Tafadhali nakuomba usimbusu mtoto wangu akiwa angali mchanga

Tafadhali nakuomba usimbusu mtoto wangu akiwa angali mchanga

Mtoto mchanga ana uwezo duni wa kupigana na magonjwa. Ni muhimu kwa jamii na rafiki wanao mtembelea mama aliye jifungua kuzingatia kuto mbusu mtoto huyu. Fanya mambo ambayo mama amekuuliza kufanya

Umejifungua mtoto wako sasa, ila sio wewe peke yako unaye fikiria kuwa ana pendeza. Familia yako, marafiki na wafanya kazi wenzako na wao wamekuja kukutembelea na kila mmoja anapendezwa na urembo wa mwanao. Baadhi ya watu hawata jizuia kumpa busu kwa midomo yake ama usoni. Ukifungua roho yako, utakubali kuwa haufurahikii jambo hili la watu kumbusu mwanao, haswa mdomoni. Inaonekana hamna njia bora ya kuwaimbia “tafadhali usimbusu mtoto wangu mchanga” bila kukaa mjeuri. Naam, tuko hapa kukujulisha kuwa kuna njia zisizo na makali za kusema hivi. Lakini kwanza, tu angalia umuhimu wa kulichukulia jambo hili kwa umakini.

 

Je, kuna umuhimu wa watu kuto mbusu mtoto wako kwenye midomo?

 

Uwezo wa kupigana na magonjwa duni

Uwezo wa mwanao wa kupigana na magonjwa uko chini sana. Ako hatarini ya kuambukizwa na magonjwa na virusi. Kwa kawaida, watoto wazee na watu wazima wakikumbana na magonjwa haya, wata weza kupigana na magonjwa haya kwa urahisi. Lakini kwa watoto, vidudu hizi vina hatari kuu. Mtoto anapo patwa na ugonjwa wa meningitis kutoka kwa busu la mtu aliye na kikohozi, kunaweza mfanya mtoto kuaga dunia. Kuna kesi nyingi za watoto waliofariki kufuatia kuambukizwa ugonjwa wa herpes na mtu ambaye hakujua ana ugonjwa ule. Kuna wakati mtoto wako ataweza kupigana na magonjwa lakini kabla ya wakati huo, anakutarajia kumlinda.

Tunaelewa! Watoto wana furahisha kwa kweli. Mashavu ya duara yaliyo laini. Nywele iliyo rahisi na harufu inayo vutia. Uzuri wote huu wa mtoto ni njia ya dunia ya kuhakikisha wazazi wana weza kuishi na kukosa usingizi, milio na kuchafuliwa nguo.

Hili sio kusema kuwa tunapaswa kuwaficha watoto wachanga hadi wanapo komaa. Ila tuna paswa kuchukua tahadhari kama wazazi walio wajibika na pia kama watu wazima walio na jukumu kwa watoto Wadogo. La kusikitisha ni kuwa sio watu wazima wote wanao elewa hatari zinazo kuja na kuwa busu na kuwapakata watoto wadogo. 

 

Baadhi ya usalama ambao familia na wageni wako wanaweza angazia

 • Hakikisha wanao mchunga mtoto na mama wana chanjo inayo faa.
 • Zoea kunawa mikono vizuri.
 • Hakikisha kuwa kila mgeni ana nawa mikono kabla ya kumshika mtoto.
 • Hakikisha kuwa yeyote mwenye ugonjwa, kikohozi ama vidonda ana epuka kumshika mtoto.
 • Zingatia usafi nyumbani mwako.
 • Kama lazima wampe mwanao busu, na wana afya bora, wambusu kwa miguu ama nyuma ya kichwa.

Watoto wanatufanya sote tusahau kila kitu. Katika muda mdogo, tunapoteza akili zote. Tuna chapisha picha zao wakiwa uchi na kuambatanishwa na maneno yanayo udhi.

Kwa hivyo tunaelewa sababu itakayo ifanya kuwaambia "usimbusu mtoto wangu" kukaa jeuri. Kama hauna uhakika, wa jinsi ya kulisema hili, turuhusu tukusaidie.

 

Jinsi Za Kusema “Usimbusu Mwanangu” Zisizo Na Makali.

Tengeneza makaratasi yanayo vutia na uziweke pahala wageni wanapo kaa ambapo hawatakosa kuziona. Maneno hayo yanafaa kusoma lolote kati ya haya:

 1. Najua ni ngumu kuto mbusu na kumpakata, lakini tafadhali Jizuie. Asanti.
 2. Vijidudu vyako ni vikubwa sana kwangu. Tafadhali usinipe busu!- mtoto.
 3. Vijidudu vitani adhiri. Tafadhali nawa mikono yako na ungoje kunipa busu baada ya miezi michache. Bado nakupenda. – mtoto
 4. Mama na baba walisema hakuna mabusu!
 5. Hakuna mabusu!

Hili silo jambo la milele la kuto mbusu. Mtoto anapo pewa chanjo na ana nafasi ya kukuza uwezo wake wa kupigana na virusi na magonjwa. Baada ya miezi michache, mtoto atakuwa akiilamba sakafu anapo tambaa.

Kama mtoto mdogo, anaweza ujaza ukuta na kinyesi na kumwaga msalani. Kabla ya wakati mrefu, tunawapata watoto wakinyonya pipi zilizo liwa wanazo zipata kwa viti. Tafadhali zingatia "usimbusu mtoto wangu" unapo enda kuwatembelea marafiki wako.

Read Also: Open Letter: My Tryst With Postpartum Depression

Written by

Risper Nyakio