Ulezi Wa Usiku Kwa Watoto: Mbadala Wa Kuwafunza Kulala Wakati Wa Usiku

Ulezi Wa Usiku Kwa Watoto: Mbadala Wa Kuwafunza Kulala Wakati Wa Usiku

Ulezi wa usiku ni mbinu mpya inayo wasaidia wazazi kuwafunza jinsi ya kulala usiku bila kusumbua. Soma zaidi kuhusu mbinu hii!

Watoto wachanga wana uraibu wa kuamka kati kati ya usiku - hasa siku za kwanza chache baada ya kuzaliwa. Lakini wanapo pata ratiba yao ya kulala (wakitimiza miezi 4), baadhi ya wazazi huamua kuanza kuwa anzishia utaratibu wa kulala, ama kuwafunza watoto wao jinsi ya kulala peke yao. Walakini, kuwafunza kulala hakufanyi kazi kwa kila mmoja. Wazazi wengine hasa wanao shauri ulezi wa pamoja, wana tatua tatizo la mtoto kusumbua usiku na 'ulezi wa usiku'.

Ulezi Wa Usiku Ni Nini Hasa?

Wakati ambapo kuwafunza kulala kuna mfunza mtoto jinsi ya kulala usiku akiwa peke yake, na ulezi wa usiku, wazazi wanaendelea kuwaitika watoto wanapo lia na kuwa bembeleza walala kwa kuwa lisha, kuwaimbia na kadhalika. Wakati ambapo huku kuna maanisha kuwa utachukua muda kabla ya kulala na kupata usingizi tosha usiku, ulezi wa usiku una faida nyingi kama ilivyo onyeshwa na The Huffington Post:

  1. Uwezo wa mtoto wako kuhisi ako salama

ulezi wa usiku

Mtoto wako ata hisi ako salama zaidi akijua kuwa wazazi wake watakuja anapo wahitaji. Kuhisi salama huku kutawasaidia kuwa na mawazo chanya kuhusu kulala.

2. Ni asili/ kawaida

Mtoto wako anapo lia, mwili wako huitikia kwa kutoa homoni inayo fahamika kama prolactin. Ambayo hutuma ujumbe wa kibailojia kwako kumchukua na kumnyonyesha mtoto wako.

3. Ni njia nzuri ya kuhimiza utangamano na mtoto wako

Hiki ni kipindi tu katika ukuaji wa mtoto wako - hakita dumu milele kabla ya kuamka usiku kuwe jambo la kale. Ulezi wa mtoto wako usiku unakukubalisha kufurahia utulivu wa mtoto wako na nyakati za kufurahisha.

Kuna mbinu na mitindo tofauti ya ulezi wa usiku, lakini hapa kuna maagizo machache kutoka kwa daktari Sears kukusaidia.

Kuwa na matarajio halisi

Huwezi mlazimisha mtoto wako kulala- jambo ambalo unaweza fanya kama mzazi ni kufanya mazingara ya mtoto wako yahimize kulala iwezekanavyo. Lengo lako linapaswa kuwa, kumsaidia mtoto wako kukuza mtazamo chanya na wenye afya wa kulala.

Fahamu kuhusu ahidi zinazo kuwa nzuri sana kuwa kweli

ulezi wa usiku

Kuna mawazo na ushauri mwingi sana kuhusu kumfanya mtoto wako alale. Wakati ambapo huenda baadhi ya mambo haya yaka saidia kwa watoto wachache, unapaswa kutia akilini kuwa kila mtoto ni wa kipekee. Na kwa hivyo huenda ushauri huo ukakosa kufanya kazi kwa mtoto wako. Kabla ya kujaribu mbinu fulani, jiulize kama ni sawa kwa mtoto wako.

Jipe nafasi ya kubadilika

Ikiwa mbinu unayo tumia kwa sasa haisaidii, usiwe na uwoga wa kufanya mabadiliko kwa utaratibu wako wa kulala hadi upate kitu ambacho kita mfaa mtoto wako na mtindo wako wa maisha.

Tafuta mahali ambapo mtoto ana lala vyema zaidi

Baadhi ya watoto hulala vyema wakiwa vyumbani vyao, kwenye vitanda vyao, wakati ambapo wengine hupendelea kulala pamoja na wazazi wao. Wengine hulala vyema na mchanganyiko kati ya njia hizi mbili. Wazazi wengi huchanganya mbinu hizi mbili katika miaka ya kwanza miwili ya watoto wao ili kugunuda kinacho fuzu kwao.

Je, mawazo yako ni yapi kuhusu kuwafunza watoto kulala?

Soma pia:Ni Salama Kwa Mtoto Kulala Na Mto na Blanketi?

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio