Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Usafi Wa Sehemu Za Siri Kwa Watoto

Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Usafi Wa Sehemu Za Siri Kwa Watoto

Kupuuza umuhimu wa kusafisha sehemu za siri kwa watoto huenda kukasababisha madhara mabaya. Soma zaidi kufahamu jinsi ya kuwafunza watoto kuhusu kusafisha genitalia zao.

Tuna mojawapo ya mazungumzo ya wamama tukinywa kahawa. Yalikuwa mazungumzo ya ucheshi hadi rafiki yangu alipo jazwa na uwogwa kwa sekunde moja kabla ya kuniambia nisipuuze umuhimu wa usafi wa genitalia kwa watoto. Kijana wake hivi majuzi alikuwa amelazwa hospitali kufuatia maambukizi yaliyo sababishwa na kuto oshwa vizuri kwa sehemu zake nyeti. Huzuni!

Usafi wa sehemu za siri za watoto ni muhimu sana. Isivyo hivyo, huenda wakaugua aina fulani ya magonjwa. Unaona, seheumu hizi ni mahali pazuri pa viini kuzaana. Kwa hivyo hakikisha kuwa una waelezea watoto wako hivi.

Pia, ikiwa wewe ni mzazi aliye na kazi nyingi na msaidizi wako ama nyanya ya mtoto anawaosha, ni muhimu uangalie sehemu zao za siri mara kwa mara.

From a young age, tuna sisitiza kwa watoto kuwa wanapaswa kunawa mikono yao, uso na nywele. Tuna wa mwagilia vitakasio vya mikono na kuwaambia wasugue mikono yao kuua viini. Ila tunapaswa kusisitiza zaidi umuhimu wa usafi wa genitalia kwa watoto, wangali wachanga, ili wawe na tabia nzuri mapema.

Usafi wa genitalia ni muhimu kwa watoto hasa wanapokuwa katika umri wa miaka 6 hadi 11 kwani huu ndio umri ambapo sehemu zao huanza kukua.

Hapa kuna vidokezo kuhusu usafi wa genitalia kwa watoto.

Usafi wa genitalia kwa watoto -  wavulana

  • Ncha ya kibofu - Wakati ambapo sehemu chini ya ngozi ya juu inaweza songa kwa urahisi, inapaswa kusafishwa mara kwa mara. Mwonyeshe mvulana wako jinsi ya kuipeleka nyuma na kuisafisha. Kuwa makini usilazimishe ngozi ya juu mbali na ncha, kwa wakati unaofaa, itaanza kusonga nyuma.
  • Hakuna sabuni - mkumbushe mtoto wako asipake sehemu hiyo sabuni. Ni sehemu nyeti na hutaki awashwe siku nzima. Ukiona vitu vyeupe kwenye sehemu hiyo, vinajulikana kama smegma na sio kitu cha kuwa na shaka nacho.
  • Maambukizo - Kuwa mwangalifu kuona groin ringworm ama jock itch. Haya ni maambukizi ya kuvu ambayo hutokea zaidi wakati ambapo kuna joto. Pia hutokea kijana wako anapo valia nguo zinazo mbana kwa sana na sehemu ya genitalia haipati mzungumko mwema wa hewa. Ishara huwa kama vile kuwa mwekendu, lengelenge na kujikuna.

 

genital hygiene for kidsUsafi wa genitalia kwa watoto - wasichana

  • Hakuna kitu zaidi -  Sehemu ya uke hujisafisha mbali na kuoshwa mara kwa mara, uke hauhitaji kitu chochote zaidi.
  • Usiingize kitu chochote - Kuingiza kitu chochote kwenye uke (kama vile vitu vya kusafisha) huenda kuka haribu ngozi hiyo laini. Pia kuna sababisha viini kuingia na kuambukiza sehemu hiyo. Kwa hivyo msisitizie msichana wako kuwa laini sana na makini na sehemu zake za kike.
  • Kutoka mbele kwenda nyuma - Kumbuka, kuosha kutoka mbele hadi nyuma. Hii inasaidia kuepuka viini vyoyote kutoka sehemu ya nyuma kufikia seheumu ya uke.
  • Mazungumzo ya hedhi - Wanapo endelea kuwa na umri zaidi, ongea nao kuhusu vipindi vya hedhi na jinsi ilivyo muhimu kwao kutunza sehemu zao za kike katika wakati huo. Wakumbushe kuwa hai shauriwa kuosha sehemu hizo sana katika kipindi hicho. Mara moja kwa siku ni sawa. Usisahau kuwafunza wasichana wako kuhusu kubadilisha pedi za hedhi mara kwa mara.

usafi wa genitalia kwa watotoUsafi wa sehemu nyeti kwa watoto - jinsi ya kuanza mada hii

Wanapo zidi kuwa na umri zaidi, wana anza kujitenga na mazungumzo kuhusu sehemu zao za genitalia, hata usafi. Ni vyema uongee nao kuhusu umuhimu wa usafi na uanzishe mada ya umuhimu wa usafi wa genitalia kwa watoto.

Kwa watoto wachanga, waeleze kuwa kuna viini mwilini wao wote na mwili wao hula seli zilizo kufa (kama jasho). Bakteria husababisha harufu mbaya na hakuna anaye taka kuwa karibu na mtu anaye nuka vibaya. Kwa hivyo wanapaswa kujisafisha mara kwa mara ili kutoa bakteria na kunukia vizuri na kuwa wenye afya!

Kumbuka, usipuuze umuhimu wa mazungumzo haya ya usafi wa sehemu nyeti kwa watoto. Sio jambo ndogo kupata maambukizi huko chini!

Chanzo: World of Moms 

Soma pia: Sababu Kwa Nini Kutibu Viini Kwa Watoto Huenda Kukakutatiza

Written by

Risper Nyakio