Wanadada!Epuka Kuyasema Mambo Haya Kwa Mchumba Wako Mnapo Fanya Mapenzi

Wanadada!Epuka Kuyasema Mambo Haya Kwa Mchumba Wako Mnapo Fanya Mapenzi

Wanandoa wanapo zungumza mara kwa mara, wanaelewana vyema na jinsi ya kumfurahisha mwingine. Ni vigumu kufikiria kuna mwanamme asiye mpenda mwanamke anaye jieleza kitandani. Na vitu ambavyo wanaume hupenda kusikia wanapo fanya mapenzi hutofautiana kutoka kwa utendaji wao kitandani hadi kwa mazungumzo ya kimapenzi kwa wanao penda vitu kama hivyo. Kila mwanamme anapenda kitu fulani, na ni sawa kwani watu wote wana tofautiana. Ila leo, tungependa kuangazia kitu tofauti. Dada, usiseme mambo haya mnapo fanya mapenzi!

Orodha Ya Mambo Ya Kuepuka Kusema Mnapo Fanya Mapenzi: Usiseme Mambo Haya Mnapo Fanya Mapenzi

usiseme mambo haya mnapo fanya mapenzi

  1. Je, unanipenda?

Huenda ikawa uliyasikia haya mahali. Kuwa kufanya mapenzi ni fizikia kwa wanaume na hisia kwa wanawake. Na wakati ambapo mazungumzo wazi kuhusu uhusiano wenu ni jambo la busara, huu sio wakati sawa wa kuwa na mazungumzo haya. Kuna wakati sawa wa kila kitu, ila, huu sio wakati bora wa mazungumzo ya aina hii. Huu ni wakati wenu kuhisi mapenzi.

2. Huu ni uhusiano wa aina gani?

Huu ni mfano mwingine wa jinsi wanawake wanavyo husisha ngono na hisia. Sio vibaya kufanya hivi, ila tuna dhani kuwa, huu sio wakati mwafaka wa mazungumzo haya.

Unaweza hifadhi swali hili hadi pale mnapo maliza kipindi chenu cha kufanya mapenzi. Ama wakati mwingine msipo kuwa kitandani, mnapo zungumza kuhusu vitu vingine, kisha unaweza ibua suala hili.

3. Unajaribu kufanya nini?

usiseme mambo haya mnapo fanya mapenzi

Mara nyingi, swali hili huja baada ya mchumba wako kukubusu na kukupasa kwa muda wa dakika 10 ama zaidi. Tungependa kudhania kuwa nyote mlifahamu mlichokuwa mnafanya mlipo anza kipindi chenu cha mabusu na kupapasana. Swali hili mara nyingi huharibu kipindi hiki, na hamu ya kufanya mapenzi kuisha.

4. Je, unafikiria nina uzito mwingi?

Ni jambo la kawaida kwa wanawake kuwa na shaka kuhusu uzito wao wa mwili. Na mkiwa na mazungumzo wazi na mchumba wako, hili ni swali ambalo linaweza ibuka kiasili.

Lakini, haijalishi jinsi mlivyo karibu na mchumba wako. Huu sio wakati mwafaka wa kumwuliza mawazo yake kuhusu uzani wako. Mna wakati mwingi sana wa kuwa na mazungumzo haya, mbali na wakati huu.

5. Pesa nilizo kuitisha ziko wapi?

Sote twapenda pesa, hasa wachumba wetu wanapo taka tununue kitu ambacho tumekitamani kwa muda mrefu. Ngoja hadi baadaye kisha umwulize kuhusu jambo hili.

Soma piaSababu Kwa Nini Uhusiano Wako Haudumu: Jinsi Ya Kuwa Na Uhusiano Unao Dumu

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio