Wanawake: Ishara Hizi Zitakusaidia Kujua Kuwa Unamtosheleza Mwanamme Wako Kimapenzi

Wanawake: Ishara Hizi Zitakusaidia Kujua Kuwa Unamtosheleza Mwanamme Wako Kimapenzi

Somo lililo chapishwa katika Makala ya Tabia Za Kimapenzi, lili onyesha kuwa wanandoa wanao toshelezana kimapenzi wanapenda kukumbatiana.

Baadhi ya wakati, huenda ikawa ni vyema kujitenga na ngono kuliko kufanya ngono isiyo watosheleza. Hakuna kitu kizuri kuliko kufahamu kuwa juhudi zako za kumfurahisha mwanamme wako kimapenzi hazi ambulii patupu. Wakati ambapo kuwa na mazungumzo wazi na mchumba wako ni mojawapo ya njia za kufahamu ikiwa unamtosheleza mume wako kimapenzi. Kuna ishara ambazo pia huenda zika kusaidia kung'amua jambo hili.

Unajua kwa sababu, baadhi ya wakati, huenda akawa anasema kuwa unamtosheleza ili asiumize hisia zako ama kukufanya uhisi vibaya.

Kuna ishara za kipekee zitakazo kusaidia kujua ikiwa anamaanisha anacho sema ama anasema ili alinde hisia zako. Endelea kusoma makala haya upate maarifa zaidi.

Je, Unamtosheleza Mume Wako Kimapenzi Ama La?

unamtosheleza mume wako kimapenzi

  1. Ana kukumbatia baada ya kipindi chenu cha mapenzi

Somo lililo chapishwa katika Makala ya Tabia Za Kimapenzi, lili onyesha kuwa wanandoa wanao toshelezana kimapenzi wanapenda kukumbatiana, kushikana na kuwa na muda wa pamoja baada ya ngono.

Ana kukumbatia baada ya mapenzi ama ana pinduka upande tofauti na kulala? Ni ishara kuwa ana furahikia mapenzi yenu.

2. Mapenzi yenu yamenoga

Wanaume wasio toshelezwa kingono hawaonyeshi mapenzi kwa wenzi wao. Hii ni kwa sababu uhusiano wao kwa jumla una athiriwa na kuto toshelezwa kingono.

Kwa hivyo anapo kuonyesha mapenzi, bila shaka unafanya jambo linalo stahili.

Wanawake: Ishara Hizi Zitakusaidia Kujua Kuwa Unamtosheleza Mwanamme Wako Kimapenzi

3. Ana ringa kuhusu weledi wako

Ikiwa wewe ni mweledi na unamtosheleza anavyo paswa, bila shaka hata koma kuringa kuhusu ustadi wako.

4. Kufanya mapenzi mara kwa mara

Unapo pata kuwa mchumba wako anaanzisha ngono mara kwa mara, hata mnapo kuwa na dakika chache kabla ya kuenda mahali ama kutoka kwenye nyumba. Hiyo ni ishara kuwa anapenda tendo hilo nawe sana. Ikiwa hangekuwa anafurahia uhusiano wenu mnapo fanya kitendo kile, bila shaka hangetia juhudi kuanzisha tendo lile mara kwa mara.

Kumbuka kuwa hizi ni ishara tu, ikiwa una shaka, zungumza kwa undani na mchumba wako, mwelezee hisia na shaka zako na kwa njia hii, huenda akakueleza mahali anapo hisi kuwa kuna doa. Kufanya mapenzi ni kuhusu wachumba wawili kuelewana na kujua kinacho mfurahisha mwingine kisha kutia juhudi kuhakikisha kuwa matakwa ya kila mtu yana toshelezwa.

Soma PiaMakosa 5 Ya Kingono Ambayo Wanaume Hufanya!

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio