Wakenya kutoka pande tofauti waungana mikono kukashifu unyama wa polisi Kenya ulio shuhudiwa leo kufuata amri za rais Uhuru Kenyatta aliye tangaza kafyu siku ya Jumatano. Kafyu hii hairuhusu watu kuwa nje kati ya masaa ya saa moja jioni hadi saa kumi na moja asubuhi. Isipokuwa makundi wa watu walio patiwa kibali cha kuwa nje, ikiwemo polisi, madaktari, wana habari na wanao uza kwenye maduka ya vyakula.

Vurugu huku unyama wa polisi ukishuhudiwa mijini tofauti Kenya
Siku ya kwanza ya kuanzishwa kwa kafyu hii ilikuwa na vurugu na misuko suko mingi. Idadi kubwa ya watu walionekana waki wakimbia polisi walio kuwa kwa idadi kubwa katika miji na mitaa yote nchini.
Mombasa mji wa raha ulikuwa na taharuki nyingi leo huku wananchi wakikimbizana na polisi. Idadi kubwa ya watu ilionekana ikiyakimbilia maisha yao baada ya polisi kuwarushia vitoa machozi na kupiga risasi nyingi hewani. Wazee kwa vijana, wake kwa waume wote walikimbia kuya nusuru maisha yao. Kanda na picha za unyama wa polisi Kenya zimejaa katika mitandao tofauti ya kijamii baada ya polisi hawa kuwaamrisha wananchi kulala chini huku wakiwachapa kwa kutumia fimbo na kuwarushia mateke. Huku wakisukumwa na kuamrishwa wakae chini wakiwa wamekaribiana. Bila kuzingatia umbali unao takikana kuzuia kuenea kwa virusi vya homa ya korona, jambo ambalo halikuzingatiwa katika kisa hiki. Wengi wakikashifu tendo hili kwani ni kuhatarisha maisha ya watu na kufanya iwe rahisi zaidi kueneza virusi vya covid-19.
Mwanahabari aliye chapwa na polisi
Kilicho wakera wananchi na wanahabari zaidi ni kanda iliyo onekana polisi mmoja akim nyanyasa mwanahabari Peter Wainaina wa chumba cha habari cha NTV. Cha kusikitisha zaidi ni kuwa masaa ya kafyu hayakuwa yameanza. Ilikuwa saa kumi na moja za jioni, lisaa limoja kabla ya kafyuu kuanza. “Nilikuwa katika shughuli za kuifanya kazi yangu na unyama nilio fanyiwa na mwana polisi ulinishika kwa mshangao kwani sikufanya chochote cha kumkasirisha na haikuwa sawa,” Wainaina aliwaambia wana habari wa Daily Nation. Chama cha wanahabari nchini kili kashifu tendo hili la unyama wa polisi Kenya na kutaka hatua kali zichukuliwe kwa polisi aliye mnyanyasa mwana habari huyu. Kumbuka kuwa wana habari ni miongoni mwa watu walio na kibali cha kuwa nje wakati wa kafyu.
Hali ilivyokuwa Nairobi
Katika mji mkuu wa nchi, kulikuwa na hali ya tatanishi huku watu wengi wakipiga foleni ndefu waki ngoja magari ya kwenda katika sehemu tofauti. Kupata magari kuliwa tatiza wengi kwani ma dereva wengi walifunga kazi mapema wakiepuka kupatwa nje masaa yasiyo kubalika. Kwa walio pata magari, nauli zilikuwa zimepanda sana kuwatatiza wengi kufika nyumbani. Kuna kisa ambapo dereva aliwaacha abiria kwenye gari la kwenye sehemu maarufu ya Utawala na kisha kupotea huku akiwaacha bila kujua la kufanya.
Watu walio jeruhiwa walipelekwa hospitalini
Leo ikiwemo ni siku ya Ijumaa ambapo mji wa Nairobi unajulikana kuwa na uhai. Kwani watu wengi hukusanyika kutoka sehemu tofauti za nchi ili wajivinjari na kuirabisha wikendi, leo mambo yalikuwa tofauti. Ilipofika wakati wa saa moja za usiku, mji ulikuwa umetulia kama maji ya mtungi. Kwa sababu wana biashara wengi walikuwa wamefunga biashara zao na kuelekea manyumbani.
Katika mitaa kama Nyeri na Nakuru, watu walifuata kanuni zilizo wekwa na serikali na hakuna watu walio onekana waki randa randa katika wakati huu. Kwa madereva wa masafa marefu kama vile kutoka mji wa Nairobi kuwasafirisha watu hadi mji wa Mombasa, wali pumzika mahali ambapo walikuwa saa moja ikifika na kuahirisha safari yao hadi kesho asubuhi kutoka saa kumi na moja za asubuhi.
Maneno ya busara
Hii haikuwa siku ya kwanza iliyo tarajiwa na watu wengi. Ila tungependa kuwahimiza wananchi wa Kenya kujaribu juu chini na kuhakikisha kuwa wanazingatia amri za kafyu zilizo wekwa na serikali. Kupigana na janga la covid-19 ni mwito na juhudi za kila mmoja wetu. Tukizingatia maagizo haya, tutayarudia maisha yetu hivi karibuni. Hakikisha kuwa una jikarantini na kujitenga na watu iwapo una shuku una dalili za covid-19. Enda kwa hospitali iliyo karibu nawe na uripoti shaka zako ili vipimo vifaavyo vifanyike kuhakikisha iwapo una virusi hivi ama la.

Kutoka Africaparent, tuna wahimiza wananchi wote kuzingatia usafi kwa kunawa mikono kila mara kwa kutumia vitakasio vyenye viwango vya kileo kinacho hitaji, ama kwa kutumia sabuni na maji safi. Hakikisha unapo kohoa ama kuchemua, unatumia sehemu ya ndani ya kiwiko chako, na kuepuka kuwa miongoni mwa watu wengi na kuzingatia umbali wa mita moja unusu.
Wasiliana na wizara ya afya nchini kuhusu virusi vya covid-19 kwa kupiga nambari hizi za dharura 0800721316 (bila malipo), 0729 471 414, 0732 353 535.
Chanzo: Standard media