Jinsi Ya Kujitayarisha Usiku Kabla Ya Upasuaji Wa C-Section

Jinsi Ya Kujitayarisha Usiku Kabla Ya Upasuaji Wa C-Section

Siku yako ya kujifungua na una fanya matayarisho ya kujifungua. Kuna vitu vichache unavyo paswa kufanya usiku kabla ya upasuaji wa c-section.

Usiku kabla ya upasuaji wa C-section, huenda ukahisi kana kwamba una shimo, hauna uhakika cha kufanya. Kati ya mambo yote, kila kitu ni mchanganyiko wa kukosa hamu na kuwa na uwoga wa kujifungua. Mengi yame chapishwa kuhusu upausji, mambo ambayo huenda yakaenda mrama na mengine sawa, lakini sio tosha kuhusu unachopaswa kufanya usiku kabla ya upasuaji.

Upasuaji wa Cesarean section (C-section) ni utaratibu wa upasuaji wa kimatibabu kujifungua mtoto ambapo unapasuliwa tumbo hadi kwenye uterasi na mtoto ana tolewa. Hata kama C-section huenda ikawa haitarajiwi, ukiwa unafahamu siku ambapo unatarajia kujifungua, hupaswi kupuuza uwezekano wa upasuaji wa C-section.

Kulingana na daktari Dana Sullivan, aliyekuwa kwa sehemu ya upasuaji wa C-section na mwandishi wa The Essential C-Section Guide (Broadway Books), anasema kuwa, "Iwapo hautarajii ama la, hakuna sababu ya kuwa na hisia hasi kuhusu upasuaji. Kujua jinsi ya kutayarisha na kufanya upasuaji uwe wa kipekee, huenda kukafanya upasuaji usiwe mgumu na wa kuogofya."

Mambo ya kufanya usiku kabla ya upasuaji wa C-section

what to do on the night before c section

Hapa kuna vitu vichache unavyopaswa kufanya usiku kabla ya siku yako kuu:

  • Angalia mkoba wako 

Nafasi kubwa ni kuwa usha weka begi utakayo beba na vitu vyote ambavyo huenda ukahitaji hospitalini usiku kabla ya upasuaji. Kwa hivyo angalia iwapo begi ama mkoba huo una vitu vyote ambavyo utahitaji ukiwa hospitalini. Ili usisahau vitu muhimu nyumbani.

  • Angalia mipango uliyofanya na hospitali

    Usiku kabla ya upasuaji wa C-section ni kama mipango yoyote ile uliyo fanya maishani mwako. Piga simu hospitalini kuhakikisha kuwa mipango yote iko sambamba. Hasa iwapo upasuaji wako ni wa masaa ya asubuhi na una mipango ya upasuaji wa kibinafsi. Waulize iwapo ungetaka mwenzi wako ama jamaa wako kwenye chumba hicho. Pia ongea na mtu atakaye kupeleka hospitalini na kukuchukua baada ya upasuaji.

  • Jitayarishe kiakili

Chukua muda kukubali kuwa mwanao ako karibu kuwasili. Jadili kuzaliwa kwake kunako karibia na mtu unaye mwamini. Huenda ikawa mwenzi wako, rafiki ama jamaa. Unaweza chukua dakika chache kuongea na mtoto wako ili kuwa na utangamano. Pia, huenda pia ukafanya uamuzi wa kupanga sherehe ndogo, mishumaa michache ili kumsherehea mtoto wako.

  • Kaa njaa

stay prepared on the night before c section

Hospitali nyingi hukukumbusha hivi siku kabla ya upasuaji. Ila, iwapo hawata kukumbusha, kuwa na wazo hili akilini. Usinywe ama kula kitu chochote masaa manane hadi kumi na mawili kabla ya upasuaji wako.

  • Weka kengele/saa ikuamshe

Usiku kabla ya upasuaji wa C-section, huenda ukawa na shaka na uwoga na kuwa na matarajio mengi hapo kati. Kwa hivyo, huenda ikawa vigumu kwako kupata usingizi. Na unapo lala usiku sana, huenda ukalala baada ya wakati unaofaa kulala. Upasuaji uliopangwa mara nyingi huwa wakati wa asubuhi. Kwa sababu mama haruhusiwi kula chochote usiku kabla ya upasuaji, ni vyema kujitayarisha ipasavyo.

Ni muhimu kujitayarisha kwa mambo usiyo tarajia hata, hata kama umepanga kujifungua kwa njia asili. Usipuuze uwezekano wa upasuaji. Jadili uwezekano huu na daktari wako kwa hivyo iwapo kutakuwa na mabadiliko, unaweza kuwa tayari.

Soma pia: Mambo 21 Usiyo Paswa Kufanya Baada Ya Upasuaji Wa C-Section

Written by

Risper Nyakio