Je, Nini Umuhimu Wa Michezo Ya Riadha Ya Timu?

Je, Nini Umuhimu Wa Michezo Ya Riadha Ya Timu?

Pre-teen and teenage years are often trying times for kids physically, emotionally and mentally. However, studies have shown that playing team sports can help them ward off depression.

Wakati wa umri wa chini ya miaka 13 na ujana, mabadiliko mengi ya mwili, hisia, kiakili na kijamii hutotokea.  Kwa sababu hii, wasiwasi na mkazo wa mawazo huenda yakatokea. Pia katika umri huu, mtoto wako anaweza kosa kukuambia kile anacho kipitia. Kwa bahati nzuri, utafiti umeonyesha  kwamba michezo ya riadha kama timu husaidia kupigana na mkazo wa mawazo.

Kucheza michezo ya timu kunaweza saidia watoto walio na mkazo wa mawazo.

michezo ya riadha

Timu Ya Voliboli Ya Wanawake Ya Nigeria

Utafiti unaonyesha kuwa kucheza michezo ya timu husaidia watoto walio na mkazo wa mawazo. Utafiti ulikua na lengo la kujua uhusiano uliopo kati ya afya ya kiakili na michezo ya timu. Watoto waliokuwa wamedhulumiwa utotoni mwao ndio waliohusishwa  kwenye utafiti huu. Majaribio haya yalikuwa kama vile maswala ya kihisia, kudhulumiwa kimapenzi, wazazi waliotumia dawa za kulevya na waliokuwa  na wazazi wasio wajibika. Uchunguzi ulionyesha kuwa mkazo wa mawazo ulikuwa chini kwa watu wazima ambao walijihusisha katika michezo ya timu, walipokuwa watoto.  Kucheza michezo ya timu kuliongeza nguvu za kiakili za watoto hawa walipokuwa wanaelekea kuwa watu wazima.

Kwa hivyo, kwa wazazi wasiowaruhusu watoto wao kucheza michezo, labda ni wakati wa kuabidilisha nyoyo. Wazazi wengi huogopa watoto wao wanaweza kuumia. Pia, kuna uwezekano wa kutoona haja hii kwani watoto wao hawataki kuwa wanariadha. Lakini mtoto wako kujihusisha na michezo sio lazima awe na tazamio la kuwa mwanariadha. Hata kama hakuna sababu kuu, mruhusu mtoto wako kucheza ajifurahishe. Kuna manufaa mengine ya kumwacha mtoto wako acheza katika timu. Michezo ya timu, hutengeneza hivi kwamba si juhudi ya mtu mmoja tu.  Ni juhudi za watu wengi ambao wanaazimia kufikia lengo moja. Kuna manufaa mengi katika michezo ya timu.

Manufaa ya michezo ya riadha ya timu 

michezo ya riadha

Haya ndio manufaa ya michezo hii kitimu:

  • Kuboresha afya ya akili

Watoto wako wataanza kujiamini mapema maishani mwao. Jambo hili litapunguza athari ambazo ujumbe usizofaa unaweza kuleta kwao. Jumbe zisizofaa huwa kila mahali na pia zinaweza kutokana na wazazi. Ujumbe huu usio faa ni kama vile, ujumbe kuhusu uzani, tabia, na kumlinganisha mtoto wako na wengine ambako hakufai.  Kwa bahati mbaya, haya mambo huathiri jinsi mtu anavyo jiheshimu. Huenda ikamfanya mtoto azidiwe na kusababisha  mkazo wa mawazo.  Hata hivyo, kucheza michezo ya timu huwawezesha watoto wako kuhisi kama wao ni sehemu ya kitu  kikubwa. Na hivi ikisaidia kukuza akili zao.

 

  • Kujenga stadi za kijamii

Kama watu wazima huwa vigumu kuunga na watu wengine. Pia si rahisi kufanya marafiki wapya au kujihisi mtulivu kataka mazingira mapya. Kwa hivyo, unaweza waza jinsi ilivyo vigumu kwa watoto wako pia. Lakini kucheza kwenye timu kunaweza kusaidia kurahisisha jambo hili.  Wanapo unganishwa na lengo moja kuu, huwa rahisi kwa watoto kufanya urafiki na wengine katika kundi hilo.

 

  • Kusitawisha sifa nzuri

Uzuri wa michezo ni kuwa mtashindana na kwa wakati mwingine, huenda utashindwa. Huo ndio ukweli. Wakati watoto wako wanapocheza kwenye timu, itawawezesha kukabiliana na kushindwa  kwa njia inayofaa. Pia huwafunza kujikusanya tena na kuendelea na maisha. Huu ndio ukweli wa jinsi maisha yalivyo. Unashindana, wakati mwingine unashinda, na, mwingine unashindwa.  Pia, kila mtoto lazima ajishindie mahali kwenye timu hivyo basi kusitawisha sifa nzuri.

 

  • Hujenga nidhamu na uwakfu

Kushinda katika michezo, lazima uwe na nidhamu na kujitolea kwa lengo kuu. Kwa urahisi, lazima uwe na jitihada kupita kiasi. Na hukana kitu ambacho hufunza jitihada kama timu inayojaribu kuafikia lengo moja. Watoto huwaangalia wenzao wanavyojitahidi na hili huwafanya kutaka kufanya zaidi. Ili kupata fanaka maishani, jitihada hizi ni muhimu. Haiumizi kujifunza mapema.

 

Nitamfunzaje mtoto wangu kupenda na kucheza kwenye timu?

kumhusisha mtoto wako katika michezo

  • Kufanya mazoezi ya msingi

Kama mambo mengi, jaribu vitu rahisi na mtoto wako.  Mchezo wowote ule mtoto wako anataka kucheza  ni vizuri kuanza mazoezi ya msingi. Lisaa limoja nje mkicheza ni sawa. Mwache afanye mambo ovyo ovyo.  Labda kukimbia au kupanda vitu.  Pia mwache mtoto aongoze.

  • Msifanye mambo nyingi.

Ni vizuri kufurahia kwamba mtoto wako anacheza michezo ya timu. Lakini usifanye vitu kwa wingi kama kumuunganisha na michezo mitano tofauti. Na pia hufai kumuunganisha mtoto wako na mchezo mmoja tu. Hii ni kwa sababu unaweza kumfanya mtoto wako aboeke. Ujanja uko katika kutafuta usawa. Hivi mtoto wako ana vipomo anavyoviweza.

  • Mwache mtoto wako afanye uamuzi

Mara nyingi jambo unalolitaka sio lile mtoto wako analitaka. Ama unamuunganisha mtoto wako na timu iliyo na rafiki zake. Hili huwa sio jambo la busara kila wakati ila muulize mtoto wako mchezo anao upendelea zaidi.

  • Mwelezee umuhimu wa uazimaji

Baada ya mtoto wako kujiunga na timu, Huenda ikawa vigumu kuliko ulivyo dhani.  Hili linaweza kumfanya mtoto wako afikirie kutoka.  Kwa hivyo mwelezee mtoto wako kuwa anafaa kumaliza hadi mwisho wa huo msimu. Katika huu umri, unamfunza mtoto wako kuwajibika.

  • Punguza kumlinganisha

Kumlinganisha mtoto wako na mwengine huleta mkazo usiohitajika.   Hii inaweza kumfanya mtoto wako ahisi kutoka. Mkumbushe kuchukua muda na kufikiria anacho taka. Pia makosa ni sehemu ya michezo ya timu.  Kwa hivyo kosa linapotokea unafaa kuwa pale kumtia nguvu.

Angalia kuwa hachoki. Mpe mtoto wako mianya. Watoto wanaposukumwa hadi mwisho wao huumia.  Huu huenda ukawa mwanzo wa mtoto kuchukia michezo ya riadha.

Read also: 20 Signs that you have a gifted child

Healthline. Cleveland Clinic

Written by

Risper Nyakio