Usingizi Wa Mtoto: Mambo Ya Kufanya Na Kuto Fanya

Usingizi Wa Mtoto: Mambo Ya Kufanya Na Kuto Fanya

Mtoto wako anapo fikisha miezi sita, anapaswa kuwa akilala kwa muda mrefu angalau lisaa limoja ama mawili. Na wala sio kwa dakika 20 kisha kuamka.

Usingizi ni muhimu sana kwa watoto wachanga. Ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha kuwa mtoto analala vizuri bila kutatizika. Katika wakati huu, mama ata pata chanya cha kulala na kupumzika kwa sababu ni vigumu kupumzika ama kufanya kazi zake mtoto akiwa ameamka. Mambo muhimu ya kuzingatia katika usingizi wa mtoto.

Usingizi wa Mtoto: Fanya mambo haya

usingizi wa mtoto

  1. Mtoto wako anapo kula miayo, fahamu kuwa ni wakati wake wa kulala. Akijikuna macho, kulia ama kuanza kusumbua ana ashiria anataka kulala. Mtoto aliye choka huwa na matatizo zaidi ya kulala. Kuwa mwangalifu kuona mojawapo ya ishara hizi.
  2. Watoto hulala kwa masaa mengi hadi masaa 16 kwa siku, huku wakiamka kwa vipindi vifupi kula na kubadilishwa nepi. Wanapo fikisha miezi mitatu, wanaanza kuwa na utaratibu wa kulala na kupunguza masaa wanayo lala. Wana anza kulala zaidi wakati wa usiku na kwa muda mfupi mchana.
  3. Kwa kawaida, watoto hulala baada ya kunyonya ama kama analishwa na kichupa. Wakati huu ni muhimu kwa mama na mtoto kwani wana tangamana na kuhisi wako karibu. Huenda ukapata kuwa kumlisha mtoto ndiyo njia ya kipekee ya kumfanya alale. Baada ya muda, utahitajika kumfunza jinsi ya kulala peke yake. Mbadili nepi kisha katika muda kati ya kula na kulala kwake.
  4. Epuka kumchukua mtoto anapo lia, kuchefua, ama kutoa sauti akiwa amelala. Huenda akawa bado amelala, unapo mchukua, itakuwa vigumu kwake kurudi kulala tena. Muangalie tu kuhakikisha kuwa kila kitu kiko shwari.
  5. Mlaze mtoto kitandani chake anapo anza kusinzia. Usimshike hadi anapo lala. Kufanya hivi kutamsaidia kujifunza jinsi ya kulala peke yake. Pia ataweza kujituliza hadi alale anapo amka kati kati ya usiku.
  6. Usalama wa mtoto wako ni muhimu sana anapo lala. Akilala sakafuni ama kwenye kiti, hakikisha kuwa unambeba na kumpeleka kitandani. Kwa njia hii analala vizuri na mgongo wake hauumii. Kumbuka kutoa mito na blanketi zaidi kwenye kitanda chake kuepuka kifo cha ghafla katika watoto (SIDS).

Mambo ya kuto fanya

maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu

  1. Usimkubalishe mtoto wako kulala kwa muda mrefu akiwa ameketi, kama vile kwenye kiti ama kwenye gari. Unapo gundua kuwa mtoto wako anasumbuliwa na usingizi, mlaze kitandani.
  2. Mtoto wako anapo fikisha miezi sita, anapaswa kuwa akilala kwa muda mrefu angalau lisaa limoja ama mawili. Na wala sio kwa dakika 20 kisha kuamka. Unaweza mchezesha ili anapo lala alale kwa muda. Kufanya hivi kutamsaidia kujua kuwa usiku ni wakati wa kulala na kulala kwa muda mrefu.
  3. Tengeneza utaratibu wa kulala na uuzingatie kadri unavyo weza. Fanya hivi kwa kumhimiza alale wakati sawa kila siku. Epuka kumlaza wakati wa alasiri ili asitaabike kulala vizuri usiku. Anapo lala hata mchana, mlaze kwenye kitanda chake, huku kutamhimiza kujua kuwa kitanda chake kina ashiria usingizi ama wakati wa kulala.

Soma Pia:Vidokezo 4 Vya Kuboresha Usingizi Wa Mtoto Na Mama

Written by

Risper Nyakio