Mojawapo ya majukumu ya mwanamme ni kumpenda na kuhakikisha kuwa mwanamke aliye maishani mwake ana furaha. Hata hivyo, haijalishi jinsi unavyo mpenda mpenzi wako wa kike, usifanye vitu hivi ili kumfanya akupende zaidi. Mapenzi yanapaswa kuwa na mipaka yake, hasa kama mnaanza kujuana na hamjaingia katika ndoa. Wanaume, tahadhari, usifanye vitu hivi kumfurahisha mwanamke.
Usifanye vitu hivi kumfurahisha mwanamke

- Kumlipia karo ya shule
Kama mmejuana kwa kipindi kifupi na mwanamke, epuka kumlipia karo ili kumfanya akupende zaidi. Kumsaidia anapokwama na kutatizika ni sawa, ila, kumlipia karo ya shule sio kitu unachotaka kufanya mwanzoni mwa uhusiano wenu. Ikiwa utafanya uamuzi wa kumlipia karo, usitarajie afanye kila kitu unachomwambia kana kwamba ana deni yako.
2. Kupuuza malengo yako ya maisha
Ulikuwa na malengo fulani ya kimaisha kabla ya kupatana na mchumba wako. Baada ya kupatana, ikiwa anakueleza kuwa hapendelei njia ya kikazi unayofuata. Sio ishara ya kuachana na kazi yako na kutupilia mbali malengo yako ya kimaisha. Mtu anayekupenda kwa kweli atakusukuma kutimiza malengo yako na wala sio kukukatisha tamaa ya ndoto zako.

3. Kutoiheshimu familia yako
Ikiwa mchumba wako wanakorofishana mara kwa mara na wakwe zake. Huenda akakuathiri kuona kuwa familia yako ndiyo inadoa. Kabla ya kufanya uamuzi wowote, chukua muda kuelewa vurugu hizi zinasababishwa na nini. Kisha ufanye uamuzi na utatue suala hilo. Mchumba wako hapaswi kuwa chanzo chako kuichukia familia yako. Kumbuka kuwa, uhusiano wenu unaweza kuisha, ila, familia yako itabaki kuwa jamii yako.
4. Kupuuza mahitaji yako kwa sababu ya yake
Mapenzi hufanisi pale ambapo wachumba wanapokuwa bila ubinafsi. Ila, sio kumaanisha kuwa unastahili kutojichunga na kupuuza mahitaji yako ili kutimiza yake. La hasha, jitunze unapomtunza mpenzio pia. Mapenzi yatakuwa na ufanisi unapoweza kujitunza na kujiendeleza kimaisha.
5. Kufanya uhalifu kwa sababu yake
Huenda ukawa umempenda binti mwenye mahitaji mengi na ghali. Usipoweza kutimiza mahitaji yake, huenda ukapata jaribio la kufanya uhalifu ili kukimu mahitaji yake. Ikiwa kwa kweli anakupenda, ataelewa unapokosa kutimiza matakwa yake. Tafuta hela kwa njia kamili.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Sababu 3 Kwa Nini Wanawake Wanachelewa Kupata Watoto