Urithi wa Kobe Bryant: Kichocheo kwa kina baba kila mahali

Urithi wa Kobe Bryant: Kichocheo kwa kina baba kila mahali

The late basketball star Kobe Bryant was a father to 4 beautiful girls, but he wasn't just any father.

Katika ulimwengu unaosherehekea siku za kina mama tatu na siku moja tu kwa kina baba, tunafaa kufanya zaidi kusherehekea   ubaba.  Na kama matukio ya hivi karibuni yamewaza kutufahamisha juu ya maisha na nyakati za mchezaji mkuu wa mpira wa vikapu Kobe Bryant; sio siri kuwa malezi bora ya baba yalikuwa kati ya urithi wa Kobe Bryant. Kobe alikuwa baba wa kuigwa, kikomo.  Na tutaweleza kwa nini tunafahamu hivi.

Urithi wa Kobe Bryant: Hadithi ya ubaba wa kung’aa

vanessa baby

Nyota wa mpira wa vikapu aliyeaga dunia kupitia kwa ajali ya ndege, alitumia ndege kama njia ya kusafiri Los Angeles. Sababu yake? Alipenda kushiriki wakati mwingi na familia yake na wakati mchache kwenye trafiki. Alipata aje wazo la kusafiri kwa ndege?

Nilikuwa nimekaa kwenye trafiki na nikamalizia Kukosa mchezo shuleni mwetu,” akimwambia Alex Rodriguez katika mwaka wa 2018. Ilibidi nifikirie njia ambayo ningefanya mazoezi na kutilia makini mchezo wangu na pia nisikose wakati na familia yangu.”

Kwa hivyo, akaangazia ndege na kuzichagua kama njia yake mwafaka ya kusafiri. Byrant mara hii akizungumza na Maria Shriver wa Jarida la Sunday Paper, alisema kuwa kuwa baba ndio anwani kubwa zaidi maishani mwake.

“Kuwa baba ndilo jambo najivunia sana duniani, ndio anwani yangu kuu,” akasema. “Nimejifunza mengi sana; lakini labda funzo kuu ni mapenzi ya nguvu na ya dhati unayokuwa nayo kwa watoto wako kama mzazi. Nimebarikiwa kupata hio nafasi mara nne sasa na hakuna jambo la kutia nguvu kama hilo duniani.”

Kobe Bryant na bibi yake Vanessa walijaliwa wasichana wanne warembo na hangekuwa na furaha zaidi ya hiyo. Katika hii sehemu ya dunia, kuna mkazo sana juu ya kujaliwa mtoto wa kiume. Ndoa nyingi husabaratika na kina mama wengi huumia kwa sababu ya kutojaliwa mtoto wa kiume. Lakini Kobe alijivunia kujaliwa watoto wanne wa kike. Hata kama Vanessa alitamani mtoto wa kiume Kobe alitosheka na wasichana wake.

Machi 2019 kwenye mazungumzo na Extra alisema, “ nafikiri anataka mtoto wa kiume zaidi yangu. Napenda kuwa na wasichana – nina furaha mpwito juu ya hilo. Ata yeye ana furaha juu ya hiyo,” akasema. “Alitaka mtoto wa kiume ili awe kijana wa mama daima – jambo kama hilo. Tutaona kama nitatimiza hilo, sijui.”

Baadhi ya sababu chache kwa nini Bryant alikuwa baba wa kipekee

Alimpenda mama wa watoto wake
kobe bryant legacy

Malezi bora ni juhudi ya ushirikiano. Na kuwa na uhusiano unaokua na mlezi mwenzi ni hatua ya kwanza kupata malezi ya kufana. Badala ya kuichukulia juujuu kuwa kuna mzazi mwingine kwenye picha, ni vizuri kufanya uamuzi wa kumshukuru mzazi mwenzi juu ya juhudi zake.

Kobe alikuwa bila shaka mwenye kicho na malezi ya Vanessa kama mama. “Tunakupenda na kukushukuru kwa  yale yote unayofanyia familia yetu,” mkimbiaji alimwandikia bibi yake siku ya dunia ya kina mama 2019. “Wewe ndio msingi  wa kila kitu ambacho ni cha dhamana kwetu.” Hili ni jambo moja ambalo lafaa kuigwa kwenye familia huku Afrika.

Aliwafunza watoto wake maadili mema
gianna mambacita
Kabla watoto wako kuanza shule na ata baada, nyinyi ndio wazazi wa kwanza na tunaweza kusema wa maana mno.  Ni wajibu wako kuwafunza watoto wako maadili yanayowatofautisha kama watu walioheshimika kwenye Jamii.  Pia ni wajibu wako kuwafunza mafunzo na maarifa yatakayo  wasaidia kuwa huru na kuendelea bila kuegemea popote.

Kobe alielewa hivi na ndio maana imenakiriwa kuwa alikuwa kocha wa wasichana wake. Sio tu kwenye mchezo wa mpira wa vikapu mbali pia maarifa mengine katika maisha kama vile kufanya jitihada kwa kila kitu wanachofanya. “Funzo la muhimu ninaloweza kuwafunza ni kufuata usharifu  na kiwango cha uazimaji kinachotakikana,” Byrant akasema kwa kuwa kocha wa wasichana wake.

Alikuwa baba aliyerithisha na kuiweka familia yake kwanza

kobe bryant legacy

Kuamkia habari za kifo chake, jamaa wa karibu wa familia yake alizungumza na jarida la People’s alikuwa na haya ya kusema: “Jambo kuu ninalotazamia baada ya kustaafu kutoka kwa NBA (2016) ni kushiriki wakati mwingi na familia yangu,” rafiki yake akasema. “Alikuwa baba aliyerithisha na kama kina baba wengi alikuwa na maono mazuri juu ya wasichana wake.”

Mchezaji mpira wa vikapu Kobe Bryant alikuwa baba mfano ulioko hapa juu lakini alikuwa zaidi. Ata marafiki na wachezaji wenza walisema haya kwa rambirambi zao jinsi alivyokuwa baba wa kuigwa.

Kumkumbuka kwa malezi yake ya kufana ndio njia bora ya kuheshimu urithi wa Kobe Byrant.

Vizuri ata zaidi, ni kuomba kielelezo kutoka kwa juhudi zake katika familia itaendeleza kudumisha urithi wake na kuhakikisha Kobe Bryant anaendelea kuishi milele.

 

People Magazine

Also read: An Open Letter To Vanessa Bryant: Living In A World Without Kobe And Gianna

Written by

Risper Nyakio