Tendo la ndoa ni muhimu sana katika maisha. Kitendo hiki kina manufaa mengi ya kiafya, kijamii na pia kuendeleza vizazi. Wanandoa wanao jihusisha katika tendo hili mara kwa mara wana pata manufaa mengi na kuusaidia uhusiano wao kukua. Mbali na kuwa na wakati wa kujifurahisha na kuwa pamoja, kuna faida nyingi za kiafya zinazo ambatana na kujihusisha katika tendo hili. Tuna angazia umuhimu wa tendo la ndoa katika ndoa, kwa afya, akili na kijamii.
Umuhimu wa kufanya tendo la ndoa kwa afya

Tendo la ndoa lina husishwa na kupata watoto. Lakini, hii haifai kuwa sababu ya kipekee. Na wala sio kujitenga na kupata mimba isiyo tarajiwa ama maambukizi ya kingono. Tazama manufaa yake.
- Kuboresha mfumo wa kinga mwilini. Kulingana na utafiti ulio fanyika kati ya wanandoa. Walio fanya tendo hili zaidi walidhibitiwa kuwa na kiwango cha juu cha immunoglobulin(IgA) kwenye mate yao. Ikilinganishwa na watu walio fanya kitendo hiki mara zaidi ya moja kwa wiki. IgA ni muhimu sana katika kupigana dhidi ya magonjwa kama vile HPV.
- Kupunguza shinikizo la damu. Utafiti una husisha ngono na kupunguka kwa shinikizo la damu. Wanandoa wanaofanya kitendo hiki mara kwa mara, hawasumbuki na tatizo la shinikizo la juu la damu.
- Kupunguza viwango vya mawazo mengi. Kuwa karibu na mchumba kuna saidia kupunguza mawazo ya kujiliwaza. Wanandoa wanahisi hawana mawazo mengi, kwani wanaweza kuzungumza na mtu anaye waelewa vyema zaidi. Kugusana na kukumbatiana kuna ufanya mwili kuachilia kichocheo cha kuhisi vyema na kuwafanya wanandoa kuwa na amani na furaha zaidi.
Manufaa zaidi

Akili ya binadamu hufaidika kwa njia nyingi. Kuwa na maisha mazuri ya kingono kuna saidia wanandoa kuwa na maisha mema nyumbani na hata kazini. Kwa wasio kuwa na hamu ya kuingia kazini, kujihusisha kwa kitendo hiki kabla ya kuingia kazini kutasaidia kuboresha hisia zako.
Umuhimu wa tendo la ndoa katika ndoa sio kupunguza mawazo tu, mbali ni zoezi bora. Ni bora katika kuboresha uzalishaji na kupunguza uchungu wakati wa hedhi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Vyakula 5 Bora Zaidi Katika Kuongeza Hamu Ya Tendo La Wanandoa