Kujaliwa mtoto huwa jambo la furaha sio kwa mama pekee mbali kwa familia na ukoo wote. Hii ni kwa kuwa umuhimu wa mtoto hupita nje ya mipaka ya familia. Hivyo pia jukumu la kulea mtoto huwa sio tu kwa mama pekee, wala familia mbali pia ukoo kwa ujumla. Leo tutaangazia usaidizi wa mume katika kunyonyesha.
Usaidizi Wa Mume Katika Kunyonyesha Ni Upi?

Kunyonyesha ni jambo la umuhimu sana. Hii ni kwa kuwa ata kampuni zimegundua hili na nyingi zimeanza kutengeneza mahali ambapo wanawake wanaweza kwenda kuwanyonyesha wadogo wao. Nafasi ya baba wakati mtoto anapozaliwa huwa pana na ya umuhimu.
Hii ni pamoja na kusaidia katika kushika mtoto ili mama apate kupumzika, kushika mtoto ili kujenga uhusiano na mtoto, kusaidia katika kumpa mtoto chakula, kumpeleka mtoto kwenye chanjo ama wakati anapohitaji kwenda hospitali. Mume huwa mkono wa pili wa mama katika kulea mtoto.
Hivyo umuhimu wa mume katika kunyonyesha huwa upi?
Ni wazi kuwa mama anapokuwa katika mazingira salama na yenye mapenzi huweza kutoa maziwa kwa wingi. Hii ni ikilinganishwa na aliyetaambani ama ana mkazo wa mawazo. Hili hupinga kutoka kwa maziwa. Kwa hivyo mume anafaa kuhakikisha kuwa ana tengeneza mandhari ya furaha, salama na yenye mapenzi kwa mama kuchochea kutoa kwa maziwa.
Pia mama huhitaji chakula bora ili kuweza kutoa maziwa kwa wingi. Na kwa kuwa wakati mwingi mama hana nguvu ama uwezo wa kufanya hili mume kuingilia kati husaidia pakubwa. Kuhakikisha kuwa mama ana chakula cha kutosha na vinywaji inasaidia mama kuwa na maziwa ya kutosha. Kwa hivyo mume ana jukumu kubwa sana sio kwa mama tu mbali pia kwa mtoto.
Mama anapopata mapumziko ya kutosha huchochea katika kutoa maziwa. Mama anapojifungua huhitaji wakati mwingi sio tu kupata mapumziko mbali pia ili apone kwa haraka. Kina mama wengi kwa sababu tofauti huwa hawapati nafasi nzuri ya kupona. Hili huchangia sana katika hali ya afya ya mama. Afya njema husaidia katika mama kutoa maziwa kwa wingi. Hivyo mume atakuwa wa muhimu sana kuhakikisha kuwa mama anapata mapumziko ya kutosha .
Wazazi wengi hawaelewi vizuri jinsi ya kunyonyesha na pia chakula kinachochea maziwa. Hivyo mume kuandamana na mke kwenye haya mafunzo itamsaidia kuelewa na hivyo kumsaidia mama. Hili litasaidia kujenga kumbukumbu juu ya waliosoma jinsi ya kushika mtoto anaponyonya ,usafi na chakula cha muhimu. Hivyo kusaidia katika unyonyeshaji.
Umuhimu wa kunyonyesha mtoto:

- Maziwa ya mama ina virutubisho sahihi katika ukuaji wa mtoto hadi kufikia miezi sita
- Hufyonzwa na kumeng’eywa kwa urahisi
- Maziwa ya titi ni safi na ina joto hivyo kuepukana na hatari za maziwa ya kutengenezwa
- Huwa na elementi na kingamwili zinazosaidia kupingana na maambukizi
- Pia zinahimiza ukuaji wa bakteria zenye faida kwenye utumbo wa mtoto
- Husaidia katika kuzuia kuhara chanzo kuu cha maafa ya watoto wadogo
- Huzuia kupunguza aleji kwenye mtoto mchanga
Ni wazi kuwa chakula cha mtoto cha pekee kwa miezi sita ya kwanza huwa maziwa ya mama. Hivyo usaidizi wa mume katika kunyonyesha ni hatua kubwa katika kulea mtoto.
Soma Pia: Njia 4 Za Kumfanya Mume Wako Kuwa Mwaminifu Kwa Ndoa Yenu