Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Fahamu Faida Za Kula Mayai Kwenye Lishe Yako

2masomo ya dakika
Fahamu Faida Za Kula Mayai Kwenye Lishe YakoFahamu Faida Za Kula Mayai Kwenye Lishe Yako

Mayai yana fahamika sana na pia kuliwa kwa wingi duniani kote. Yana tayarishwa kwa njia tofauti na ni muhimu sana kwa afya yako. Je, unafahamu umuhimu wa kula mayai kwenye lishe yako?

Umuhimu Wa Kula Mayai

1.Mayai yana protini

Yai moja lina gramu 6 za bidhaa iliyo na amino acids ambazo ni kuu katika ujenzi wa protini. Ni muhimu kwa sababu mwili wako hauna uwezo wa kutengeneza peke yake. Sehemu nyeupe ya yai huwa na nusu protini na kiwango kidogo cha ufuta na kolesteroli.

2. Yana virutubisho vingi

Yai lina virutubisho vingi, vitamini, madini na amino acids kwa kila kalori ikilinganishwa na vyakula vingine. Unapo kula yai, unapata:

  • Protini yenye ubora
  • Selenium
  • Antioxidants
  • Phosphorous
  • Choline

3. Mayai yana kolesteroli nzuri

Kolesteroli nzuri inayo fahamika kama HDL huonekana kuongezeka kwa watu wanao kula mayai 3 ama zaidi kwa siku. Kolesteroli mbaya LDL huongezeka pia. Inakuwa vigumu kwa isiyo kuwa nzuri kukuumiza na kufanya iwe rahisi kwa ile nzuri kutoa isiyo faa mwilini.

4. Kupunguza nafasi zako za kupata kiharusi

Hata kama utafiti unatofautiana, inaonekana kuwa kula yai kila siku kunapunguza hatari hiyo. Katika utafiti uliofanyika Uchina, watu walio kula angalau yai moja kwa siku walikuwa na nafasi asilimia 30 kidogo za kufa kutokana na kiharusi ikilinganishwa na wale ambao hawakula mayai.

5. Kusaidia kuhisi umeshiba

Mayai ni mazuri sana kwa watu walio na lengo la kupunguza uzito wa mwili. Lina kalori 70 na ni rahisi kuchakatwa na kutumika mwilini. Kwa hivyo kukufanya uhisi umeshiba upesi unapo kula pamoja na mboga zingine.

6. Kusaidia na afya ya macho

Yana saidia macho yako kwa sababu yana antioxidants lutein na zeaxanthin zinazo kusaidia kuepuka magonjwa ya macho. Baadhi ya magonjwa yaliyo maarufu zaidi ya macho ni cataracts. Mboga za kijani kama vile mchicha na sukuma wiki zina antioxidants hizi lakini mayai ni chanzo bora zaidi. Kwa sababu ufuta ulioko kwenye mayai ni rahisi kutumika mwilini mwako.

7. Kufanya ubongo uwe shupavu

Mayai yana vitamini D ambayo ni nzuri kwa sehemu ya kijivu na vigumu kupata kutoka kwa chakula chochote. Na yana choline inayo saidia na seli za neva. Choline pia ni muhimu sana kwa wanawake wenye mimba na wanao nyonyesha kwa sababu ya jukumu lake katika ukuaji wa ubongo.

Njia za kutayarisha mayai

Balanced nigerian diet beans

Kuna njia nyingi ambazo unaweza tumia kutayarisha mayai yako. Huenda ukachagua:

  • Kuchemsha
  • Kukaanga
  • Kupiga yaliyo pigwa(scrambled)

Soma pia:Je, Ungependa Usaidizi Wa Kupanga Ratiba Ya Lishe Ya Wiki Moja?

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Feeding & Nutrition
  • /
  • Fahamu Faida Za Kula Mayai Kwenye Lishe Yako
Gawa:
  • Mayai Na Magonjwa Ya Moyo: Kula Yai Moja Hakuna Uhusiano Na Magonjwa Ya Moyo Kulingana Na Utafiti

    Mayai Na Magonjwa Ya Moyo: Kula Yai Moja Hakuna Uhusiano Na Magonjwa Ya Moyo Kulingana Na Utafiti

  • Epuka Kula Usiku: Hatari Za Kula Chakula Kingi Usiku

    Epuka Kula Usiku: Hatari Za Kula Chakula Kingi Usiku

  • Umuhimu Wa Kuongeza Mayai Kwa Lishe Ya Watoto

    Umuhimu Wa Kuongeza Mayai Kwa Lishe Ya Watoto

  • Je, Usingizi Ni Muhimu Kwa Afya?

    Je, Usingizi Ni Muhimu Kwa Afya?

  • Mayai Na Magonjwa Ya Moyo: Kula Yai Moja Hakuna Uhusiano Na Magonjwa Ya Moyo Kulingana Na Utafiti

    Mayai Na Magonjwa Ya Moyo: Kula Yai Moja Hakuna Uhusiano Na Magonjwa Ya Moyo Kulingana Na Utafiti

  • Epuka Kula Usiku: Hatari Za Kula Chakula Kingi Usiku

    Epuka Kula Usiku: Hatari Za Kula Chakula Kingi Usiku

  • Umuhimu Wa Kuongeza Mayai Kwa Lishe Ya Watoto

    Umuhimu Wa Kuongeza Mayai Kwa Lishe Ya Watoto

  • Je, Usingizi Ni Muhimu Kwa Afya?

    Je, Usingizi Ni Muhimu Kwa Afya?

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it