Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Usiyafanye Haya Baada Ya Kupoteza Mimba: Afya Yako Baada Ya Kupoteza Mimba

3 min read
Usiyafanye Haya Baada Ya Kupoteza Mimba: Afya Yako Baada Ya Kupoteza MimbaUsiyafanye Haya Baada Ya Kupoteza Mimba: Afya Yako Baada Ya Kupoteza Mimba

Mwanamke yeyote aliyepoteza mimba anafahamu kuwa kuharibika kwa mimba ni jambo linalo wafilisisha haijalishi umri wa mimba kabla ya kuharibika kwake.

Mwanamke yeyote aliyepoteza mimba anafahamu kuwa kuharibika kwa mimba ni jambo linalo wafilisisha haijalishi umri wa mimba kabla ya kuharibika kwake. Hasa kama alikuwa amepanga ujauzito na alikuwa anatarajia kuitwa mama kwa sana. Kupona baada ya kupoteza mimba sio jambo rahisi. Mama, usiyafanye haya baada ya kupoteza mimba.

Usifanye mambo haya baada ya kupoteza mimba

losing a baby, ishara za mama kupoteza mimba

  • Kuhisi uko peke yako

Baada ya kupoteza mimba, utahisi kana kwamba wewe pekee ndiye uliyepoteza mimba na hakuna mtu anayeelewa unachokipitia. Usihisi hivi.

Ukweli ni kuwa, kupoteza mimba hufanyika kwa sana. Kupoteza mimba kabla ya kujifungua pia hufanyika na ni maarufu kuliko watu wanavyojua. Hatari ni kuwa, watu hawazungumzii vya kutosha jambo hili. Ikiwa ungependa watu wajue unachokipitia ama ungependa kupona kwa usiri wako, usihisi kana kwamba uko peke yako.

  • Usijilaumu

Ni vigumu kutohisi kana kwamba haukufanya jambo lililosababisha tokeo la kupoteza mimba. Kuhisi hatia jambo mbaya linapofanyikia mtu aliye muhimu kwetu, na hakuna mtu muhimu kwa mama kuliko mwanawe. Kuna njia za kukusaidia kutohisi hatia baada ya kupoteza mimba.

  • Kushangaa iwapo uko sawa

Safari ya kila mtu ya majonzi huwa tofauti. Wengine wanataka kuwajulisha watu wanachokipitia na kusaidiwa kuegemezwa kihisia na marafiki zao, wakati ambapo wengine wanapenda kunyamaza na kuwajuza watu wachache wanao waamini.

  • Kusikiliza maoni hasi

Kupoteza ujauzito ni jambo ambalo kama jamii, hatuzungumzii vya kutosha. Kwa hivyo, mama anaposema kuwa amepoteza mimba, watu wengi hawajui jinsi ya kumpa faraja.  Na hivyo basi, huenda wakajipata wakisema maneno yanayo mwumiza mama.

usiyafanye haya baada ya kupoteza mimba

  • Kuiweka kama siri

Hata kama hutaki kumwambia kila mtu kilicho tendeka na unachokipitia, kuzungumza na watu wachache kutasaidia kupunguza mzigo wa unayopitia. Pia, unapowajulisha marafiki wa karibu na familia kilichokutendekea, watajua jinsi ya kuwa wanapokuwa karibu nawe.

  • Kupuuza mahitaji yako ya kihisia

Kuziba hisia na kuendelea na maisha yako kana kwamba hakuna kitu kilichofanyika kutakuwa na athari hasi zaidi. Ni muhimu kwa mama kujipa wakati wa kuomboleza na kukubali kilichofanyika. Kubeba kila kitu moyoni kana kwamba hakuna kitu kisichokuwa sawa kutakuathiri baadaye. Ikiwezekana, chukua wiki chache ubadili mazingira yako ili uweze kupona.

  • Kuepuka msaada wa kitaalum

Umejipatia wakati mwingi na subira. Umekuwa na siku nzuri baada ya kupoteza mimba na siku sawa ama zaidi ambazo hazikuwa sawa. Katika siku mbaya, ni vigumu kutoka kitandani. Hauna nishati ya kufanya kitu chochote, hata vitu ambavyo ulivipendelea hapo mbeleni. Hauna hamu ya kula ama kunywa ama kuwasiliana na watu. Ikiwa unahisi hivi, ni wakati wa kupata usaidizi wa kitaalum.

Usiyafanye haya baada ya kupoteza mimba huku ukiendelea kupona. Mpigie daktari wako mzungumze naye.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Maambukizi 10 Yanayo Sababisha Mama Mjamzito Kupoteza Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Miscarriage
  • /
  • Usiyafanye Haya Baada Ya Kupoteza Mimba: Afya Yako Baada Ya Kupoteza Mimba
Share:
  • Je, Mimba Ya Miezi Mitatu Inaweza Kutoka? Ishara Za Mapema Za Kupoteza Mimba

    Je, Mimba Ya Miezi Mitatu Inaweza Kutoka? Ishara Za Mapema Za Kupoteza Mimba

  • Kuvuja Damu Katika Mimba: Dalili Za Mimba Changa Kuharibika

    Kuvuja Damu Katika Mimba: Dalili Za Mimba Changa Kuharibika

  • Jinsi Ya Kurejelea Maisha Baada Ya Kuharibika Kwa Mimba

    Jinsi Ya Kurejelea Maisha Baada Ya Kuharibika Kwa Mimba

  • Je, Mimba Ya Miezi Mitatu Inaweza Kutoka? Ishara Za Mapema Za Kupoteza Mimba

    Je, Mimba Ya Miezi Mitatu Inaweza Kutoka? Ishara Za Mapema Za Kupoteza Mimba

  • Kuvuja Damu Katika Mimba: Dalili Za Mimba Changa Kuharibika

    Kuvuja Damu Katika Mimba: Dalili Za Mimba Changa Kuharibika

  • Jinsi Ya Kurejelea Maisha Baada Ya Kuharibika Kwa Mimba

    Jinsi Ya Kurejelea Maisha Baada Ya Kuharibika Kwa Mimba

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it