • Anatambua na kutaja angalau rangi nne
 • Ana uwezo wa kuhesabu hadi 10 ama zaidi
 • Anazijua herufi nyingi
 • Anataja wanyama kama vile paka, mbwa na samaki
 • Huenda akaweza kuliandika jina lake na baadhi ya herufi na nambari

Vidokezo: 

 • Epuka kumsukuma mwanao kusoma ama kuandika iwapo bado hayuko tayari. Mtoto wako mdogo ataifikisha hatua hii muhimu katika mwendo wake.
 • Usitarajie mwandiko ulio msafi na unao someka kwa sasa. Msifu mwanao kwa juhudi za kusoma na kuandika.
 • Endelea kumsomea na kusoma na mtoto wako mchanga. Hakikisha kuwa vipindi hivi vina mhusisha na umwulize maswali. Pia, mhimize mwanao kuvi ashiria rangi na michoro tofauti kwenye kitabu.
 • Mpeleke mwanao kwenye mbuga na uga na mahali kwingineko kwa kufurahisha kadri iwezekanavyo. Hakikisha kuwa safari hizi zinafurahisha na kuhusisha. Kwa mfano, unapokuwa kwenye mbuga mfunze mwanao kuhusu sehemu mbali mbali za ua ama mti.
 • Mpe mwanao vitu vingi vya kucheza navyo. Ni muhimu katika kuhimiza ukuaji wake wa kiakili.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mwanao:

 • Hawezi kuhesabu hadi 10
 • Hawezi kukwambia jina lake
 • Anashindwa kujua majina ya rangi tofauti
 • Ana shida ya kuwa makini kwa shughuli angalau kwa dakika chache

mtoto wako wa miaka mitano

Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

Mtoto wako wa miaka mitano ni uhai wa sherehe na anapenda kupewa uangalifu zaidi. Uwezo wake wa kuingiliana umeimarika kwa sana. Anafurahikia kuwa miongoni mwa wengine na kucheza na marafiki wake.

Katika umri wa miaka mitano, mtoto wako huenda akawa na rafiki wa ndani na kwa sasa anapenda kucheza na rafiki zake ikilinganishwa na kucheza mwenyewe. Mtoto wako mchanga anahitaji mapenzi, ulinzi, uangalifu na kibali chako. Atafanya mambo mengi ili kupata kibali chako na kukubalika kihisia nawe. Wewe bado ndiye mtu muhimu zaidi maishani mwake!

Wakati ambako kelele imepungua, huenda mtoto wako bado akawa na mhemko wa hisia ukifutanishwa na " sio sawa!" huku akiikanyagisha miguu yake midogo kwenye sakafu. Yote haya ni sawa. Utagundua kuwa tabia hii hupunguka mnamo muda wa miezi ijayo.

Je, nini kingine unacho kitarajia katika hatua hii ya ukuaji wa muingiliano na hisia zake?

 • Huenda mwanao akawa wa kupeana masharti, hasa anapocheza na marafiki wake
 • Ako tayari kuviwaga vidoli vyake na anao wapenda zaidi
 • Huenda akadanganya, kwa jitihada za kukupendeza
 • Mara kwa mara, anapenda kucheza peke yake
 • Anaongea kwa sana na atakuwa na mazungumzo marefu na yeyote anaye sikiza
 • Anapenda kuenda nje, hata kama ni kufika kwenye duka
 • Anapenda michezo ya kudhania  na huenda akajiongelesha

Vidokezo

 • Huu ni wakati wa kutayarisha siku za michezo na marafiki zake wadogo. Mtoto wako atafurahikia kuwa miongoni mwa watoto wengine na kusoma mambo muhimu ya kuingiliana.
 • Sisitiza umuhimu wa tabia nzuri. Ili iwapo amejitahidi kukuhadithia "hadithi," mkumbushe kuwa hapaswi kuingilia mazungumzo ya wa mtu mwingine anapo kuwa akiongea. Mtumia kutumia majina kama "kunradhi, na pole."
 • Iwapo kupeana masharti wakati mwingine huenda ikawa kawaida, ukigundua kuwa inapiku mipaka, mwongeleshe kwa upole kuhusu jinsi jambo hilo si njema. Katika siku za michezo na marafiki wake, himiza michezo ambapo kila mmoja anahusishwa.
 • Mpe uangalifu wake wote anapo kuongelesha na msikize kwa makini. Iwapo unahitaji kushughulikia jambo fulani, usimpe kisogo. Ila, mwambie kuwa utarudi baada ya muda mfupi.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako:

 • Hapendi kucheza na watoto wengine
 • Anapenda kuzingirwa na watoto wazee kumliko
 • Anatumia nguvu ama maneno mabaya anapo cheza
 • Anakasirika mara kwa mara, kitoto
 • Hapendi kuenda nje ya nyumba

Ukuaji wa Lugha na Mazungumzo

Uwezo wa lugha na kuzungumza wa mtoto wako wa miaka mitano umekua kwa sana. Huenda ukahisi kuwa mtoto wako anaongea bila kuacha na atajua kuviongelelea vitu tofauti. Sio jambo ya kustaajabisha kwa sababu watoto katika umri huu watajua maneno yanayo karibia 2,000.

Hapa ni baadhi ya ukuaji unao tarajia katika hatua hii:

 • Ana zungumza vyema na watu wengine
 • Anaongea kuhusu mambo ama kuhadithi kwa urahisi
 • Anaweza soma maneno mawili ama matatu
 • Watu wageni wanaweza kumwelewa kwa wakati mwingi
 • Anatumia utendaji ujao kama: " Tuende kwenye mbuga kesho!"
 • Anatumia maneno kama ("mimi, wewe, yeye, wao" nakadhalika) vyema
 • Anafuata maagizo yake vyema. Kama vile: "Tafadhali mwambie dada yako aje, anawe mikono na ale chakula cha jioni."
 • Anaelewa jinsi hadithi inavyo paswa kuwa (kinachotangulia, kufuata na kumalizia)

Vidokezo: 

 • Mhimize mtoto wako akwambie kuhusu siku yake, na kumbuka kuuliza maswali baadaye.
 • Cheza michezo ya kufurahisha na mwanao.
 • Unapo msomea na kusoma na mwanao, ashiria maneno rahisi unapo soma. Kwa njia hii, mtoto wako atasoma kuhusisha sauti na jinsi neno linavyo tamkwa. Na hatimaye kufanya kujisomea na kuyandika maneno haya rahisi kwake.
 • Unapo maliza kusoma hadithi, mwulize mtoto wako akuhadithie mlicho soma. Inahimiza ukuaji wake wa kuongea na kiakili kwani mtoto wako anahitaji kukumbuka ili akuhadithie hadithi ile.
 • Mfunze mwanao nyimbo mpya.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hawezi kukielewa chochote
 • Haongei sana na watu wengine
 • Haonekani kuyaelewa maswali ama maagizo
 • Anashtuka kwa sana
 • Anaonyesha dalili za kuzumbaa kwa yale anayo yajua

mtoto wa miaka mitano

Afya na Lishe

Ni muhimu sana kwa mtoto wako wa miaka mitano kupata lishe bora kuimairisha afya na ukuaji wake. Mapumziko ni muhimu kwake na usingizi. Wakati ambapo mtoto wako huenda akaacha kulala sana kwa sasa, anahitaji masaa kati ya 9 hadi 10 ya kulala kila usiku.

Iwapo urefu na uzito hutofautiana kwa sana, na pia huadhiriwa na familia, kwa kawaida, katika umri huu, mtoto wako ana uzito wa kilo 18 na urefu unaokaribi sentimita 109.

Lishe ya kalori kwa wavulana na wasichana katika umri hii huwa ifuatavyo:

 • Wavulana: 1,660 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,555 Kcal/kwa siku

Lishe ya kawaida na kalori hizi huenda ikahusisha kipande cha mkate na kuku iliyo tengenezewa nyumbani, wali na kikombe cha maziwa.

Ili kufanya mambo rahisi zaidi, tunaangazia mambo ambayo mtoto wako wa miaka mitano anapaswa kuwa akikula:

Protini

Katika miaka mitano, mtoto wako anahitaji vijiko viwili vya protini (kwa ujumla karibia gramu 32.4) kila siku. Jaribu kumpa samaki wa kuchemshwa (kiasi cha kiganja cha mtoto), bakuli ndogo la maharagwe ama yai la kuchemsha.

Matunda

Pia anahitaji vikombe vitatu (gramu 100) vya matunda kila siku. Kikombe kimoja cha matunda ni sawa na yaliyo toka shambani, yaliyo gandishwa ma kukaushwa. Nusu (1/2) tofaha moja kubwa, 1/8 ya ndizi, na zabibu. Unaweza mpa matunda yaliyo changanywa na nafaka ama yoghurt.

Iwapo mtoto wako anataka kunywa maji ya sharubati, hakikisha kuwa ni asilimia 100 ya maji matamu bila sukari za kuongezwa. Pia, jaribu kumlisha matunda kutoka shambani iwezekanavyo, hasa na ngozi yake ya nje.

Mboga

Katika hatua hii, mtoto wako anahitaji vikombe visivyo pungua viwili vya (gramu 100 kila moja) vya mboga kila siku. Jaribu kumpa fiber na mboga zilizo na iron nyingi kama vile spinachi, karoti zinginezo.

Pia, unaweza kumpa kikombe kimoja cha mboga kinacho toshana na kikombe kimoja cha mboga zilizo pikwa, mboga za majani, nyanya moja kubwa na karoti mbili.

Mpe mwanao mboga tofauti za rangi nyingi kutoka kijani, nyekundu, rangi ya machungwa, maharagwe kila wiki. Unapo chagua mboga zilizo hifadhiwa, chagua zilizo na kiwango cha chini cha sodium.

Nafaka

Mwanzishie mwanao ounsi nne za nafaka katika lishe zake. Ounsi moja ya nafaka ni sawa na kipande kimoja cha mkate,kikombe kimoja cha nafaka zilizo tayari ama nusu kikombe cha wali uliopikwa.

Unaweza chagua kutoka kwa nafaka nzima kama vile, mkate usio wa mtama mweupe, mchele wa hudhurungi. Ila, usisahau kupunguza kiwango cha nafaka zilizo tayarishwa kama vil mkate mweupe ama mchele.

Maziwa

Katika umri huu, mtoto wako anapaswa kunywa maziwa angalau ounsi 17 hadi 20 za maziwa kila siku.

Huenda ukampa maziwa yaliyo hifadhiwa ama yogurt badala ya maziwa, na ounsi mbili za cheese iliyo tengenezwa.

Kwa ufupi, haya ni baadhi ya mahitaji ya mtoto wako ya kila siku (tazama viwango tulivyo angazia hapo juu)

 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 32.4 kwa wavulana; gramu 32.4 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Chanjo na maradhi ya kawaida

Mtoto wako hana chanjo yoyote inayo karibia kwa wakati huu. Soma makala haya kuhakikisha kuwa ratiba ya mtoto wako wa miaka mitano imefuatiliwa. Shauriwa na mtaalum wa watoto hukusu kumpa mtoto wako dawa ya mafua.

Maradhi ya kawaida ya watoto katika umri huu ni kama vile ugonjwa wa Hand, Foot and Mouth, na kikohozi na mafua.

Wakati ambapo huwezi epuka maradhi haya, unaweza imarisha uwezo wa mwanao wa kupigana na maradhi kwa kumpa lishe bora na vinywaji vingi, matunda na mboga. Zingatia hali ya juu ya usafi kama vile kunawa mikono ambayo huenda ikasaidia sana katika kumlinda mwanao kutokana na magonjwa.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kati ya magonjwa haya ya kawaida ambayo huenda yakamshika mwanao, ya kawaida kabisa huenda yakawa ni kukohoa, homa na joto jingi. Tuangazie jinsi ya kuyatibu nyumbani.

 • Kutibu homa: Kwa ujumla, unashauri kuepukana na madawa ya kununua bila ya kuidhinishwa na daktari. Homa husababishwa na viini kwa hivyo dawa nyingi hazisaidii kuponyesha. Walakini, iwapo homa hii inazidi na kuwa joto jingi na maumivu na kuumwa, ni vyema upate ushauri wa daktari.
 • Kutibu joto jingi: Mpatie mwanao vinywaji vingi, iwapo na joto inayo zidi 38°C (100.4°F)hakikisha kuwa anapata mapumziko ya kutosha. Pia, huenda ukampangusa na maji vuguvugu kwenye utosi wake, chini ya makwapa na sehemu nyeti kupunguza joto ile. Walakini, iwapo joto yake inaongezeka zaidi ya 38°C (100.4°F),unapaswa kumpeleka kwa daktari akupe mawaidha jinsi ya kudhibiti afya ya mtoto wako.
 • Kutibu kikohozi:Kukohoa ni kawaida kwa watoto. Huenda kukawa kwa kusinya na kufuatiwa na homa kali. Ni bora kuwa ujaribu kutibu maradhi haya kinyumbani kwa kutumia kitunguu saumu, asali, maji ya vuguvugu na ginger. Pia unaweza mwuliza mtoto wako anywe maji glasi nane za maji kutuliza kutokuwa na starehe. Iwapo kikohozi hakipungui kwa siku tatu ama tano, pata ushauri wa daktari.

Ni muhimu kujua kuwa baadhi ya matibabu haya huweza kununuliwa bila ya ushauri wa daktari. Ni vyema kuwa matibabu ya kwanza ya mwano iwe ni ya kinyumbani.

Mpe mtoto wako vinywaji vingi vyenye joto kutuliza kikohozi chake ama mafua. Msaidie kukiweka kiwango kidogo cha maji yenye chumvi kwenye mdomo kisha kutema bila ya kumeza kuiponya kuhisi vibaya kwenye shingo.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mtoto wako:

 • Ana uzito mdogo na haongezei urefu wake
 • Anapata joto jingi (39 degrees Cel na zaidi)
 • Ana upele usio wa kawaida na vidonda kwenye mwili wake

Mwezi uliopita: 4 years 11 months

Mwezi ujao: 5 years 1 month

Reference: Web MD

(*Disclaimer: This is the median height and weight according to WHO standards)

Republished with permission from The Asian Parent

Written by

Risper Nyakio