Jinsi Ya Kufunza Watoto Kuhusu Usafi Wa Mwili

Jinsi Ya Kufunza Watoto Kuhusu Usafi Wa Mwili

Usafi wa mwili kwa watoto ni muhimu sana kwao na afya yao. Fahamu baadhi ya vitu vya kimsingi vya kuwafunza!

Kuwafunza watoto wako vitu vya kimsingi kuhusu usafi wa mwili kwa watoto ni muhimu kwa kuwaweka wakiwa wasafi na wenye afya. Ni muhimu kwa watoto wako wachanga kuzingatia usafi mzuri- kunawa mikono hasa - kwa sababu wanatumia wakati mwingi sana wakiwasiliana kwa karibu na watoto wengine darasani, wakitumia kila kitu kwa pamoja kutoka kwa dawati, kwa vitu, kalamu za rangi hadi kwa viini. Mtoto wako anapokuwa na umri wa makamu, mabadiliko ya homoni husababisha utoaji mwingi wa mafuta mwilini na harufu ya mwili. Utakuwa na furaha kujua huku ngoja hadi wakati huo kuwafunza afya bora na tabia nzuri za usafi. Kuwafunza watoto kuhusu usafi wa kibinafsi huewezi sisitizwa vya kutosha.

Baadhi ya vitu vya kimsingi vya usafi wa mwili kwa watoto

Kunawa mikono

Jinsi Ya Kufunza Watoto Kuhusu Usafi Wa Mwili

 

Kumfunza mtoto wako jinsi ya kunawa mikono huenda ikawa tabia muhimu zaidi ya afya na usafi wa afya. Fikiria kuhusu bidhaa zote tofauti na mahali unaweza gusa kila siku. Kunawa mikono, bila shaka ni mojawapo ya njia bora zaidi za kuepuka maradhi na kuzuia viini kusambaa. Hakikisha kuwa mtoto wako anatumia sabuni kwa angalau sekunde 15- mfereji ukiwa hauja funguliwa ili kuhifadhi maji- kabla ya kusuuza. Sharti la lazima kukumbuka ni kunawa mikono yako kwa wakati unao takikana kuimba "Happy Birthday" mara mbili.

Mhimize mtoto wako kunawa mikono yake na maji na sabuni:

  • wakati mikono yako inakaa imechafuka
  • kabla ya kula ama kutayarisha chakula
  • baada ya kugusa nyama mbichi, kama vile ya kuku ama ng'ombe
  • punde tu baada ya kugusa wanyama
  • Ukimaliza kuchemua, kukohoa ama kupigwa chafya
  • baada ya kugusa vitu kama damu, mkojo ama kutapika
  • Ukitoka msalani

Kuchemua na kukohoa

Jinsi Ya Kufunza Watoto Kuhusu Usafi Wa Mwili

Viini huenda mbali. Huenda ukawa unafahamu kuwa kuchemua huwa na mwendo wa angalau maili 100 kwa saa na kunaweza tuma viini 100,000 kwenye hewa. Utafiti unaonyesha kuwa kuchemua na kukohoa kuna weza kuwa na mwendo wa hadi mara 200 zaidi kuliko ilivyo dhaniwa hapo awali. Mfunze mwanao tabia ya kufunika mdomo wake na mapua kwa kutumia tishu ama upande wa ndani wa kiwiko chake anapo kohoa ama kuchemua.

Macho, mdomo na mapua

Jinsi Ya Kufunza Watoto Kuhusu Usafi Wa Mwili

 

Viini husambaa kwa urahisi kwenye mwili kupitia kwa mucous membrane kwenye macho, mapua na mdomo. Mkumbushe mtoto wako kutogusa macho na mapua yake ovyo.

Usafi wa meno

usafi wa meno kwa watoto - meno

Watoto wa shule huwa na uwezo wa mwendo tosha wa kufanya kazi ya kusugua meno yao wenyewe, hata kama huenda bado ukahitajika kuwasaidia hadi wanapo fika umri wa miaka 6 ama 7. Mfunze mtoto wako tabia ya kusugua meno na ulimi, ndani ya mdomo na mwanzo wa meno. Tumia saa kuwa himiza kusugua meno kwa muda mrefu, na ufanye jambo linalo wavutia ili watumie muda mrefu kusugua.

Wakati wa kuoga

usafi wa mwili kwa watoto

 

Wazazi wengi hupata kuwa kuosha mwili wakati wa jioni ni njia nzuri ya kupumzisha mtoto kabla ya kuenda kulala. Kumwosha wakati wa jioni kunaweza saidia kupunguza upele wa asubuhi. Baadhi ya watoto hupendelea kuoga kwa shower ambayo hupunguza wakati baada ya kutoka shuleni ama wanapo enda shuleni. Pia maji mengi yana hifadhiwa. Watoto wengi wanaweza jiosha kuanza kwa umri wa miaka 6. Huenda ukataka kumsimamia akioga na kujisuuza hadi anapo kuwa stadi wa kujiosha. Na kuwa hakika kuweka mkeka salama kuepuka ajali za kuanguka kwenye sakafu iliyo na maji wanapo maliza.

Watoto wanahitaji kuoga mara kwa mara.  Unaweza himiza kuoga mwisho wa siku kama sehemu ya ratiba yao ya kulala. Hakikisha kuwa mtoto wako anaosha mwili wao wote, ukihusisha chini ya mikono yao na genitalia, upande wa nyuma na kuwa mwili wao umekauka vyema kabla ya kuvalia nguo.

Nguo na viatu

Watoto wanahitaji nguo safi kila siku, hata kama nguo zao za kitambo hazinuki. Safisha chupi zao kila siku ni muhimu sana. Wewe (ama wakiwa wa umri tosha) unaweza anika sare zao za kushele kupigwa na upepo wanapofika nyumbani kila siku.

Huenda ukahitajika kumfunza mwanao tabia za usafi mzuri wa mwili. Hii itakuwa muhimu zaidi wanapo endelea kukua na kufika umri wa makamo. Kuweza kuongea kwa uwazi na uaminifu kuhusu kuwa msafi kutakusaidia kudhibiti mambo magumu zaidi ya usafi wa mwili ambayo yata ibuka wakiwa na umri wa mkubwa.

Kumbukumbu: VeryWellFamily

Soma pia: Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Usafi Wa Sehemu Za Siri Kwa Watoto

Written by

Risper Nyakio