Je, Usingizi Ni Muhimu Kwa Afya?

Je, Usingizi Ni Muhimu Kwa Afya?

Watu wanafahamu umuhimu wa lishe bora na kufanya mazoezi ili kuisha maisha yenye afya. Ila, wanapuuza umuhimu wa kupata usingizi tosha ili kuepuka magonjwa.

Je, ubora wa usingizi wako ni upi? Unapata angalau masaa manane ya usingizi usio katizwa kila siku? Natumai unapata usingizi tosha kwa sababu utafiti mpya unakisia kwamba kuna uhusiano kati ya usingizi na afya. Tuna lenga kukuelimisha kuhusu umuhimu wa usingizi kwa afya.

Tunaishi kwa dunia ambayo ina mambo mengi na yote yanaenda kasi na ambapo pesa zimepatiwa kipau mbele. Wakati hautoshi kwa binadamu yeyote yule na kila mtu anajaribu kufanya mengi awezavyo na wakati wake. Wakati unao tengwa wa kulala umezidi kupunguka na sio jambo jipya kusikia mtu akisema kuwa amekuwa akipata masaa mawili ya usingizi kila siku.

Wakati ambapo dunia inafahamu faida za kula vyema na kufanya mazoezi, umuhimu wa kupata usingizi tosha bado unahitaji kuelimishwa zaidi kwa watu. Watu wengi hawaelewei umuhimu wa usingizi kwa afya.

Usingizi tosha una husisha nini?

kupata usingizi unapo shindwa

Baadhi ya watu wanahitaji usingizi mwingi ikilinganishwa na wengine na hii inalingana na umri wa mtu. Kulingana na kituo cha kudhibiti magonjwa, watoto wachanga wa umri wa miezi kati ya 0-12, wanahitaji usingizi mwingi wa kati ya masaa 12- 17. Wanao tembea na wanao ingia shuleni wa miaka 1-5, wanahitaji masaa angalau 10-15 ya kulala. Watoto wa umri kati ya miaka 6-12 wanahitaji kati ya masaa 9-12 ya usingizi. Watu wachanga wa umri wa miaka 12-18 wanahitaji masaa kati ya 8-10 ya usingizi. Na watu wazima wa miaka zaidi ya 18 wana hitaji masaa 7 ya usingizi.

Hapa chini kuna orodha ya umuhimu wa usingizi kwa afya

  1. Kuboresha mfumo wa kinga

Katika masaa ya kufanya kazi, mwili wote una kwazwa kifikira. Kulala kuna ukubalisha mwili kupumzika na kupona kutokana na uchovu. Kati kati ya utaratibu huu wa kupona ni mfumo wa kinga ambao jukumu lake ni kulinda mwili kutokana na maradhi. Ikiwa una shangaa kwa nini usingizi ni muhimu kwa afya, una jibu lako sasa.

2. Kuepuka kufilisika kimawazo

Baadhi ya utafiti umeonyesha kuwa kuna uhusiano kati ya afya ya akili na mitindo ya kulala. Somo lililo chapishwa kwenye jarida la Australian and New Zealanda Journal of Psychiatry lilionyesha kuwa watu wanaoteseka kutokana na changamoto za kulala mara nyingi huwa wame filisika kimawazo.

Somo lingine lililo onekana kwenye JAMA Psychiatry na lililo angazia mitindo ya kujiua kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 lilipata kuwa usingizi ulichangia kwenye vifo hivo. Ni wazi kwa nini usingizi ni muhimu kwa afya.

3. Unaweza kusaidia kuwa na uzito mdogo wa mwili

Kuna utafiti unao pingana kwenye kurasa inayo ongea kuhusu usingizi na uzito wa mwili. Wakati ambapo utafiti mwingi kwa miaka mingi unaonyesha aina ya uhusiano kati ya usingizi na uzito zaidi wa mwili, mtaalum hivi majuzi alishuku utafiti wa hapo kale kwa kukosa kuangalia hali zingine kama kisukari, unywaji wa pombe na kukosa kufanya mazoezi na kadhalika.

Hata kama uhusiano kati ya wanao kosa usingizi na uzito wa mwili sio wazi, jambo moja ambalo ni wazi ni kuwa, kukosa usingizi kuna athiri uwezo wa mwili wa kuwa na mtindo wenye afya wa maisha.

4. Unakusaidia kuongeza utendaji kazi wako

umuhimu wa usingizi kwa afya

Uhusiano kati ya usingizi na utendaji kazi ume julikana kwa muda mrefu na wana biashara. Mfanyakazi anaye lala vyema ana utendaji bora kazini. Baadhi ya wana biashara wame husisha vipindi vifupi vya kulala kwenye ratiba ya kazi ya wafanyakazi wao ili kuwakubalisha kupata nyingi kutoka kwa usingizi.

5. Kusikiliza kwa makini 

Masomo ya utafiti yame onyesha kuwa mitindo ya kulala ina adhiri utendaji kazi wako na uwezo wako wa kusikiliza na pia akili yako. Somo lililo onekana kwenye jarida la Child Psychology na Psychiatry lili onyesha uhusiano kati ya mitindo ya watoto ya kulala na kufuzu kwao kwenye masomo.

6. Kulinda moyo kutokana na magonjwa 

Kazi ya moyo mwilini ni kupampu damu na hewa kwenye mwili siku yote. Kwa sababu hii, moyo una shinikizo hasa tunapo fanya kazi ama kufanya mazoezi.

Wakati wa kulala, utendaji kazi wa moyo unapunguzwa sana. Kadri unavyo lala, ndivyo moyo wako unavyo pata kupumzika. Usingizi tosha umejulikana kupunguza shinikizo la damu ambayo ni mojawapo ya sababu zinazo fanya moyo kuugua. Ripoti iliyofanywa na kituo cha kudhibiti magonjwa na matibabu unaonyesha kuwa usingizi tosha unasaidia mwili kudhibiti shinikizo la damu.

7. Kuepusha maradhi ya gastro intestinal

Baadhi ya masomo yameonyesha uhusiano kati ya kutopata usingizi tosha na kufura kwa tumbo. Utafiti ulio fanywa na World Journal of Gastroenterelogy ulionyesha kuwa kukosa usingizi tosha kunaweza sababisha maradhi ya gastro intestinal

Kukosa usingizi tosha kuna athari hasi. Na kuna athiri afya na maisha yako na pia kukuweka katika hatari ya kupata maradhi hasi.

Vyanzo: healthysleep.med.harvard.edu

Soma Pia:Mambo Ya Kufanya Unapo Tatizika Kupata Usingizi Usiku

Written by

Risper Nyakio