Tatizo la ushirikina limekuwa kwa ongezeko kuu nchini Kenya

Tatizo la ushirikina limekuwa kwa ongezeko kuu nchini Kenya

Jambo la ushirikina limekua tangu jadi. Ila hata baada ya mafunzo ya kikristo, jambo hili halija pungua katika familia. Wana biashara wana jitumbukiza katika uraibu huu ili biashara zao ziimarike.

Je, mbona kumekuwa na ongezeko la ushirikina nchini Kenya? Ushirikina ni kuamini mambo yanayo husiana na uchawi na pia amani kuwa kuna miungu wengi. Tatizo hili lina zikumba nchi zinazo kuwa na pwani. Kenya ikiwa miongoni wa taifa hizi. Ripoti mbali mbali zilizo fanywa zina onyesha kuwa Kenya ni miongoni mwa nchi zinazo amini ushirikina. Mataifa mengine kama Ethiopia, Congo, Nigeria, Rwanda na Zambia pia yakiiwemo.

Suala hili la ushirikina Nchini Kenya limekua kwa uongezefu kwa miaka iliyo pita. Nchi hili lina kubaliana na changamoto hili la usherati Kwani hakuna kizuizi cha dini ambalo mtu anapaswa kujiunga nalo. Wananchi wako huru kuabudu popote pale panapo wafaa. Kufuatia uhuru huu, kumekua na madini tofauti katika taifa hili. Dini zingine hazifuatani na mafunzo ya kikristo ipasazwo na wana jihusisha na Imani zilizo tofauti kabisa. 

Chanzo cha ushirikina nchini Kenya

Tatizo la ushirikina limekuwa kwa ongezeko kuu nchini Kenya

  • Tendo hili la ushirikina ni la kitambo ambapo watu walienda kwa watabiri kusuluhisha matatizo yao tofauti. Wali amini kuwa watabiri hawa wana nguvu nyingi tofauti kama vile kutabiri maisha yao yatakavyo kuwa usoni. Wali amini pia watabiri wange wasaidia kusuluhisha shida zao za kifamilia na kimapenzi. Hapo zamani, watabiri walipewa hadhi katika mitaa waliyo ishi. Watu walifunga safari kutoka pande mbali mbali ili kuweza kuwatembelea watabiri hawa.
  • Kufuatia mafunzo ya kikristo yaliyo letwa na wamishonari, umaarufu wa ushirikina nchini uliweza kupunguka. Licha ya masomo ya Mungu, sio kila mtu aliye yaamini masomo haya mapya. Wazee katika jamii walibaki kwa mili na utamaduni za ushirikina.
  • Baadhi ya wananchi na wakristo pia wanajihusisha na tendo hili ili kupata utajiri wa kirahisi. Wahubiri tofauti pia wanasemekana kujihusisha na tendo hili lisilo ambatana na mafunzo ya kijamii. 
  • Watu wana amini kuwa ushirikina unawasaidia kurejesha familia zao zilizo haribika. Ama kurejesha nguvu ya kiume katika wanaume. Wanawake pia wana jitumbukiza kwa uraibu huu ili waweze kupata watoto ama waweke ndoa zao. Walio maliza shule na kukosa kazi wanasemekana kujitumbukiza katika ushirikina ndio wapate kazi. Mabibi wengine pia wanatumia hirizi ili mabwana zao wasi toke nje ya ndoa. Wenye roho chafu pia waliweza kuenda kwa waganga ili kuharibu maisha ya watu walio kuwa mbele yao na kuya vuruga.
  • Wana Biashara kadhalika nchini both kwa sekta ya kibinafsi na ya serikali pia wanasemekana kutumia ushirikina. Ili kuweka biashara zao. Unapo enda kwa mtabiri, unatumia pesa nyingi. Maanake wao huhimiza wanao watembelea kuenda na vitu tofauti. Kama vile pesa ama wanyama kama kuku. Wanatumia pesa nyingi kununua vitu vinavyo hitajika. Pia wanastahili kufanya matembezi zaidi ya mara moja kwa watabiri hawa. Watu kutoka sehemu mbali wanatembea kwa muda mrefu ili kupata services za watabiri ama waganga. Wanatumia hirizi wanazo pewa ili mambo yaende wana vyotaka. Ambapo zingine hazifanyi kazi. Wanatumia pesa nyingi kufanya hivi. Kwa watu wanao tafuta kazi, wanaweza kutumia pesa hizo kuanzisha biashara iwapo ndogo ili kujikimu maishani. Wahubiri wanao jihusisha na uraibu huu pia wanafaa kushikwa Kwani wanawapoteza wafuasi wanao abudu kanisani mwao.

 

Jambo hili la ushirikina limepitwa na wakati. Wanao shiriki katika jambo hili wanastahili kujua sio vyema. Mikakati inafaa kuanzishwa katika maeneo tofauti ya nchi hii kushirikisha juhudi za kuwa elimisha wananchi kuhusu ubaya wa uraibu huu. Wananchi wanafaa kuhimasishwa pia kuachana na tabia za kitamaaduni zilizo pitwa na Wakati. Elimu za kikistro zinafaa kuhimasishwa. Ni muhimu kufunza watu kumtegemea Mwenyezi Mungu iwapo wana kabiliana na matatizo maishani mwao na si kutegemea binadamu wenzao. Uongozi wa nchi pia unaeza anzisha miradi ya kusuluhisha tatizo hili kupitia kueka mikakati mufti katika kuanzisha dini. Ambapo kila mtu anayetaka kuanzisha dini nchini lazima awe na masomo ya theologia na pia aweze kuchunguzwa ipasavyo. Vijana wasio na kazi pia wanaeza pewa kazi ili kuzuia kujiingiza kwa ushirikina ili waweze kufanikiwa kupata kazi. Elimu dhidi ya ushirikina ni muhimu na ita changia pakubwa katika kupigana na ushirikina nchini Kenya. 

 

Read Also: Some African superstitions worth believing because they are backed by science

Written by

Risper Nyakio