Unapaswa Kufanya Nini Unapo Jipata Na Mimba Isiyo Tarajiwa

Unapaswa Kufanya Nini Unapo Jipata Na Mimba Isiyo Tarajiwa

Mimba isiyo takikana huwa chanzo cha shaka na kiwewe kwa mwanamke ambaye hako tayari kifizikia, kihisia na kisaikolojia kuwa mama.

Kulingana na takwimu, karibu nusu ya mimba huko Umarekani huwa bila kupangwa. Idadi huwa juu pia katika nchi za Afrika. Mimba isiyo takikana huwa chanzo cha shaka na kiwewe kwa mwanamke anaye husika. Mwanamke anapo pata mimba bila kuwa tayari kifizikia, kihisia na kisaikolojia kuwa mama, na huenda akajipata akifanya utafiti kujua uamuzi atakao fanya.

Mimba isiyo takikana inaweza kuwa na athari ya kubadilisha maisha ya mtu yeyote yule. Lakini kabla ya kuangazia jinsi ya kukabiliana nayo, ina maana gani?

Mimba isiyo takikana ni nini hasa?

mimba isiyo takikana

Healthline ina fafanua kauli hii kama kisa ambacho mwanamke mwenye mimba hataki ama hayuko tayari kuwa mama.

Vyanzo vya mimba isiyo tarajiwa

Kulingana na watu wengi, kufanya mapenzi bila kinga huwa chanzo kikubwa cha wanawake kupata mimba wasipokuwa tayari. Lakini hii siyo sababu pekee inayo sababisha mwanamke kupata mtoto angali hayuko tayari.

Vyanzo vya mimba isiyo pangiwa

  • Kutofanya kazi kwa vidhibiti uzalishaji
  • Kuto fuzu kwa mbinu za kupanga uzazi
  • Kufanya mapenzi bila kinga
  • Kubakwa
  1. Kufeli kwa mbinu za kudhibiti uzalishaji

Inapofika kwa vidhibiti uzalishaji, kuna aina nyingi tofauti. Mtu anaweza amua kutumia kondomu za kike ama za kiume, kumeza tembe, sindano ama intra-uterine devices. Kila mbinu huja na onyo lake kuwa haina uhakika wa asilimia 100. Na kumaanisha kuwa mwanamke bado anaweza pata mimba hata baada ya kuzitumia.

2. Kuto fuzu kwa mbinu za kupanga uzazi

Wanawake wengi wanaweza tabiri vyema kupata mimba ama mimba isiyo tarajiwa kwa kuhesabu mzunguko wa kipindi cha hedhi na kufahamu siku zao za kupevuka kwa yai na wakati wanapo kuwa na rutuba zaidi. Kufuata hedhi yako kuna kusaidia kung'amua wakati ambapo ni salama kufanya mapenzi bila kupata mimba ama wakati bora zaidi kwako kupata mimba.

Muda wa wastani wa kipindi cha hedhi huwa siku 28. Ila siku hizi hutofautiana kwa wanawake. Mzunguko huanza siku ya kwanza ya hedhi na kuisha siku ya kwanza ya kipindi kijacho. Kipindi chenye rutuba huanza siku tatu kabla na baada ya siku yako ya 14. Siku yako ya ku ovulate ikiwa siku ya 14 kutoka siku yako ya kwanza ya kipindi chako cha hedhi. Mbinu hii haina kinga asilimia 100, kwani manii yana uwezo wa kudumu mwilini hadi siku nne. Na kumaanisha kuwa mwanamke anaweza pata mimba hata kama alifanya mapenzi mwisho katika siku zake salama.

3. Kufanya mapenzi bila kinga

Kufanya ngono bila kutumia njia yoyote ile ya kupanga uzazi ni njia dhabiti ya kupata mimba isiyo tarajiwa. Kutumia mbinu za kudhibiti uzalishaji hakuta ondoa kwa asilimia 100 shaka ya kutunga, lakini kutapunguza kwa njia kubwa. Na mimba sio jambo la pekee la kuwa na shaka kuhusu. Kuna magonjwa kama ukimwi unao sambaa kupitia kwa ngono bila kinga na haina tiba. Huenda pia ukapata maambukizi kama vile gonorrhea ama syphilis na mengine mengi.

4. Kubakwa

Kubakwa ni pale ambapo mtu wa jinsia moja ana lazimisha mwingine katika kitendo cha wanandoa ama ngono bila ruhusa yake. Kumbuka kuwa, hata kama wanawake ndiyo wanao fahamika kubakwa sana, wanaume pia hubakwa. Ila, mwanamke anapo bakwa, ndipo tunapo kuwa na kisa cha mimba isiyo tarajiwa. Unapo bakwa, hakikisha kuwa una ripoti kwa kituo cha polisi na kisha kwenda hospitalini kupata dawa za kukulinda dhidi ya ukimwi (PEP). Kisha hakikisha kuwa unaenda kupata ushauri kwani tendo hili huenda lika kuathiri pakubwa.

Athari za mimba isiyo pangwa

mimba isiyo pangwa

Ni chaguo la mwanamke anacho taka kufanya anapo jipata na mimba ambayo haja pangia. Huenda mambo yafuatayo yaka tendeka:

  • Akafilisika kimawazo
  • Kupata kiwewe
  • Kuwa na shaka
  • Mawazo mengi
  • Matatizo ya kifedha

Unapo jipata na mimba isiyo pangwa

Mwanamke nchini Kenya ana uhuru wa kutoa mimba ikiwa maisha ya mama iko hatarini. Na kutoa mimba nje ya kituo cha hospitali huwa na athari hasi kwa afya mama na huenda akaaga kwa mchakato huo.

Hakikisha kuwa unafikiria kwa makini kabla ya kufanya uamuzi wowote ule. Na ukiamua kuweke ujauzito huo, una hitaji usaidizi mkubwa kutoka kwa watu walio karibu nawe, kukabiliana na athari zile.

Soma Pia:Kuna Uwezekano Wa Kupata Mimba Unapo Nyonyesha?

Vyanzo: Opinion Front

Healthline

US National Library of Medicine

US Department of Health Services

NHS

lawpadi.com

Written by

Risper Nyakio