Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6

3masomo ya dakika
Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6

Hakikisha una maji tosha mwilini. Mwili wako hautafanya kazi vizuri ukiwa na ukosefu wa maji tosha. Huenda ukashindwa kuchakata maziwa tosha ya mtoto wako.

Unapaswa kunyonyesha mtoto miezi mingapi? Bila shaka hili ni swali ambalo huwa tatiza wamama wengi wa mara ya kwanza. Kunyonyesha ni suala binafasi lakini ambalo litakuwa na maoni mengi kutoka kwa famikia na marafiki. Baadhi yao hufikiria kuwa kuna umri hasa. Wengine wana amini kuwa mtoto anapaswa kunyonyeshwa vyema iwezekanavyo. Lakini haya yote ni maoni tu. Mwongozo mwafaka ambao wamama wanapaswa kufuata ni upi?

Kweli ni kuwa hakuna sharti gumu na linalo fuatwa kuhusu muda unao paswa kunyonyesha, ila wataalum wa matibabu wana ushauri wa wakati, kulingana na manufaa ya kiafya. Hasa, wataalum hawa wana shauri kunyonyesha kwa angalau miezi 6.

Muda huu huwa na manufaa ya kiafya kwa mama na mtoto. Kwa mama ni kama vile kupunguza uzito wa mwili baada ya kujifungua, kupunguza hatari za maradhi ya moyo, kisukari na aina zingine za saratani.

Unapaswa kunyonyesha miezi mingapi?

Unapaswa kunyonyesha mtoto miezi mingapi

Utafiti mpya umepata kuwa wamama wanao nyonyesha kwa angalau miezi sita ama zaidi wanaweza kuwa na ufuta mchache kwenye maini yao. Na kupunguza hatari za kutatizika na NAFLD(non-alcoholic fatty live disease). Mara nyingi ugonjwa huu una husishwa na uzito wa kupindukia wa mwili na baadhi ya matatizo ya kula.

Watafiti walifuata wanawake 844 kwa miaka 25 baada ya kujifungua. Katika mwisho wa utafiti, wanawake hao walikuwa na miaka 49 na zaidi.

Waligundua kuwa wanawake walio nyonyesha watoto wao kwa angalau miezi 6 walikuwa na asilimia 52 chache za kupata maradhi ya maini ikilinganishwa na wamama ambao wali nyonyesha kwa muda chini ya mwezi mmoja. Karibu asilimia 6 ya wanawake kwenye utafiti huo wali ugua NAFLD.

"Matokeo haya yana changia kwa mwili wa ushuhuda unao kua na kuonyesha kuwa kunyonyesha mtoto humpa mama faida nyingi za kiafya," alisema kiongozi wa utafiti huo daktari Veeral Ajmera kutoka Chuo Kikuu cha California huko San Diego.

Mazoezi na vidokezo vya kunyonyesha

exercise at home during coronavirus

Utafiti huu una jibu swali la "unapaswa kunyonyesha mtoto miezi mingapi?" Cha kufurahisha ni kuwa pia uligundua kuwa wanawake wanao nyonyesha muda mrefu wana mitindo ya maisha yenye afya. Hii huenda ikawa ilichangia katika kupunguza hatari za kuugua NAFLD kwani shughuli za kifizikia husaidia kuboresha ugonjwa wa ufuta wa maini.

Pia, uligundua kuwa wanawake wanaofanya mazoezi huonekana kunyonyesha kwa vipindi virefu zaidi. Kwa hivyo ikiwa una panga kunyonyesha kwa muda mrefu, ni vyema uanze kufanya mazoezi.

Yote unayo hitaji kujua kuhusu kufanya mazoezi na kunyonyesha:

  • Kufanya mazoezi haku athiri utoaji wa maziwa. Tafuta mazoezi mepesi. Baadhi ya masomo yame onyesha kuwa kufanya mazoezi mazito kunaweza badili viwango vya lactic acid kwenye maziwa ya mama na kuathiri ladha yake
  • Usikose kula kalori. Mwili wako lazima ufanye kazi kutengeneza maziwa ya mama. Na kufanya hivi kunachoma kalori. Utatumia kalori nyingi unapo fanya mazoezi kwa hivyo tia hilo akilini. Kwa hivyo kula lishe bora iliyo na kalori
  • Hakikisha una maji tosha mwilini. Mwili wako hautafanya kazi vizuri ukiwa na ukosefu wa maji tosha. Huenda ukashindwa kuchakata maziwa tosha ya mtoto wako. Kwa hivyo kuwa makini na mwili wako na ugundue unapo hisi kiu.

Kwa sasa kwani unafahamu miezi unayo paswa kunyonyesha, ni wakati wa kuanza kufanya mazoezi pia!

Vyanzo: Reuters, The US National Library of Medicine, Aaptiv

Soma Pia:Mara 3 Ambapo Ni Sawa Kukoma Kunyonyesha Mtoto

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Feeding & Nutrition
  • /
  • Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6
Gawa:
  • Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kukosa Maji Tosha Mwilini Ukiwa Na Mimba

    Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kukosa Maji Tosha Mwilini Ukiwa Na Mimba

  • Ratiba Ya Chakula Cha Mtoto Wa Miezi Sita

    Ratiba Ya Chakula Cha Mtoto Wa Miezi Sita

  • Faida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa Mama

    Faida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa Mama

  • Ishara Kuwa Mtoto Wako Hapati Maziwa Tosha Ya Mama

    Ishara Kuwa Mtoto Wako Hapati Maziwa Tosha Ya Mama

  • Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kukosa Maji Tosha Mwilini Ukiwa Na Mimba

    Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kukosa Maji Tosha Mwilini Ukiwa Na Mimba

  • Ratiba Ya Chakula Cha Mtoto Wa Miezi Sita

    Ratiba Ya Chakula Cha Mtoto Wa Miezi Sita

  • Faida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa Mama

    Faida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa Mama

  • Ishara Kuwa Mtoto Wako Hapati Maziwa Tosha Ya Mama

    Ishara Kuwa Mtoto Wako Hapati Maziwa Tosha Ya Mama

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it