Kutumia Siku Ya Kwanza Ya Kipindi Cha Hedhi Kufahamu Umri Wa Mimba

Kutumia Siku Ya Kwanza Ya Kipindi Cha Hedhi Kufahamu Umri Wa Mimba

Kwa kutumia siku ya mwisho ya kipindi cha hedhi na kipimo cha ultrasound, mama anaweza kufahamu umri wa mimba.

Nilipata mimba lini? Huenda likawa swali ngumu kujibukwa sababu kuhesabu siku ulipo tunga mimba hufanywa kutumia siku ya kwanza ya kipindi chako cha hedhi cha mwisho. Pia, unaweza tumia ultra sound kudhibiti umri wa mimba yako.

Jinsi ya kuhesabu umri wa ujauzito wako

Kipindi chako cha hedhi cha mwisho

dalili za mimba huanza kuonekana lini

Ikiwa mwanamke ana kipindi kisicho cha kawaida na anafahamu siku ambapo kipindi chake cha mwisho kilianza, umri wa ujauzito wake unaweza hesabiwa kutoka tarahe hiyo.  Umri wa mimba una hesabiwa kutoka siku ya kwanza ya kipindi cha mwisho cha hedhi cha mama. Na wala sio kutoka siku ambapo alitunga mimba.

Kufanya ultrasound

Hii ndiyo njia dhabiti zaidi ya kupima umri wa mtoto katika siku za mapema za ujauzito. Hufanyika mapema kutoka wiki ya 5 ama 6 baada ya kipindi cha hedhi cha mwisho cha mama. Na kadri ujauzito unavyo zidi kukua, ubora wa mbinu hii kutambua umri wa fetusi hupungua.

Wakati bora wa kufahamu umri wa ujauzito wako ni kati ya wiki ya nane ya mimba hadi ya 18. Njia bora zaidi ni kuhesabu kuanza siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho ya mama kisha kudhihirisha kwa kutumia ultrasound.

Katika visa spesheli ambapo mwanamke alizalishwa kwa kupitia mbinu za kisasa kama IVF (in vitro fertilization) anajua siku hasa alipo tunga mimba.

Kwa kesi zinginezo, ni vigumu mwanamke kujua siku hasa. Hasa kwa wanawake walio na vipindi visivyo vya kawaida vya hedhi. Na wasio kumbuka siku ambapo kipindi chao cha mwisho kilianza. Inakuwa vigumu pia kufahamu umri wa ujauzito wao.

Naweza panga siku yangu ya kujifungua?

umri wa mimba

Ikiwa unaepuka kupata mimba wakati fulani ama kupanga wakati ambapo unataka kujifungua, unaweza jaribu kutunga mimba wakati fulani. Sio kila mwanamke anaye kuwa na bahati na kujifungua wakati anao taka. Lakini hata unapo tunga wakati fulani, hauwezi dhibiti wakati ambapo utajifungua.

Hizi ndizo njia za kipekee za kufahamu umri wa mimba unapokuwa mjamzito. Kutumia wakati ulipo anza kipindi cha hedhi na kipimo cha ultrasound.

Chanzo: WebMD

Soma Pia:Je, Ni Wakati Upi Ulio Bora Kufanya Kipimo Cha Mimba?

Written by

Risper Nyakio