Ni kawaida kwa watu wanao fikisha umri wao wa kuwa watu wazima kujipata wakiwa na chunusi ama upele kwenye uso. Hata hivyo, hakuna anaye furahia kuwa na upele kwenye uso, sote tuna taka kuwa na uso ulio mwororo usio na doa. Usitie shaka unapo gundua kuwa uso wako una upele.
Upele ni nini?

Upele ni hali hasi ya ngozi, ambapo mtu hupata vidonda vidogo, huenda vikawa vya rangi nyekundu ama nyeupe zilizo na usaha. Baada ya kujikuna uso, upele huibuka, hata baada ya kujikuna, madoa hubaki kwenye uso.
Kuna sababu nyingi zinazo fanya mtu kuwa na upele
Sababu za kuwa na upele:
- Kukwazwa kimawazo
- Vichocheo kubadilika mwilini
- Kutumia mafuta fulani usoni
- Kuwa na kipindi cha hedhi
Nitafanya nini kuhusu upele wangu?
- Kusafisha uso wako mara mbili kwa siku kutumia maji na sabuni isiyo kuwa na harufu kali
- Usisugue uso wako sana, huenda ukauumiza uso wako
- Nawa uso baada ya kufanya mazoezi
- Hakikisha wakati wote kuwa una nawa uso kabla ya kulala
Kutibu upele kwenye uso

Kuna krimu nyingi ambazo zinatumika kusaidia uso uvutie zaidi na kutatua matatizo yake.
Lakini, jambo la kwanza unalo paswa kufanya ni kuwasiliana na daktari, hasa mtaalum wa ngozi. Vipimo ni muhimu sana ili kufahamu chanzo cha tatizo lako la uso. Kufanya vipimo kutamsaidia pia kufahamu iwapo una mzio wowote wa ngozi. Pia anapo kupatia madawa atajua dawa zilizo hatari kwako.
Kumbuka kufanya mambo haya:
- Usiguse uso wako kutumia mikono michafu
- Usitumie mafuta ya nywele kwa uso
- Shika nywele zako nyuma, zisiguse uso wako
- Usibonyeze upele kwa kutumia vidole vyako
- Tumia sunscreen kwa uso wako
Kumbuka kuwa ni kawaida kabisa kupata upele kadri unavyo zidi kuzeeka. Usiwe na shaka sana, ila jaribu kupata msaada kutatua hali yako. Sawa na sehemu nyingine ya mwili, uso unapaswa kutunzwa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Matatizo Ya Kiafya Mwanamke Anayo Kumbana Nayo Katika Mimba