Jinsi Umri Unavyo Athiri Uhusiano Wako Wa Kimapenzi

Jinsi Umri Unavyo Athiri Uhusiano Wako Wa Kimapenzi

Haupaswi kuangalia umri wa mtu unaye penda mbali unapaswa kuangalia mambo mengine muhimu kama mna andamana na kutangamana vyema.

Umri ni nambari tu, na hakuna vizuizi vya umri wa mtu unaye amua kupenda kwani pia mapenzi hayana macho na haya chagui utakaye penda.

Haupaswi kuangalia umri wa mtu unaye penda mbali unapaswa kuangalia mambo mengine muhimu kama mna andamana na kutangamana vyema. Ni kweli kuwa unaweza pata mapenzi na kutoshelezwa kihisia na furaha isiyo na kifani katika watu usio tarajia. Haijalishi umri wao, ama tofauti kati ya umri wenu nao. Tuna angazia mambo unayo tarajia unapo kuwa kwa uhusiano na watu wa umri mbali mbali.

Jinsi umri unavyo athiri uhusianowako wa kimapenzi

umri unavyo athiri uhusiano

Wapenzi wa umri wa miaka ya 20s ya mapema na kumalizia 20s

Aina ya uhusiano huu ni rahisi. Kulingana na wataalum wa mapenzi, mwanamke aliye katika miaka ya mapema ya 20 anapo kutana na mwanamme anaye malizia miaka yake ya 20, huenda mkawa na uhusiano mzuri na usio na matatizo na wakati rahisi na mwema katika mapenzi yenu.

Viwango vya kukomaa kati ya wawili hawa havija tofautiana sana kwani wanawake hukomaa kwa kasi ikilinganishwa na wanaume. Kwa hivyo wawili hawa watakuwa na maono sawa katika mambo mbalimbali.

Miaka ya mapema ya 20s na miaka ya kumalizia 30s

Huenda uhusiano wa aina hii ukaegemea kuongozwa ama kutawaliwa. Mwanamme anaye karibia miaka yake ya 40 na mwanamke aliye katika umri wake wa miaka 20 inahisi sio sawa. Mmoja atahisi kuwa amekomaa zaidi na kuwa huyo mwingine ni mtoto kwake.

Miaka ya kati ya 20s na ya mapema ya 30s

 

umri unavyo athiri uhusiano

Uhusiano kati ya wanamke katika miaka yake ya kati ya 20s na mwanamme aliye katika miaka yake ya mapema ya 30 ni uhusiano bora. Wanawake wanapo fikisha umri huu, huwa wameanza kufikiria watakavyo anzia maisha ya kifamilia na kupata watoto. Sio kuwa wangependa vitu hivyo sasa hivi, lakini viko kwa malengo yao ya siku za usoni. Kwa wanaume, kipindi hiki hutendeka wanapokuwa katika miaka yao ya mapema ya 30s. Kwa hivyo kuna uwezekano uhusiano wa aina hii utafuzu.

Miaka ya kati ya 20s na ya kumalizia ya 30s

Mwanamme anaye malizia 30s zake huenda akataka kufunga ndoa mapema iwezekanavyo kwa sababu wengi kama sio marafiki wake wote wamefanya hivi tayari. Na huenda akawa na tatizo anapo pata mchumba aliye katika miaka ya kati ya 20s.

Katika umri huo, huenda akawa na mawazo ya kufunga ndoa ila, hana haraka za kufanya hivi kwani bado ana wakati. Katika umri huu, wanawake wengi huwa makini na kazi zao na kujifurahisha maishani. Uhusiano kati ya wawili hawa utakuwa na tatizo ambapo mmoja atahisi kuwa anamsukuma mwingine kufunga ndoa wakati ambapo mwingine anahisi kuwa ana hitaji wakati zaidi kabla ya kufanya uamuzi ule.

Miaka ya kumalizia 20s na ya kumalizia 30s

Huenda uhusiano kati ya wachumba wa umri huu ukawa mojawapo ya uhusiano bora zaidi.

Wanawake wanapo malizia miaka yao ya 20s huwa wamejigungua, wanacho taka na wasicho taka, aina ya familia wanayo taka na aina ya mchumba ambao wangependa. Huenda wengi wao wakawa wana kazi nzuri na fedha pia. Na huenda wanaume waka gundua mambo haya wakiwa katika miaka ya kati ya 30s. Kwa hivyo kunapo kuwa na uchumba kati ya wawili hawa, unaweza pata watu wawili walio komaa na wenye ujasiri kuhusu wanacho taka maishani.

Miaka ya kati ya 30s na ya kumalizia ya 30s

Wachumba katika kitengo hiki huenda wakawa na aina fulani ya shaka. Huenda mwanamke akawa na shaka kuhusu ugumba kukaribia na wakawa katika mbio za kupata watoto kabla ya saa yao ya uzazi kuwadia. Na huenda mwanamme pia akawa na shaka sawa ama hata kukosa mbio, huku kutafanya wakose wakati tosha wa kujuana zaidi na kukuza uhusiano wao kabla ya kupata watoto.

Je, una mengi ambayo ungependa kutujulisha kuhusu vile ambavyo umri unavyo athiri uhusianowako ama ulivyo athiri uhusiano wa hapo awali? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi.

Soma Pia: Maswali 5 Katika Uhusiano Unayo Ogopa Kumwuliza Bwana Yako Lakini Unastahili

Written by

Risper Nyakio