Aina tano(5) za ushirikina ulio wa kawaida sana nchini Kenya

Aina tano(5) za ushirikina ulio wa kawaida sana nchini Kenya

Kuna imani kuwa kila jambo linalo tendeka lina sababu. Hizi ni imani zilizo pitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kama vile mtu anapo tegwa akitembea, kuna imani kuwa kuna watu wanao mtaja.

Je, una amini katika ushirikina? Ni aina gani za ushirikina unazo amini ama ambazo umeziskia? Ushirikina Kenya ni jambo la kawaida. Ni bayana kuwa kwa njia moja sote tuna amini katika ushirikina. Tuna amini katika ushirikina na ku ushirikisha na matukio fulani katika maisha yetu. Hata kama muda una badilika na kuna dini zisizo amini katika ushirikina, na zinahubiri watu waache kuamini njia hizi, bado tunajipata tukiamini mambo yaliyo pitishwa kwetu na wazee wetu katika jamii. Ushirikina ni imani ambayo haina sababu za kimsingi ya maarifa. Kwa mara nyingi, unatumika kutabiri matukio yatakayo tendeka. Matukio yanayo tendeka leo ama saa hii yanatumika kubashiri kitakacho tendeka hapo usoni. Hii ni imani tu na kwa wakati mwingi, huenda ikakosa kuwa sawa. Imani hizi zimepitishwa kutoka kizazi hadi kingine, kutoka kwa babu zetu hadi kwa wajukuu wake wanao endelea kuipitisha kwa vizazi vingine.

Ushirikina Kenya: Aina 5 Zinazo Julikana Kwa Sana

Aina tano(5) za ushirikina ulio wa kawaida sana nchini Kenya

 

  • Kuumiza mguu wako wa kushoto

 

Huenda ikawa umetoka nyumbani kwa furaha tele moyoni. Kuvalia nguo na viatu za kuvutia na una elekea kupatana na mtu fulani. Ukiwa katika safari yako kuelekea mahala pale unajikwaa na kuumiza mguu wako wa kushoto. Watu wana amini kuwa hiyo ni ishara kuwa kitu kibaya kitatendeka. Unapo enda na jambo mbaya linatokea, unakumbuka kuwa ulipewa ishara ambayo hauku zingatia. Watu wengi wana tamani wange umia mguu wa kulia kwani hiyo ni ishara ya bahati. Kutegwa unapo tembea pia ni ishara kuwa kuna mtu anaye kuongelelea mahali. Ulipo tajwa, ukategwa. Imani hii imekuwa kwa miaka mingi.

 

  • Nyota ya risasi

 

Tulipo kuwa wachanga, tulipende kukaa nje na kutazama mbingu. Nyota zilitupendeza kweli kweli. Tuli amini kuwa tunapo ona nyote ya risasi na kusema tunacho tamani huku tume funga macho, vitu tunavyo tamani vingetendeka. Huenda ikawa tuliamini hivi kwani nyota hizi zilikuwa nadra kuona. Hata kama kwa mara nyingi mambo haya haya kuwa yanatendeka, bado tuliendelea kusema tunayo tamani. Hadi wa leo, bado kuna watu wanao amini jambo hili.

 

  • Kunyongwa na mate ama kujiuma ulimi

 

Ishai kutendekea kuwa wakati unapo kuwa ukiongea na watu ama marafiki wako, unajiuma ulimi ama una nyongwa na mate? Najua maswali nyingi zilikupata ukishangaa mbona kumetendeka hivyo. Ikawaje ukajiuma ulimi. Huku Kenya, tuna amini kuwa unapo jiuma ulimi kuna mtu anakusengenya. Pia unapo nyongwa na mate, kuna watu walio kuwa wana ongea kukuhusu. Huenda ikawa umetoka kwa kongamano fulani. Punde tu unapo shika njia kuelekea nyumbani, unajiuma ulimi unapo ongea. Tuna amini kuwa ni watu wa uliko toka wanao ongea kukuhusu.

 

  • Imani kuhusu jino

 

Tulipokuwa wachanga, Tulikuwa tuna ng’olewa meno nyumbani na shangazi ama babu zetu. Sio watu wengi waliokuwa wanaenda kung’olewa meno hospitalini. Tulipo ng’olewa men, nakumbuka wakati mmoja babu yangu akinishauri nilitupe jino hilo kwa paa ya nyumba. Kwani ndege angelichukua na jino lingine lingekua kwa haraka. Watu wengine waliamini kuwa unastahili kulieka jino hilo pembeni mwa kitanda chako. Kwa imani kuwa unapo fanya hivi jino lako lingekua kwa haraka. 

  • Kuwepo kwa bundi

Ndege wa bundi kwa wakati wote ame aminika kuwa ishara ya matukio au mambo mabaya. Ni nadra kwa ndege hawa kuonekana. Tulipo kuwa wachanga mara tu huyu ndege alipo onekana, nakumbuka babu yangu ama babangu akimtupia mawe ili atoke kwa uwanja wa nyumbani. Kuonekana kwake kulikuwa ishara kuwa mtu ata aga dunia katika familia hiyo. Sijui ama ni kukua na imani hiyo ama ilikuwa kweli lakini kila ndege huyu alipo onekana kwa mti karibu na nyumba fulani na wanafamilia wakose kumfukuza, kuna mtu aliye kufa katika jamii hiyo. Kufuatia kukua na imani hii, hadi wa leo, tunapo waona ndege hawa, jambo la kawaida kufanya ni kuwafukuza kwa kuwarushia mawe. 

Tumekuwa tukiamini mambo mengi tangu utotoni, na mengi ya haya yalipitishwa kutoka kwa wazee wetu. Ni ishara kuwa kuna imani ambazo jamii zitaendelea kuamini na kupitisha kwa vizazi vinavyo kuja nyuma yao. Hata tunapo jizuia kufikiria namna hiyo, tuna tumia matukio ya saa hii kuashiria kitacho tendeka hapo usoni. Ushirikina haupatikani Kenya peke yake mbali katika nchi nyingi.

Read Also: Ward Off Black Magic Using These Simple Steps

Written by

Risper Nyakio