Kila uhusiano ni muhimu katika kuendeleza ukuaji wa mtoto maishani mwake. Uhusiano unamsaidia kufahamu nyanja mbali mbali maishani. Je, unafahamu umuhimu wa uhusiano katika ukuaji wa mtoto? Soma zaidi.
Mazingira ya uhusiano ni muhimu sana hasa katika siku za mwanzo za ukuaji wa ubongo wa mtoto. Katika siku hizi, mtoto anaanza kukua kuwa mtu kamilifu katika nyanja zote za maisha. Uhusiano wa kwanza ulio muhimu zaidi ni uhusiano wa kinyumbani na wazazi. Mazingira ya uhusiano nyumbani yana jukumu kubwa katika maisha ya mtoto na mtu atakaye kua siku zake za usoni. Uhusiano kati ya mtoto na babu zake, shangazi, walimu na watu wengine wanao ishi naye ni muhimu pia.
Umuhimu wa uhusiano bora katika ukuaji wa mtoto

Uhusiano bora unamsaidia mtoto kuwa na vitu hivi:
Kila mtu huwa na jukumu katika maisha ya mtoto. Watoto wachanga huwatazamia watu wakubwa maishani mwao kama vile nyanya na babu zao kuwaongoza. Wanapo wahadithia hadithi za kale, wana tengeneza uhusiano wa kuaminika kati yao. Wanakuza uwezo wa kuwaamini watu walio karibu nao.
Mtoto husoma jinsi ya kuwa rafiki bora kutoka kwa watu walio karibu naye anapo kua, na uhusiano walio nao. Mtoto anapo kua pamoja na watu wanao aminika, walio wakweli, nafasi kubwa ni kuwa katika siku zake za usoni, atakuwa rafiki wa kuaminika.
Watoto pia hawasumbuki kutengeneza urafiki na watu wengine katika siku zao za usoni.

Watoto wanapokua wakifahamu kuwa wanaweza waambia wazazi wao jambo lolote, wanapata ujasiri wa kuwa na mazungumzo wazi nao. Mtoto anaye jua kuwa anaweza zungumza na wazazi wake mara nyingi huwajulisha kabla ya kufanya jambo. Wazazi watachukua chanya hiki kumshauri iwapo ni jambo la busara ama la.
Mtoto anapo jua kuwa kuna watu wanao mwamini na kumwegemeza, anapata ujasiri wa kufanya vitu vingi. Mtoto huenda akaanza kufuzu masomoni mwake kufuatia mahusiano yake.
Mahusiano bora huchangia pakubwa katika ukuaji wa mtoto. Ni vyema kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanatengeneza mazingira bora kwa ukuaji wa mtoto.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto: Mtoto Wa Mwezi Mmoja