Lishe ya mboga imekuwa maarufu na watu wengi kuizingatia kwa kipindi cha miaka michache iliyopita. Huku lishe hii ikiwa na manufaa mengi ya kiafya, kuna imani nyingi zinazoendelezwa zisizo za ukweli. Katika makala haya, tunaangazia ukweli kuhusu lishe ya mboga na imani zisizo za kweli.
Ukweli kuhusu lishe ya mboga
1.Ukila lishe ya mboga unapoteza uzito

Kuna imani kuwa kula lishe ya mboga na mimea ni dhamana ya kupoteza uzito wa mwili wakati wote. Kumbuka kuwa ili lishe ikusaidie kupoteza uzito, unapaswa kuzingatia ulaji wa lishe yenye afya. Kuna baadhi ya lishe za mboga ambazo sio za afya. Huenda zikawa na ufuta mwingi. Ili kupoteza uzito zaidi wa mwili, ni muhimu kufanya mazoezi na kuzingatia ulaji wa lishe yenye afya.
2. Wanaozingatia lishe ya mimea hawapati protini tosha
Sio kweli. Kuna vyakula vingi mbadala ambavyo vina wingi wa protini. Kama vile wild rice, lentils, seitan, quinoa, spirulina na aina zingine za maharagwe. Mboga kama viazi vitamu, viazi, broccoli, mchicha na asparagus huwa na kiasi cha protini.
3. Maziwa na bidhaa zake ni muhimu kuwa na mifupa yenye nguvu
Bidhaa za maziwa sio muhimu katika kuwa na mifupa yenye nguvu. Maziwa na bidhaa zake hazihitajiki kuipa mifupa nguvu. Mbali kalisi ndiyo inayohitajika. Vyakula kama maharagwe, mchicha, mbegu za chia, seaweed na peas huwa na kalisi.
4. Lishe za mimea zina hatarisha afya

Kulingana na utafiti, nyama nyekundu inahusishwa na afya duni. Watu wanaokula nyama nyekundu kwa wingi mara nyingi hutatizika kutokana na matatizo ya kiafya kama kisukari, uzito mwingi wa mwili, ugonjwa wa moyo na saratani ya colon. Hivi basi, lishe isiyo na nyama ina afya zaidi, na kulinda mwili kutokana na magonjwa.
Kula lishe yenye nyama nyeupe ama laini kuna manufaa mengi kwa mwili. Baadhi ya nyama nyeupe ni kama vile kuku, nyama ya sungura na samaki. Kula lishe ya mboga pekee huenda kukasababisha upungufu wa baadhi ya madini mwilini.
5. Unahitaji nyama kupata misuli ya mwili
Kuna imani kuwa usipokuwa protini zinazotokana na wanyama, hutaweza kujenga misuli ya mwili. Misuli hutokana na ulaji wa protini. Kuna mimea na mboga zinazokuwa na protini, kwa hivyo unaweza kupata misuli bila kula nyama.
Soma Pia: Umuhimu Wa Lishe Bora Katika Kusafisha Mirija Ya Uzazi