Mambo 21 Usiyo Paswa Kufanya Baada Ya Upasuaji Wa C-Section

Mambo 21 Usiyo Paswa Kufanya Baada Ya Upasuaji Wa C-Section

Usiwai fikiria kuwa upasuaji wa C-section unakufanya kuwa mama asiye timia.

Umefanyiwa upasuaji wa C-section hivi majuzi. Upasuaji huu unafanyika kwa mama wote kati yetu. Mambo yasipofuata kitabu, hatimaye utahisi uchungu mwingi sana, maisha yako hatarini, na upasuaji wa C-section.

Huenda likawa jambo gumu kwa baadhi ya wanawake, ila hatuwezi badilisha mambo na kuyafanya tofauti ili tuendelee kutoka hapo... na tafuta kitu cha kukuchekesha ndani yake. Kwa sababu kucheka kutakusaidia -- hata kama kuta kuuma sana ukicheka kwa nguvu.

what not to do after c-section

Chukua mto, hasa wewe mama wa upasuaji wa C-section katika hatua hii yako ya uponyaji, na uishikilie kwa upole kwenye tumbo lako kwa sababu huenda kukawa na kicheko hapa na pale kwenye orodha ya vitu ninavyo fikiria haupaswi kufanya baada ya upasuaji wa C-section.

Mambo ya kutofanya baada ya upasuaji wa C-section

 • Usitupe masaa 32,446 ukijihurumia kwa sababu haukujifungua kwa njia asili ama kupitia kwa uke wako.
 • Usiwe na fikira dhidi ya upasuaji wa c-section haijalishi kikundi ambacho utajipata ndani yake. Hakuna wengi wao- ila wana kelele tu. Hata Ina May Gaskin ambaye ana shauri ukunga na kujifungua kwa njia ya asili pia anafikiria kuwa upasuaji wa C-section hauhitajiki. Ila baadhi ya wakati, unahitajika.
 • Usifikirie kuwa kujiendesha nyumbani ukitoka hospitalini kutakuwa jambo rahisi. Ndio, unaenda nyumbani na hilo ni jambo nzuri ila kila uvimbe gari linapitia litakuwacha ukihisi uchungu mwingi. Mwambie yeyote anakupeleka nyumbani aendeshe gari pole pole na ujiegemeze kwa kutumia mto.

what not to do after c-section

 • Usidhubutu kuwa mgonjwa kwa sababu ukichemua unapo pona kutokana na upasuaji wa C-section uchungu huo kwenye sehemu ilifanywa upasuaji itauma sana. Lazima utumie mto kupunguza uchungu huo.
 • Usikohoe pia kwani kunachangia kuhisi uchungu.
 • Usikule kitu chochote ambacho kitakupatia hewa.
 • Usikule kitu chochote ambacho kitakufanya ukose maji mwilini.
 • Usiringe kuhusu shepu isiyo na doa ya kichwa cha mtoto wako kwa sababu hakuwa mtoto bikira.
 • Hata usiseme "mtoto bikira" kwa nguvu. 
 • Usipoteze uwezo wako wa kuwa mcheshi.. hata siku moja..
 • Usicheke iwapo hauna mto mkononi.
 • Usisahau kuwa na mito mingi karibu nawe wakati wote. Unaihitaji kulinda alama yako ya upasuaji kutokana na kukohoa, kucheka, kuchemua, ila pia jiinue vyema na ustareheke ili usiumwe na kitu chochote unapo pona.
 • Usilie kwenye bafu ukishangaa ni lini utajihisi vyema tena. Ni sawa, unaweza lia, ila sio kwa nguvu sana kwani alama yako ya upasuaji itauma na utaumwa.
 • Usimkasirikie mtaalum wako wa afya ya uke kwa kuto fanya kiinimacho kufanya tumbo yako iwe sawa kama hapo awali anapo kazana kumtoa mtoto. Nafikiria tumbo hiyo ni nzuri ili usione alama ya upasuaji.
 • Usiichokoze alama yako ya upasuaji. Hata usiiangalie. Mwache bwanako aiangalie kuhakikisha iko sawa.

what not to do after c-section

 • Usi tarajie kufa ganzi kuishi wakati huo huo. Imekuwa miaka 3 na bado nahisi kufa ganzi.
 • Usifikirie kuwa madaktari walisahau kurudisha abs zako pale zilizo kuwa. Ziko hapo.... ila zitachukua wakati mwingi sana kuhisi kana kwamba unaweza zitumia tena.
 • Usijichoshe na kazi ya kinyumbani. Wacha jamaa na marafiki wako wakusaidie kufanya kazi ya kinyumbani kama vile kuosha vyombo na kupika ili utumie nguvu zako kupona na usikimbize vitu kwani huku huenda kuka simamisha safari yako ya uponaji.
 • Usipande ngazi. Iwapo una sakafu mbili, tulie kwenye moja kati ya hizo mbili.
 • Usisahau kuwa madawa ya kupunguza uchungu na marafiki wako. Bila shaka usizinywe kwa kiwango kikubwa, ila cha kutosha tu, siku yote iwapo kuna umuhimu ili usiwe na uchungu na unaweza furahia mtoto wako anayependeza... ama watoto wa mama wengi.
 • Usiwai fikiria hata kwa sekunde moja kuwa upasuaji wako wa C-section unakufanya kuwa mama mdogo ama kuwa hauku jifungua mtoto wako. Mtoto alitoka tu kwa mfuko kwenye tumbo lako, huku amefunguliwa kama zawadi.

Kwa umoja, wamama wangu wa upasuaji wa C-section. Mpone kwa kasi!

Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza na CafeMom na yakachapishwa na ruhusa ya theAsianparent kisha yaka na Risper Nyakio.

Soma pia: A Personal Experience On Giving Birth During The Coronavirus Pandemic

Written by

Risper Nyakio