Faida 5 Za Unyonyeshaji Wa Kipekee Kwa Mtoto Mchanga!

Faida 5 Za Unyonyeshaji Wa Kipekee Kwa Mtoto Mchanga!

Mama anaye nyonyesha ana himizwa kuwa makini na lishe yake. Kula lishe kamili na yenye afya iliyo na virutubisho vyote.

Je, mtoto mchanga ana paswa kulishwa nini? Unyonyeshaji wa kipekee kwa watoto walio chini ya miezi sita kuna shauriwa. Unyonyeshaji wa kipekee ni pale ambapo mama anamlisha mtoto wake mchanga maziwa ya mama bila kuongeza vyakula ama viowevu vingine.

Unyonyeshaji wa kipekee ni muhimu sana kwa mama na mtoto mchanga. Kitendo kinacho anza kati ya lisaa limoja baada ya mama kujifungua. Anapo anza kufanya hivi, anapunguza nafasi ya kutunga mimba tena hata baada ya kufanya mapenzi bila kinga. Unapo jihusisha katika tendo la ndoa na hauzingatii unyonyeshaji wa kipekee, kuna nafasi nyingi za kutunga mimba tena. Ikiwa mwanamke hanyonyeshi mtoto wake, ni vyema kuwa na mbinu ya kudhibiti uzalishaji ili kuepuka kutunga mimba muda baada ya wiki nne.

Unyonyeshaji wa kipekee una manufaa gani kwa mtoto

kuumwa na chuchu

 • Mtoto mchanga aliye na miezi chini ya sita anastahili kunyonyeshwa maziwa ya mama peke yake bila chakula kingine. Na mara kati ya 8 hadi 12 kwa siku.
 • Mama anastahili kumlisha mtoto baada ya kila masaa matatu. Lishe ya mchana haipaswi kupitisha masaa manne mchana ama masaa sita usiku.
 • Vipindi vya hedhi vinapo rejea angali ana nyonyesha mtoto chini ya miezi sita, ana nafasi za kutunga mimba.

Mama anapo mwanzishia mtoto chakula kigumu, kamwe hayuko salama tena na anaweza tunga mimba. Ni vyema kuwa na mbinu ya kupanga uzazi.

Manufaa ya maziwa ya mama

unyonyeshaji wa kipekee

Faida kwa mtoto mchanga

 • Mtoto anapata lishe kamilifu
 • Ni rahisi kufyonza kwa urahisi
 • Ana lindwa dhidi ya maambukizi
 • Ulinzi dhidi ya mzio
 • Kuongeza utamano kati ya mama na mtoto

Faida kwa mama anaye nyonyesha

 • Kuboresha utangamano wa mama na mwanawe
 • Anaweza kupunguza uzito wa mwili
 • Kunamsaidia kudhibiti uzalishaji kabla ya miezi sita

Mama anaye nyonyesha ana himizwa kuwa makini na lishe yake. Kula lishe kamili na yenye afya iliyo na virutubisho vyote. Mama anatosheleka kihisia anapo mnyonyesha mtoto wake na kumshibisha. Kila mama anapo mpakata mtoto wake na kumnyonyesha, uhusiano wao unakua zaidi.

Soma PiaKutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

Written by

Risper Nyakio