Jinsi Ya Kusaidia Mtoto Wako Kukuza Tabia Ya Kunawa Mikono

Jinsi Ya Kusaidia Mtoto Wako Kukuza Tabia Ya Kunawa Mikono

Mikono michafu ni chanzo cha magonjwa yanayo julikana kama mafua. Soma umuhimu wa kunawa mikono na ufahamu jinsi ya kumsaidia mwanao kunawa mikono katika makala haya.

Hivi karibuni, mwalimu alifunza wanafunzi wake umuhimu wa kuosha mikono kutumia maonyesho ya picha. Umuhimu wa kunawa mikono hauwezi tiwa chumvi. Lakini, ni ukweli kwamba ni mojawapo ya matendo ambayo watu hawatilii maanani.

 

a teacher's graphic display on the importance of washing hands

Chanzo cha picha: Facebook

Hii ni kwa sababu hatuoni kamili  madhara ya kutembea na mikono michafu kwa kuwa hatuwezi ona virusi au bakteria katika mikono yetu. Matokeo yake huwa ni kushikwa na ugonjwa, ni vigumu kuunganisha wakati ambapo tuligusa kipatakalishi bila kuosha mikono baadaye. Katika makala haya, tunajifunza umuhimu wa kunawa mikono, na pia kufunza mtoto wako kukuza tabia yake ya kuoga mikono.

Umuhimu wa kunawa mikono kulingana na Sayansi ni upi?

Kulingana na CDC, watoto milioni 1.8 chini ya miaka tano hufa kila mwaka kutokana na kuendesha na pneumonia-magonjwa ambayo yanaua watato katika kiwango cha juu duniani. Ujumbe huu unaonyesha umuhimu mkubwa sana wa kunawa mikono unapoangazia uhusiano wa moja kwa moja kati ya magonjwa haya na kuosha mikono.

Sam Stephens ambaye ni mkubwa wa Msingi wa Safisha Ulimwengu, ambalo ni shirika lisilo na faida hutoa sabuni na mafunzo ya usafi kwa jamii zisizojiweza kote duniani, anakubaliana kwamba “ kunawa mikono kutumia sabuni inaweza punguza kipimo cha vifo kutokana na magonjwa haya kwa kiwango cha asilimia 65. Wakati ambapo watu wanaosha mikono vile ifaavyo na wakati ufaao,njia hii inaweza kuwa fanisi kushinda dawa,chanjo au maji safi zaidi, kama njia ya kuingilia kati dhidi ya pneumonia na kuendesha.”

Zaidi ni kuwa?

benefits of washing hands

Kuosha mikono haizuilii pneumonia na kuendesha. Inasaidia dhidi ya kuenea kwa bakteria ambazo  zinakinzana na viuavija sumu, hivi kupunguza magonjwa kama vile shida ya tumbo, mafua na homa. Chini kuna baadhi ya umuhimu wa kunawa mikono mara kwa mara:

 • Kuzuia kwa kuendesha na magonjwa mengine

Kuosha mikono ni njia ya uhakika ya kuondoa bakteria ambazo wewe na mtoto wako mmeathirika nayo. Hii husaidia kuzuia bakteria ambazo zinaweza kua katika miili yetu na kuwa hatari.

 • Epuka maambukizi ya kawaida ya macho

Kugusa macho na mikono yako ni jambo ambalo mtu hufanya bila hiari ambalo hutokea kila unapohisi kugusa macho yako. Usipo osha mikono yako mara kwa mara, unahatarisha kueneza bakteria hizi ndani ya macho yako, ambayo husababisha maambukizi ya macho.

 • Weka nyumba yako bila bakteria

Weka nyumba ikiwa safi kwa kuua viini katika sakafu na nyuso za nyumba kutumia bidhaa za usafi ambazo zina msingi wa pombe ili kupunguza bakteria. Hii pia inamaanisha kwamba lazima uoshe mikono mara kwa mara ili mikono yako isiwe kiini cha kuenea kwa bakteria nyumbani.

 • Wakati mdogo nje ya shuleni na kazini

Bakteria zinajulikana kusababisha magonjwa kama vile homa, kuendesha na shida ya tumbo. Una uwezekano wa kushikwa na magonjwa haya usipo osha mikono yako mara kwa mara, kumaanisha unaweza kosa kwenda shuleni au kazini.

 • Bili iliyopunguka ya gharama za hospitali

Ni jambo dhahiri kuwa lazima ulipe bili ya hospitali iwapo wewe au mtoto wako atagonjeka. Kwa hivyo kujaribu kuzuia magonjwa haya kwa kuosha mikono mara kwa mara inaweza saidia kupunguza bili yako.

Nitasaidia mtoto wangu vipi kukuza tabia ya kunawa mikono?

umuhimu wa kunawa mikono

Wazazi huchangia pakubwa sana kwa kusaidia watoto wao kufahamu umuhimu wa usafi kwa kuosha mikono. Kuanza mapema pia kunasaidia uendelevu wa tabia hii. Ili akiwa mkubwa ataliona kama jambo la kawaida. Pia unaweza fanya tendo hili liwe la kufurahisha kwa kuimba wimbo wa kuosha mikono. Pia unaweza buni mchezo. Hivi ndivyo utasaidia mtoto wako ili aoshe mikono yake kila wakati.

 • Kumkumbusha kila wakati

Kukuza tabia inahitaji wakati na kazi.Jizoeshe kumkumbusha mtoto wao kuosha mikono kila anapotoka msalani, kabla ya kula, baada ya kushika mnyama nyumbani, baada ya kucheza nje na baada ya kukohoa, kuchemua au kutoa makamasi.

 • Kuwa mfano wa kuigwa

Mtoto wako ataosha mikono akiona pia wewe kama mzazi unaosha mikono yako pia kila wakati. Atafahamu kuwa kuna umuhimu wa kufanya jambo lile.

 • Ongea kuhusu umuhimu wake

Kama njia ya kuelimisha mtoto wako kuhusu umuhimu wa kusafisha mikono yako, mwambie pia kuhusu magonjwa ambayo yanazuiliwa na kuosha mikono.

Ukijaribu kuvutia tabia ya kuosha mikono katika mtoto wako, kuna mambo kadhaa ambayo ya kufuata ili kuhakikisha kwamba bakteria mikononi imeoshwa vizuri. Inua mtoto wako kama haifikii pahali pa kunawia mikono.

Hapa pana hatua nne ili kuhakikisha ume nawa mikono yako vyema:

 • Paka mikono yako maji kisha jipake sabuni ili kutengeza povu za sabuni.
 • Sugua mikono yako pamoja kwa muda utakaouchukua kutamka maneno “siku ya kuzaliwa njema” mara mbili akilini. Safisha mikono yako vizuri ukianza na kofi la mkono,kisha nyuma ya mkono wako, katikati ya vidole kila chini ya kucha.
 • Mwagilia mikono yako maji safi, yanayotiririka kisha isugue kumaliza sabuni yote.
 • Tikisa mikono yako mara kadhaa, kisha ikaushe na tauli safi au katika kifaa cha kukausha mikono.

Mtoto wangu anapaswa kunawa mikono lini?

umuhimu wa kunawa mikono

Mtoto wako anapaswa kuosha mikono yake kabla ya:

 • Kula
 • Kugusa midomo,macho au mapua
 • Kugusa kidonda

Na baadaye:

 • Kwenda msalani
 • Kutoka shuleni
 • Kucheza na wanyama
 • Kutumia vifaa vya kuchezea
 • Kutoa makamasi
 • Kuwa karibu na mtu mgojnwa
 • Kugusa nepi
 • Kugusa uchafu
 • Kucheza nyumbani

Katika hali ambapo hauna maji au sabuni unaweza tumia sabuni ya kuua viini. Walakini, kutumia sabuni na maji ndio njia mwafaka ili kuhifadhi usafi mikononi kwa kuwa sabuni ya kuua viini haitoi uchafu wote.

Soma Pia : Teacher’s Experiment Shows How Dirty Hands Are After Touching Your Laptop

Hapa ni jinsi unavyo paswa kunawa mikono kulingana na WHO:

Chanzo: www.kidshealth.org

Originally written by Lydia Ume

Translated by Risper Nyakio

Written by

Risper Nyakio