Ushauri Bora Kuhusu Ndoa Kwa Wanao Lenga Kuoana

Ushauri Bora Kuhusu Ndoa Kwa Wanao Lenga Kuoana

Wanandoa wana shauriana kubaki pamoja kwa mazuri na mabaya wanapo apa katika harusi, kwa sababu nzuri. Kuna wasaidia kufahamu kuwa wana hitajiana.

Hakuna ndoa iliyo sawa na nyingine. Sawa na uhusiano, kila uhusiano una pande hasi na chanya. Hata mchumba mmoja anapo toka kwa uhusiano na kuingia kwa uhusiano mwingine, mambo yana badilika kwani anakutana na mtu mwingine tofauti. Makala yetu ya ushauri kuhusu ndoa kwa wanandoa utakuelimisha jinsi ya kujitenga na utengamano katika uhusiano wenu.

Vidokezo 5 vya ushauri bora kuhusu ndoa

ushauri kuhusu ndoa

  1. Kuwa na akili wazi, kwani uhusiano unao didimia hauja andikwa kwenye jiwe

Huenda kama wanandoa ama wachumba mkahisi kuwa mapenzi kati ya wawili wenu yana didimia. Msijichukie wala kuchukiana. Jaribuni kadri mnavyo weza kuona iwapo mnaweza rejesha mapenzi kwenye uhusiano wenu. Kupitia kwa mazungumzo ama kwenda darasa za ushauri kwa wataalum wa mambo ya ndoa na uhusiano. Msikate tamaa kabla ya kufanya yote m-wezayo.

2. Mpende mchumba wako na moyo wako wote

Kuna usemi wa kimombo, unapo mpenda mtu, unawaachilia wawe huru. Wenye maana kuwa mapenzi sio jela ama kuwa mali yako, la hasha. Unapo mpenda mtu, mpende kwa moyo wako wote, ila mwache awe na uhuru wa kufanya anacho taka. Kwa njia hii utaweza kumwelewa pia na kujua lugha yake ya mapenzi. Na pia, usitazame uhusiano wa mtu mwingine, kwani kila uhusiano ni tofauti.

3. Tarajia changamoto kwenye uhusiano wenu

Wanandoa wana shauriana kubaki pamoja kwa mazuri na mabaya wanapo apa katika harusi, kwa sababu nzuri. Kuwa pamoja katika misuko suko ya aina zote kutawasaidia wanandoa kuwa una umoja zaidi kuliko ilivyo kuwa mwanzoni. Pia, watagundua kuwa wana furaha zaidi wakiwa pamoja kuliko wakiwa mbali.

4. Mwegemeze mchumba wako na uheshimu chaguo lake

kumfanya mchumba akufikirie

Kuwa kwa ndoa ama uhusiano na mtu kuna maana kuwa mna umoja na nyinyi ni marafiki mbali na kuwa wachumba. Mojawapo ya majukumu yako makuu ni kuhakikisha kuwa kamwe hahisi kana kwamba ako peke yake. Anapo fanya uamuzi mkuu maishani mwake, kuwa sako kwa bako naye. Anapo tatizika, msaidie uwezavyo.

5. Fahamu nguvu na uwezo wenu

Ni muhimu sana kwa wanandoa kufahamu nyanja ambazo wanafuzu na zile ambazo hawafuzu. Kwa kufanya hivi, mtaweza kugundua mambo mnayo faa kutilia mkazo ili kujikuza. Pia, usichukulie kimzaha na kumcheka mchumba wako anapo feli katika jambo fulani. Badala yake, hakikisha kuwa unamfunza.

Soma PiaJinsi Umri Unavyo Athiri Uhusiano Wako Wa Kimapenzi

Written by

Risper Nyakio