Upele Kwa Uso Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kutatua

Upele Kwa Uso Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kutatua

Wanawake wengi huzungumza jinsi kujifungua kulivyo na masomo mengi, yote ambayo ni ukweli. Lakini kuna mambo mengi hasi ambayo huja na safari hii ya mimba na kujifungua. Mwili wako utashuhudia mabadiliko na kuhisi kana kwamba kuna kitu ambacho sio sawa. Baadhi ya sehemu za ngozi yako huenda zika nyooka na kutoa alama. Huenda ukapoteza nywele zaidi kuliko mtu wa kawaida. Ngozi kupoteza rangi na mabadiliko kwenye chuchu. Upele baada ya kujifungua ni mojawapo ya mabadiliko yanayo andamana na mwisho wa safari yako ya mimba. Makala haya yana kuelimisha jinsi ya kutatua tatizo la acne baada ya kujifungua.

Kwa baadhi ya wanawake, upele usoni huonekana katika ujauzito. Wakati ambapo kwa wengine, hufanyika baada ya kujifungua. Upele unao baki, huenda ukaisha siku chache baada ya kujifungua ama ukiwa na mimba. Kulingana na mwili na homoni zako.

Upele baada ya kujifungua: Ni nini hasa? Ni kawaida?

upele baada ya kujifungua

Upele ni tatizo la ngozi ambalo watu hushuhudia wanapo vuja ujana, umri ambao viungo vya ngono vime komaa na wana uwezo wa kupata watoto. Acne baada ya kujifungua mara nyingi huonekana kwa uso lakini inaweza sambaa kwa sehemu zingine za mwili.

Hali hii ni kawaida na hakuna haja ya kuwa na shaka. Kwa baadhi ya wamama, huishi bila matibabu yoyote. Wakati ambapo kwa wengine huhitaji vitu zaidi ili kuisha. Kwa hivyo kwa sababu upele wa ndugu yako wa kike ama rafiki yako uliisha bila kufanyiwa chochote, hakumaanishi kuwa yako itafanya hivyo.

Sababu za upele baada ya kujifungua

Hapa chini kuna sababu chache kwa nini acne hutokea baada ya kujifungua.

  • Kiwango cha homoni

Ujauzito ni kipindi katika maisha ya mwanamke ambapo mabadiliko ya homoni huwa mengi. Na hii ndiyo sababu kuu kwa nini wanawake wengi hushuhudia upele kwenye uso baada ya kujifungua. Pia, kunyonyesha huenda kukasababisha utoaji wa homoni ambazo zinaweza anzisha upele kwenye uso. Kwa baadhi ya wanawake, viwango vya homoni hushuka baada ya kujifungua, kwa wengine huenda ikachukua wiki chache.

  • Kukosa maji tosha mwilini

Kiwango cha maji mwilini kinapaswa kuwa juu baada ya kujifungua. Kukosa maji tosha mwilini husababisha ngozi ya nje kuvunjika na kusababisha upele. Kunyonyesha ni njia ya kupoteza maji kutoka mwilini wa mama. Kwa hivyo atahitaji kunywa viowevu vingi kusawazisha vitu vyote.

  • Fikira nyingi

Kujifungua mtoto huja na mawazo mengi kwani ni mambo mengi yanayo hitajika kufanywa. Hasa kwa wazazi wa mara ya kwanza. Unatatizika kujua jinsi ya kufanya vitu fulani na hili huenda lika athiri kiwango cha usingizi unacho kipata kwa siku. Na kusababisha upele kwa uso.

Jinsi ya kutibu upele baada ya kujifungua

kukoma kupanga uzazi

Matibabu ya acne huwa aina mbili. Matibabu unapo nyonyesha na usipo.

  • Matibabu unapo nyonyesha

Wakati wa mimba, una shauriwa kuwa mwangalifu wa matibabu unayo chukua. Na ni vivyo hivyo unapo nyonyesha. Baadhi ya matibabu huenda yaka badili mzunguko wa maziwa ya mama. Kwa hivyo, kwa kutibu acne unapokuwa ukinyonyesha, unaweza jaribu bidhaa zilizo na salicylic acid, benzoyl peroxide ama glycolic acid. Walakini, upele ukizidi, chukua antibiotics za topical, azelaic acid na benzoyl peroxide.

  • Matibabu usipo nyonyesha

Usipo kuwa una nyonyesha, una uhuru zaidi wa kuzuru matibabu zaidi. Tembe ni njia bora kwa sababu itasaidia kutoka chanzo cha upele huo. Zina sawazisha homoni hizi. Pia, unaweza endea matibabu yaliyo orodheshwa hapo juu. Huenda daktari wako aka kushauri kuchukua tembe za acne.

Matibabu Mengine

Matibabu mengine ni kama vile bidhaa za utunzaji wa ngozi, kuhakikisha kuwa ngozi yako ina unyevu nyevu tosha na kupunguza kukwazwa kimawazo kuepuka mlipuko zaidi wa upele usoni. Kula lishe yenye afya na kupunguza muda unao kaa kwa jua kwa sababu ngozi huwa nyeti baada ya kujifungua.

Hata kama mlipuko wa acne baada ya kujifungua huwa ni kawaida, ikiwa ni chungu ama ziko kwa sehemu za mwili zisizo za kawaida, hakikisha kuwa umemwona daktari wako.

Soma pia:Vyakula Ambavyo Unapaswa Kuepuka Katika Mwezi Wako Wa Kwanza Wa Ujauzito

Written by

Risper Nyakio