Fanya Mazoezi Kuboresha Afya Na Urefu Wa Maisha Yako!

Fanya Mazoezi Kuboresha Afya Na Urefu Wa Maisha Yako!

Ni muhimu kufanya mazoezi haijalishi umri wako. Mazoezi yanasaidia mwili na akili yako. Yana timiza haya vipi? Na ni njia gani bora zaidi ya kuya ongeza kwenye maisha yako? Tuna angalia umuhimu wa mazoezi maishani mwako.

Kwa nini mazoezi ni muhimu

umuhimu wa mazoezi

Yana weza kusaidia kuishi muda mrefu, kuwa na maisha yenye afya kwa sababu yanaweza:

 • Kuweka mifupa, misuli na viungo vya mwili vikiwa na afya
 • Kupunguza nafasi zako za kupata kisukari, saratani ya colon ama maradhi ya mifupa kukosa nguvu
 • Kupunguza shinikizo la damu
 • Kukusaidia kudhibiti kukwazwa kimawazo na kuboresha mhemko wako
 • Kupunguza ishara za kuwa na wasi wasi ama fikira nyingi
 • Kupunguza nafasi zako za kupata maradhi ya moyo

Unapaswa kufanya mazoezi kiwango gani?

Unapo zidi kuzeeka, huenda ukaanza kuwa na uwoga wa kufanya mazoezi. Huenda ukadhani kuwa yanaweza kuumiza ama lazima ujiunge na madarasa ya kufanya zoezi. Ama ukakosa uhakika wa mazoezi ya kufanya.

Suala kuu si unako fanyia mazoezi ama jinsi unavyo yafanya, anza tu.

Watu wazima wenye afya wanapaswa kulenga angalau dakika 150 za shughuli zinazo fanya mtima wako na damu ipige kila wiki. Bila shaka, unaweza fanya hivi kwenye darasa za mazoezi. Lakini pia unaweza timiza haya kwa kutembea. Ni vyema pia kufanya mazoezi yanayo husisha misuli muhimu mwilini angalau mara mbili kwa wiki. Pia, unaweza jaribu kufanya mazoezi ya kukusaidia na mwendo mara mbili ama tatu kwa wiki kukusaidia unapo tembea.

Wakati ambapo dakika 150 huenda zikaonekana kama muda mrefu, sio lazima ufanye mazoezi haya kwa pamoja. Unaweza tembea dakika 10 karibu na nyumba ama utumie dakika 10 ukifagia kiwanja cha nyumba. Na dakika zako zitafika.

Ikiwa unahisi una nishati tosha, unapata manufaa zaidi ya kiafya ukifanya mazoezi dakika 300 kwa wiki.

Lakini lengo rahisi ni kujaribu kupata dakika 30 za mazoezi mazito siku nyingi. Unaweza kufanya hivi wiki zingine na kushindwa zingine. Kumbuka kuwa ni lengo na wala sio sharti. Fanya kinacho wezekana kwako.

Umuhimu wa mazoezi: Njia tofauti za kufanya mazoezi

umuhimu wa mazoezi

Kuna njia mbili za kutimiza lengo la damu na mtima kupiga. Kufanya mazoezi ama kufanya shughuli za kifizikia.

Mazoezi ambayo unaweza jihusisha katika ni kama vile kujiunga na darasa la mazoezi (gym), kuogelea, kupiga dondi ama michezo kama mpira wa vikapu.

Shughuli za kifizikia ni kazi zako za kila siku kama vile kuenda dukani, kuzungusha mnyama wako wa nyumbani, kutoa magugu shambani. Kuhusisha mambo haya mawili kwenye kazi zako za kila siku kutakusaidia kuwa na afya na kuishi maisha marefu. Lakini ni vyema wakati wote kuwasiliana na daktari wako kabla ya kufanya mazoezi mazito, hasa kama una matatizo yoyote ya kiafya.

Pia unaweza:

 • Endesha baiskeli
 • Kutembea
 • Kutumia kifaa cha kukata nyasi kupunguza urefu wa nyasi
 • Kucheza mchezo kama mpira wa tenisi
 • Kubeba vyakula kutoka sokoni

Unapaswa kuanza kuhisi una nguvu zaidi ama nishati baada ya wiki chache. Mazoezi ni muhimu sana katika kuwa na afya njema ya kifizikia, kihisia, na kiakili.

Soma Pia:Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

Written by

Risper Nyakio