Je, Unaweza Pima Mimba Ikose Kuonekana?

Je, Unaweza Pima Mimba Ikose Kuonekana?

Vipimo vya nyumbani ni njia rahisi ya kujua iwapo una mimba ama la. Watu wengi wana chagua kufanya vipimo vya nyumbani kwani ni rahisi, havichukui muda mrefu na hauhitaji vitu vingi kufanya kipimo hiki. Kwa mara nyingi, vijiti vya vipimo hivi vina tumbukizwa kwenye mkojo ili kujua iwapo kuna homoni ya HCG kwenye mkojo ule ambayo ni homoni ya mimba. Homoni hii inayo tengenezwa mwilini siku za mwanzo za mimba. Mara nyingi, vipimo vya mimba vya nyumbani huwa kweli na matokeo yake huwa kweli ila kuna wakati na sababu ambazo huenda zikafanya kipimo hiki kuwa na matokeo hasi ama yasiyo ya kweli. Ni kweli kuwa unaweza pima mimba ikose kuonekana kwa sababu ya mambo tofauti ambayo tuna angazia.

Je, Unaweza Pima Mimba Ikose Kuonekana?

  1. Mimba ya kemikali

Kuna uwezekano wa kuwa na matokeo chanya ya kipimo cha mimba hata kama hauna mimba. Hii ndiyo inajulikana kama chanya isiyo kweli na wakati mwingine mwingine hujulikana kama mimba ya kemikali. Hii hutendeka wakati ambapo yai ama embryo hukosa kujishikilia kwenye kuta za uterasi e na huenda ikasababishwa na sababu nyingi kama vile: fibroids, scar tissue ama matatizo ya uterasi. Iwapo utafanya kipimo ukiwa na matatizo haya, huenda kipimo kikawa hasi na ukose kujua hali yako ya mimba. Kwa sababu hii, unashauriwa kufanya kipimo chako cha mimba cha nyumbani baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi.

unaweza pima mimba ikose kuonekana

2. Mimba ya ectopic

Baadhi ya wakati yai huenda likajishikilia nje ya kuta za uterasi na kusababisha hali inayo julikana kama mimba ya ectopic. Yai hukwama kweny fallopian tube inapokuwa kwenye safari ya kuelekea kwenye uterasi. Sababu zinazo sababisha mimba ya aina hii ni kama vile:

  • Kuwa na kidonda kwenye tishu za fallopian tube ama kuwa na historia ya maambukizi ya uterasi.

Ishara za kuwa na mimba ya ectopic ni kama vile:

  • Kuhisi kutapika na chuchu za kuwasha
  • Uchungu mwingi kwenye tumbo ama sehemu ya chini
  • Kizunguzungu ama kuzirahi
  • Kuhisi uchungu mara kwa mara kwa tumbo, mabega, shingo ama pelvis yako

3. Kuharibika kwa mimba ama kutoa mimba

Punde tu baada ya kuharibika kwa mimba ama kutoa mimba, kipimo cha mimba kitadhihirisha kuwa una mimba. Kwa sababu viwango vya homoni ya HCG bado ziko juu. Ila usiwe na shaka kwani vitapungua baada ya wiki tano ama sita.

unaweza pima mimba ikose kuonekana

4. Kutumia vifaa vilivyo haribika

Kuna uwezekano wa kupata matokeo yasiyo ya kweli ukitumia kifaa kilicho haribika. Kuwa makini kuangalia tarehe za kuharibika kwa kifaa kabla ya kukinunua. Pia unaweza pima mimba ikose kuonekana ukipima mimba mapema sana. Wataalum wa afya hushauri upime mimba siku baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi.

Kumbukumbu: Wedmd

Soma pia: Jinsi ya kupima mimba kwa kutumia dawa ya meno

Written by

Risper Nyakio