Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Ishara 5 Kuwa Ndoa Yenu Inahitaji ushauri Wa Kitaalum

3 min read
Ishara 5 Kuwa Ndoa Yenu Inahitaji ushauri Wa KitaalumIshara 5 Kuwa Ndoa Yenu Inahitaji ushauri Wa Kitaalum

Ni muhimu kwa wanandoa kupata ushauri wa kitaalum wa ndoa ili kuwasaidia kutatua matatizo katika ndoa yao kuepuka talaka.

Ndoa huwa na panda shuke zake. Ila, matatizo haya yanaweza kuzidi na wanandoa kuhisi kwamba mapenzi yameisha na kila mtu angependa kwenda njia tofauti. Kabla ya kufanya uamuzi huu, ni muhimu kwa wanandoa kupata ushauri wa kitaalum wa ndoa. Tazama ishara zaidi kuwa wanandoa wanahitaji ushauri kutoka kwa mtaalum.

Ishara unahitaji ushauri wa kitaalum wa ndoa

ushauri wa kitaalum wa ndoa

  1. Vita ndiyo njia ya kipekee ya kuwaunganisha kihisia

Wanandoa waliona uwoga wa kuonyesha kasoro zao kihisia kwa wachumba wao mara nyingi hupigana kwani inawapatia uungano wa kihisia bila kuonekana wanyonge. Ikiwa huu tu ndiyo wakati unapohisi mna uungano na mchumba wako ni mnapokuwa na vita na vurugu, ni muhimu kwenu kutafuta mshauri wa ndoa na mjifunze upya jinsi ya kuwasiliana na mchumba wako.

2. Matatizo ya kujithamini kuzidi katika ndoa

Ikiwa unahisi kuwa matatizo yako ya kujithamini yamezidi tangu ulipofunga ndoa, huenda mchumba wako akawa anakunyanyasa kihisia. Wachumba wanaokunyanyasa kihisia mara kwa mara hukutusi ama kukupuuza hata mbele ya familia na marafiki. Huenda wakaanza vita vya maksudi nawe ama kusema mambo yanayo kuumiza kisha kukulaumu kwa kujali sana unapokasirika.

Jambo hili litaathiri nyanja tofauti za maisha yako, ikiwemo kazi, uhusiano wako na watoto wenu na marafiki, kwa hivyo, pata usaidizi wa wakitaalum.

3. Matatizo ya kifizikia ama kiakili

ushauri wa kitaalum wa ndoa

Wakati ambapo mchumba mmoja amefahamika kuwa na matatizo ya kifizikia ama ugonjwa kama saratani, ndoa huathirika pakubwa. Mchumba aliyeathirika huenda akajitenga na watu, kuwa na mhemko wa hisia ama kusombwa na mawazo na kufanya mawasiliano yawe magumu. Ushauri wa ndoa ni njia bora kwa wanandoa kuzungumza kuhusu uwoga wao na aina ya kuegemezwa wanako hitaji.

4. Matatizo kumpa mwingine kipau mbele

Ikiwa kazi yako, watoto, marafiki ama mambo mengine yanakuja kabla ya mchumba wako, huenda ukawa una matatizo kumpa mchumba wako kipau mbele. Wakati ambapo wanandoa hawawezi kutarajiwa kuwa pamoja wakati wote, ni muhimu kwao kuwa na wakati wa kipekee kuboresha uhusiano wao na kufanya mambo wanayo yapenda. Ikiwa hukumbuki wakati wa mwisho mlifanya kitu cha kufurahisha na mchumba wako, ni vyema kuwasiliana na mtaalum wa ushauri wa ndoa.

5. Kutosikizana na mchumba wako

Kila wanandoa hupitia kipindi wanapojuta kuwa katika ndoa, ila, kipindi hiki hupita. Walakini, ikiwa umekuwa ukihisi kwa muda mrefu ama unahisi kuwa mapenzi yenu yameisha na ungependa talaka, ni muhimu kufanyiwa ushauri wa kitaalum wa ndoa. Ili wewe na mchumba wako mpate chanya cha kuzungumzia chanzo cha kufifia kwa hisia zenu.

Soma Pia: Njia 3 Ambazo Wanandoa Wanaweza Kutumia Ili Kuwa Na Vita Vya Haki Katika Ndoa

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Relationship & Sex
  • /
  • Ishara 5 Kuwa Ndoa Yenu Inahitaji ushauri Wa Kitaalum
Share:
  • Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

    Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

  • Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

    Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

  • Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

    Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

  • Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

    Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

  • Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

    Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

  • Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

    Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it