Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Kuna Uwezekano Wa Kupata Mimba Unapo Nyonyesha?

3 min read
Kuna Uwezekano Wa Kupata Mimba Unapo Nyonyesha?Kuna Uwezekano Wa Kupata Mimba Unapo Nyonyesha?

Kunyonyesha kuna linda dhidi ya kiwango cha kupevuka kwa yai. Lakini katika kipindi chako cha hedhi, kuna uwezekano wa kupevuka kwa yai na kupata mimba.

Ikiwa umejifungua mtoto hivi majuzi, akili yako huenda ikawa na maswali chungu nzima. Hasa ukitaka kujua zaidi kuhusu maisha mapya ya kuwa mama. Kutaka kujua kama mtoto wako anapata maziwa tosha na wakati utakapo anza kulala vizuri usiku. Mojawapo ya maswali makuu ambayo wanawake wanao nyonyesha ni kama unaweza pata mimba unapo nyonyesha. Huenda ukawa umesikia kuwa kunyonyesha kuna fanya kazi sawa na vidhibiti uzalishaji.

Unaweza pata mimba unapo nyonyesha?

unaweza pata mimba unapo nyonyesha

 

Jibu ni ndiyo. Kunyonyesha kuna linda dhidi ya kiwango cha kupevuka kwa yai. Lakini katika kipindi chako cha hedhi, kuna uwezekano wa kupevuka kwa yai na kupata mimba kabla ya kupata kipindi chako cha hedhi.

Mama anapo nyonyesha pekee na mara kwa mara, kuna nafasi ndogo kuwa yai lake litapevuka hadi pale atakapo anza kumlisha mtoto chakula kingine. Lakini imani hapa ni kuwa, huku kuna fanya kazi kwa mama anaye nyonyesha pekee. Na sio wanawake wanao walisha watoto wao kitu kingine mbali na maziwa ya mama. Unapo nyonyesha mara kwa mara, mwili wako utakuwa unapata homoni. Vidhibiti mimba hufanya kazi vyema zaidi, na usipo tumia, huenda ukapata mimba.

Mbinu ya kudhibiti uzalishaji ya lactational amenorrhea method

Mbinu hii imekisiwa kufanya kazi kwa asilimia 98 katika miezi ya kwanza sita baada ya kujifungua. Unapo timiza mambo haya. Lakini asilimia ya utendaji kazi ya mbinu hii hupungua mtoto anapo anza kuzeeka na hali ina badilika, kama vile mtoto kuanza kula vyakula vigumu ama kunywa maziwa ya mama kidogo na kulala muda zaidi wakati wa usiku.

Mambo ya kutimiza ili kutumia mbinu hii:

unaweza pata mimba unapo nyonyesha

  • Mtoto wako lazima awe mchanga kuliko miezi sita
  • Unapaswa kunyonyesha kwa angalau kila masaa manne kwa siku na kila masaa sita kila usiku
  • Unapo tumia mbinu hii, huwezi lisha mtoto formula badala ya maziwa ya mama

Kumbuka kuwa unaweza anza kuovulate tena wakati wowote bila maarifa yako. Huku kuna maana kuwa unaweza pata mimba kabla ya kupata kipindi chako cha kwanza cha hedhi baada ya kujifungua. Kivipi? Una rutuba wakati unapo ovulate na huku hutendeka kabla ya kipindi chako, wiki mbili kabla. Kwa hivyo usingoja hadi pale unapo pata kipindi chako cha hedhi kutafuta mbinu mwafaka ya kudhibiti uzalishaji.

Wanawake wachache hutegemea mbinu hii kudhibiti mimba, kwa sababu huenda ikawa hii ndiyo mbinu rahisi kwao. Baadhi ya wanawake hunyonyesha watoto wao wasaa wote hadi wanapo fikisha miezi sita.

Ikiwa ungependa kutumia mbinu ya kunyonyesha kama njia asili ya kudhibiti uzalishaji, wasiliana na daktari wako kabla ya kuzaliwa kwa mwanao.

Kudhibiti uzalishaji ni muhimu baada ya kujifungua

Na homoni, hakuna kitu kilicho dhabiti. Ikiwa hungependa mtoto mwingine hivi karibuni, wasiliana na daktari wako kuhusu mbinu za kudhibiti uzalishaji. Atakupatia maarifa tosha ili ufanye uamuzi unao faa.

Soma Pia:Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kupunguza Tumbo Baada Ya Kujifungua!

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Kuna Uwezekano Wa Kupata Mimba Unapo Nyonyesha?
Share:
  • Kupevuka Kwa Yai Huanza Lini Kwa Mwanamke?

    Kupevuka Kwa Yai Huanza Lini Kwa Mwanamke?

  • Ongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation

    Ongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation

  • Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

    Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

  • Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

    Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

  • Kupevuka Kwa Yai Huanza Lini Kwa Mwanamke?

    Kupevuka Kwa Yai Huanza Lini Kwa Mwanamke?

  • Ongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation

    Ongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation

  • Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

    Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

  • Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

    Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it