Ili kuanza uhusiano, wachumba wanapaswa kuwa na angalau jambo moja lililo sawa kati yao, usawa katika uhusiano ni muhimu.. Aidha mambo wanayo taka kutimiza, vitu wanavyo penda kufanya ama malengo yao ya kimaisha.
Hauhitaji usawa ili kumpenda mtu

Katika uhusiano, kuwa na usawa ni muhimu. Lakini usawa huu haufanyi uamuzi mtu utakaye mpenda. Hata kama hili ni jambo na wazo lisilo maarufu, ni ukweli kabisa. Na sababu ni kuwa, hakuna anaye fanya uamuzi wa mtu atakaye mpenda. Mapenzi ni jambo linalo fanyika kiasili, bila kupangwa ama kuwa na kusudi.
Kuvutiana kwa watu wengi mara nyingi huwa jambo usilo weza kueleza. Unajipata tu umempenda mtu kufuatia sababu usizo weza kueleza, na hilo ni sawa. Uko sawa na usiwe na shaka. Kila mtu hupitia hatua hiyo maishani mwake angalau mara moja.
Kumpenda mtu na kumpa mapenzi ya thati, hauna nguvu za kupingana na hisia hizo zenye nguvu kukushinda.
Unapaswa kuwa katika uhusiano na mtu usiye na usawa naye

Hata kama kuna watu wanao zidi na kuwapenda watu hata kama hawana usawa, ni jambo ambalo huenda likawaumiza baadaye. Katika uhusiano na mapenzi, ni muhimu kwa wachumba kuwa na mambo sawa wanayo penda. Hata kama haufanyi uamuzi wa utakaye mpenda, kuzidi na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu usiye mpenda, bila shaka kutaleta matokeo hasi. Hakuna njia ingine ama tukio chanya kutoka kwa kitendo hiki.
Kuingia katika uhusiano na mtu mliye na tofauti na hamna usawa kabisa wa kimaisha ama nyanja yoyote ile kutakuwa na hatima mbaya.
Huwezi kuwa na mpenzi ambaye maono yake ya maisha ni tofauti sana na yako. Ili kuwa na uhusiano wenye mafanikio, mnapaswa kuwa na usawa ili muweze kujiendeleza maishani pia. Kufanya hivi kutawasaidia kusuluhisha matatizo yenu yanapo ibuka.
Je, unakubaliana nasi kuwa lazima wachumba wawe na usawa katika uhusiano ili mapenzi na uhusiano wao kufuzu?
Soma Pia: Njia 3 Ambavyo Uhusiano Unaathiriwa Baada Ya Mchumba Kutoka Nje