Utaratibu wa Afya Ya Meno Ni Salama Kwa Ujauzito?

Utaratibu wa Afya Ya Meno Ni Salama Kwa Ujauzito?

Is dental anesthesia safe during pregnancy? What dental procedures are allowed while pregnant? Here are the answers to your questions...

Afya ya meno, utaratibu wa kugandishwa meno ni salama kwa ujauzito? Ni utaratibu upi wa meno unakubalika unapokuwa mjamzito? Tuna pata maswali mengi sana kama haya kutoka kwa mama watarajia kwenye theAsianparent app.

Wakati wa ujauzito, matatizo mengi ya meno huwa kawaida:
 • Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito yanaweza kufanya ufizi kuwa kwenye hatari kubwa ya ukoga unaosababisha kufura na kuvuja damu. Hii pia hujulikana kama  gingivitis ya ujauzito ama ugonjwa wa ufizi.

Unaweza kugundua kuwa ufizi wako huvuja damu kwa wepesi, haswa unapopiga meno mswaki. Hili huonekana mara nyingi kati ya mwezi wa pili na wa nane wa ujauzito.

 • Ujauzito pia huongeza nafasi ya kupatwa na periodontitis (maambukizi ya ufizi) kwa sababu ya ongezeko la estrogen na progesterone.

Periodontitis ni hali mbaya kuliko gingivitis, inajumuisha uharibifu wa mifupa inayozingira meno. Hili linaweza kusababisha meno yako kutingika. Iwapo itaendelea bila ya matibabu, unaweza kupoteza meno inayotingika. Ata, kulingana na utafiti, periodontitis huhusishwa na uchungu wa uzazi wa mapema na kumpata mtoto wenye uzito wa chini.

 • Kuoza kwa meno kunaweza kuongezeka kwa sababu ya mabadiliko kwenye lishe kama vile kukula vyakula vilivyo na sukari nyingi, ongezeko la asidi kwenye kimya kwa sababu ya kutapika, kinywa kilichokauka, ama afya iliyodhoofika ya kimya kutokana na kichefuchefu na kutapika.
 • Is dental anaesthesia safe during pregnancy?

  Picha: Shutterstock

Je, utaratibu wa kugandishwa meno ni salama kwa ujauzito?

Ni bora kuchelewesha mambo yote yanayohusiana na meno iwapo siyo ya dharura (kama vile kusafisha meno ama utaratibu wa urembo) hadi baada ya kujifungua. Iwapo kuna jambo la dharura, hakikisha kuwa daktari wako wa meno amejua kuwa wewe ni mjamzito.

Matibabu ya meno, kama ni lazima, hufanyika kwenye kipindi kati ya mwezi wa nne na wa sita wa ujauzito ili kupunguza madhara. Ni bora kujiepusha wakati wa kipindi cha miezi mitatu ya kwanza  kwa sababu huu ndio wakati muhimu sana kwenye kukua kwa mtoto. Matibabu katika miezi mitatu ya mwisho pia haipendekezwi kwa sababu ya kule kulala chali wakati wa kufanyiwa matibabu.

Iwapo meno yanahitaji kujazwa, amalgam inafaa kutotumika na kitu kingine mbadala kutumika (kama vile tooth-colored resins), ambazo hazina utaridi. Hizi zinafaa kutumika badala yake ili kuzuia uharibifu unaotokana na utaridi.

Iwapo utahitaji picha ya meno ya X-ray, daktari wako atangoja mpaka umempata mtoto wako, hata kama X-rays nyingi za meno hazidhuru tumbo(abdomen) ama nyonga.

Kwa maarifa zaidi, chuo cha America cha obstretrics na gynecology kilisema kuwa picha zote za meno (ambazo risasi imetumika kufunika tumbo na tezi) ni salama wakati wa ujauzito. Daktari wako wa meno atafunika koo kwa kutumia kitambaa chenye risasi ili kukinga tezi  kutokana na miale ya picha.

Pia, kazi ya kurekebisha meno uhusisha antibaotiki kuzuia ama kutibu maambukizi. Antibaotiki kama vile penicillin, amoxicillin na clindamycin ambazo hujulikana kama kundi la B kwa usalama wakati wa ujauzito, zinaweza kuamrishwa baada ya matibabu.

Iwapo ulikuwa unabana meno kwa kutumia braces na ukawa mjamzito, kubadilishwa kwa braces ni salama kwa kipindi chote cha ujauzito. Ingawaje, haipendekezwi kuweka braces wakati wa ujauzito.

Je, kugandishwa kwa meno ni salama wakati wa ujauzito?

Ni vizuri kumjulisha daktari wa afya ya meno wako kuhusu ujauzito ili waweza kufanya uchaguzi juu ya kugandishwa kuliko bora na kipima viwango vinavyotarajiwa. Kulingana na American college of Obstretrics and Gynecology, matumizi ya kugandishwa kinyumbani kwa kutumia (lidocaine with or without epinephrine) ni salama wakati wa ujauzito.

Utafiti uliyofanyika Agosti 2015, katika jarida la  American Dental Association uliwafuata kina mama waliokuwa wamefanyiwa matibabu yaliyotumia kufa ganzi kama vile lidocaine na kundi lingine ambalo halikutumia. Utafiti ulionyesha kuwa matibabu haya yalikuwa salama wakati wa ujauzito kwa sababu hayaleti utofauti kwenye visa vya kupoteza mimba, kuzaa watoto wenye kasoro, kujifungua kabla ya wakati ama matatizo ya uzito kwa mtoto.

Is dental anaesthesia safe during pregnancy?

Picha: Shutterstock

Kulingana na mwandishi wa machapisho hayo Dr Hagai, “uchunguzi wetu haukupata ushahidi wowote kuonyesha kuwa matibabu ya meno ukitumia nusukaputi ni mbaya wakati wa ujauzito. Tuliangazia kutambua iwapo kulikuwa na hatari iliyohusiana na matibabu ya meno ukitumia nusukaputi na matokeo ya ujauzito. Hatukupata athari zozote zile.”

Naweza ng’olewa jino nikiwa mjamzito?

Kwa kila juhudi, daktari wako atajaribu kuokoa jino lako. Ingawaje, kama jino lako limeharibika sana kwa kuoza ama kujeruhiwa, linaweza kuweka afya yako ya kimya ama mwili wote kwenye hatari na ni bora kutolewa.  Bakteria kutoka kwa jino lililooza zinaweza kutapakaa kila mahali kwenye mfumo wako wa damu.

Kuna uwezekano daktari wako atapendekeza kipindi cha kati ya mwezi wa nne hadi wa sita kama bora zaidi kutoa meno. Kwa hio njia unaweza kuepukana na X-rays katika kipindi mahututi cha kwanza cha ujauzito, na pia adha inayotokana na kulala chali kwa muda mrefu wakati wa kipindi cha mwisho cha ujauzito/ trimesta ya tatu.

Ni vyema kuondolewa mizizi ya jino wakati wa ujauzito?

Wakati jino lako linapooza hadi kufikia ndani ya jino kwenye neva  inaweza kuwa chungu sana.

Katika matibabu ya kuondoa mizizi, unarekebisha  na kuokoa jino ambalo limeoza  sana ama lenye maambukizi. Wakati wa kuondoa mizizi, neva na shapo hutolewa kutoka kwa jino na ndani yake huoshwa na kufungwa. Hilo jino kisha hujazwa kwa kutumia taji linalofanana na hayo meno mengine. Hili huondoa haja ya kungoa jino.

Wakati wa dharura, kuondoa mizizi kwenye jino  kunaweza kufanyika  wakati wowote wa ujauzito na si lazima kucheleweshwe. Ingawaje, kwa vile miale ya X-rays hutumika, wakati mwafaka wa matibabu ni katika trimesta ya pili ya ujauzito.

Is dental anaesthesia safe during pregnancy

Naweza kufanya meno kuwa meupe wakati wa ujauzito?           

Ni vyema kuchelewesha kusafisha meno na mambo mengine ambayo si ya dharura ya urembo hadi baada ya kujifungua.

Matibabu kama hayo yanafaa kuepukika haswa wakati wa miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito kwani unaweza hisi adha kulala chali wakati ile dawa ya kungarisha meno inapopakwa na kupona.

Iwapo unatumia vingarishi mbadala pale nyumbani, hakikisha kuwa umeangalia kiwango cha hydrogen peroxide kisipite asilimia sita.

Naweza kufanyiwa matibabu ya orthodontic wakati wa ujauzito?

Iwapo umeanza matibabu ya orthodontic tayari, unaweza kuendelea nayo ata baada ya ujauzito. kwa sababu ya mabadiliko kwenye homoni, wanawake wengine wajawazito wanaweza pata kufura kwenye ufizi. Ambayo inaweza kusababisha kujikuna kwenye nyaya za kufunga meno. Daktari wako anaweza kupendekeza dawa zilizo salama za kupaka kupunguza uchungu.

Iwapo unafungwa meno kwa mara ya kwanza wakati uko mjamzito, daktari wako atapendekeza ungoje hadi baada ya kujifungua.

Hii ni kwa sababu kuweka hizi nyaya huhitaji X-rays ambazo unataka kuepukana nazo haswa wakati wa ujauzito. Pia, unaongeza uzito wakati wa ujauzito, ambalo huleta mabadiliko kwenye sura ya uso, mdomo na hufanya kuweka na kurekebisha hizi nyaya kuwa ngumu.

Kutunza meno wakati wa ujauzito

Hivi ndivyo unavyofaa kutunza meno na ufizi wako wakati wa ujauzito:

 • Safisha meno yako vizuri mara mbili kila siku kwa dakika mbili ukitumia dawa ya meno iliyo na flouride
 • Tumia uzi mwembamba mara moja kwa siku kutoa chembechembe za chakula katikati ya meno, ambayo huleta ukoga
 • Iwapo una kichefuchefu, (nausea and vomiting), jiepushe na kusugua meno yako baada ya kichefuchefu kwani yatafanyika kuwa nadhifu na asidi inayotoka kwa tumbo. Hii inaweza kuathiri eneo la juu la jino lako.

Badala yake, pitisha maji kwenye kinywa chako na ugonje saa moja kabla ya kusugua meno. Hii itasaidia kuzuia asidi kutoka kwa kutapika kutoharibu meno yako. Pia unaweza nawisha na mchanganyiko wa baking soda(kijiko kimoja cha baking soda kwa kikombe kimoja cha maji) kuyeyusha ile asidi.

 • Jiepushe na kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi (kama vile fizzy drinks na chai tamu) na chakula chenye sukari pia kwa mara nyingi.
 • Kunywa maji kwa wingi wakati wote mchana haswa katikati ya milo.
 • Iwapo unahisi njaa katikati ya milo, kula chakula kama vile mboga, matunda, maziwa ya kugandishwa na ujiepushe na chakula chenye sukari nyingi ama asidi.
 • Jiepushe na michanganyo ya kuosha midomo iliyo na pombe
 • Kunawisha meno kwa kutumia maji ya chumvi kila siku (kijiko kimoja cha chumvi kilichoongezwa kwenye kikombe kimoja cha maji vuguvugu) inaweza kuzuia kufura kwa ufizi. Pitisha hayo maji kinywani kwa dakika chache kabla ya kutema (lakini usimeze).

(Vyanzo: American Pregnancy Association, American Dental Association, NHS, HealthHub)

Soma PIA: Want To Combat Dental Plaque? Use These Natural Items

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio