Uzazi wa mpango ni maamuzi ya mtu ama wanandoa kuhusu wakati watakapo jifungua, idadi ya watoto watakao pata na baada ya muda upi. Kuna umuhimu wa uzazi wa mpango mwingi, kwa mwanamke, mwanamme, mtoto na hata familia na jamii kwa ujumla.
Umuhimu wa kupanga uzazi wa kijumla

- Kumsaidia mama kurejelea hali yake ya hapo awali kabla ya kupata mimba
- Kuzuia mimba isiyo tarajiwa
- Kuwasaidia wanandoa kujipanga kifedha na kihisia watakapo jifungua
- Kuwawezesha wanandoa kuwahudumia watoto wao vyema wanapo zaliwa
- Kumpa mama wakati tosha wa kujipanga kimaisha na kufanya mambo mengine kama vile masomo, ama biashara
- Kumwezesha mama kuwa hudumia watoto wengine
- Kuisaidia nchi kukuza uchumi wake
- Kupunguza idadi ya watu walio ulimwenguni
Njia za kupanga uzazi na faida kwa mwanamke
Faida: Kuboresha mzunguko wa hedhi na kuufanya uwe wa kawaida zaidi
Kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa saratani ya kizazi, ama ya ovari
Kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa mzunguko wa hedhi
Faida: Kulinda dhidi ya kupata maambukizi ya zinaa kama vile herpes na gonorrhoea

Faida: Kuongeza uzito kwa wanao tatizika na uzito wa chini
Kupunguka kwa idadi ya damu inayo toka katika kipindi cha hedhi
Kupunguza uzani kwa wanao tatizika na uzito mwingi (hutofautiana kati ya watu)
Wanao paswa kutumia uzazi wa mpango
Mtu yeyote yule aliye fikisha umri wa kujifungua kwa wanawake anapaswa kutumia uzazi wa mpango. Ikiwa wangali wachanga na wako shuleni, wanapaswa kuzungumza na wazazi wao. Wavulana ambao hawaja oana wanapaswa kutumia kondomu wanapo fanya mapenzi.
Kupanga uzazi kuna faida nyingi kwa mwanamke, mwanamme, watoto na jamii kwa ujumla. Ili wanandoa wafahamu mbinu itakayo wafaa zaidia ya kupanga uzazi, ni vyema kuwasiliana na daktari. Ataweza kuwashauri kuhusu mbinu iliyo bora zaidi kwao. Wanawake wanaweza nufaika kutokana na umuhimu wa uzazi wa mpango hasa katika kusawazisha hedhi yao.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Njia Tofauti Za Kuzuia Mimba Kama Vile Kwa Kutumia Chumvi!