Usifanye Vitu Hivi Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Wa C-section!

Usifanye Vitu Hivi Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Wa C-section!

Siku za kwanza chache baada ya kufanyiwa upasuaji wa c-section hazitakuwa rahisi. Kadri uwezavyo epuka kukohoa, kwani utahisi uchungu wa kupindukia kwenye kidonda chako.

Ulifanyiwa upasuaji wa C-section? Usiwe na shaka, hutendeka hata kwa wamama wanao jitayarisha zaidi. Wakati wote vitu haviendi kama tulivyo panga. Na ukajipata katika hali ambapo upasuaji ulikuwa njia pekee ya kujifungua ili kusalamisha maisha yako ama ya mtoto. Huenda likawa ni jambo gumu kwa baadhi ya wamama, lakini hatuna uwezo wa kubadilisha yaliyo fanyika, tuna songa mbele. Chukua mto uuweke kwenye alama yako ya C-section ikawa ungali unapona kwani hapa kuna vitu vyenye ucheshi zaidi. Usifanye haya baada ya upasuaji wa C-section ili kufanya kipindi hiki cha maisha yako kisiwe chenye uchungu mwingi.

Usifanye haya baada ya upasuaji wa c-section

Usifanye Vitu Hivi Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Wa C-section!

 • Usi upoteze wasaa wako ukijuta ama kuhuzunika kwa sababu huku jifungua kwa njia asili
 • Usikubalishe watu walio na maoni hasi kuhusu upasuaji huu wakufanye uhisi vibaya. Ni wengi sana, na wana kelele sana. Sio hatia yako kuwa ulipata upasuaji wa C-section
 • Usifikirie kuwa safari yako nyumbani kutoka hospitalini itakuwa rahisi. Ni kweli, kuwa unaenda nyumbani, na una furaha kupindukia, lakini kila gari linapo simama kwa kasi, utahisi uchungu ambao hukudhania kuwa unaweza hisi. Mshauri anaye endesha, asiwe na kasi, na uwekelee mto kwenye tumbo yako
 • Usikubali kugonjeka, kwa sababu unapo chemua ungali unapona kutokana na c-section, uchungu huo kwenye kidonda utauma sana. Mto unapaswa kuwa mkononi wakati wote kupunguza maumivu hayo.
 • Jisitiri uwezavyo kukohoa ikiwezekana
 • Usile chochote kitakacho kufanya uwe na gesi
 • Usile kitu kitakacho kufanya uvimbiwe ama ushindwe kwenda msalani
 • Ni vyema kucheka, sote tunahitaji kuongezewa siku zaidi duniani, lakini kwa sababu yoyote ile, usicheke ikiwa hauna mto laini mkononi
 • Usisahau kuwa na mito mingi karibu nawe wakati wote. Unaihitaji ili kulinda kidonda chako unapo kohoa, kucheka ama kuchemua. Na pia kujiinua ili usiumizwe na kitu chochote unapo pona
 • Usilie ukikoga na kushangaa wakati ambapo utakuwa sawa. Ni sawa, unaweza lia, lakini kidogo tu, sio nguvu ili kidonda chako kisiume sana
 • Usimkasirikie daktari wako wa afya ya uke kwa kuto fanya miujiza ya kufanya tumbo yako iwe laini tena kama hapo awali baada ya kujifungua. Mawazo yangu kuwa, tumbo hiyo inakusaidia kuto ona kidonda chako

Usifanye Vitu Hivi Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Wa C-section!

 • Usichezee kidonda hicho, ikiwezekana hata usikiangalie. Mruhusu bwana yako afanye kazi hiyo
 • Usitarajie kuganda huko kuende kwa kasi. Baadhi ya wanawake huhisi kuganda huko hata baada ya miaka mitatu
 • Usifikirie kuwa madaktari walificha abs zako. Bado ziko, ila,,, itachukua muda kwako kuhisi kama unaweza zitumia tena
 • Usijisumbue na kazi za nyumbani. Waache marafiki na jamaa wako wakusaidie na kazi za kupika na kusafisha ili umakinike na uponaji wako na usikimbize vitu kwani utapunguza uponaji kasi
 • Usipande stairs ikiwezekana. Katika kipindi hiki, hamia kwa chumba usipo hitajika kupanda ngazi
 • Usisahau kuwa dawa za uchungu ni rafiki zako katika kipindi hiki. Kumbuka usichukue nyingi sana, lakini za kutosha, wakati unaofaa, ili usi hisi uchungu na uwe na wakati mwema na mtoto wako ama watoto wako kwa wamama walio na zaidi ya mmoja
 • Na kamwe usifikirie kuwa wewe sio mama aliye komaa kwa sababu hauku jifungua kwa njia asili. Mtoto alitoka kwenye mfuko tumboni mwako akiwa hajafunikwa kama zawadi.

Ni matumaini yangu kuwa wamama wote walio jifungua kupitia upasuaji wa C-section wata pona kwa kasi!

Soma Pia:Ulifahamu Kuwa Alama Yako Ya Upasuaji Wa C-section Inaweza Pona?

Written by

Risper Nyakio