Kwa mtoto ama mtuma mzima, utaratibu wa kulala ni muhimu sana. Inakusaidia kupata kiwango tosha cha usingizi unacho hitaji kufanya kazi vyema siku nzima.
Umuhimu wa utaratibu wa kulala
Kwa watu wengi, siku zao hukuwa ndefu na zenye kazi nyingi. Kupata usingizi tosha ni njia ya kuponya mwili kutayarisha siku nyingine. Kuwa na ratiba ya kulala ni njia ya kujulisha akili kuwa ni wakati wa kumalizia siku. Kwa hivyo, mambo unayo fanya kabla ya kuenda kulala yana changia kukufanya upate usingizi. Unapo endelea kufanya mambo haya, akili yako inapata ujumbe.

Walakini, haijalisha utaratibu ulio nao wa kulala, unapaswa kuwa wa kutuliza. Epuka mambo kama kufagia nyumba ama kujibu barua pepe zako usiku. Kwa watoto wako, usiwa himize kucheza michezo ya video ama kufanya kazi ya ziada muda mfupi kabla ya kulala. Mambo haya yata wafanya wasitake kulala.
Utaratibu wa kulala wa watoto
Weka wakati halisi wa kulala na uhakikishe kuwa kila mtu ana zingatia. Kwa wakati, watoto wako watazoea.
- Kuwa na ishara ya wakati wa kulala
Kwa sababu watoto wengi hawako makini sana na wakati. Unaweza kuwa na kuwa na mambo ambayo unafanya ili kuashiria kuwa wakati wa kulala umewadia. Huenda ikawa kama vile kuweka vidoli mbali ama kuoga. Kwa njia hii, mtoto anajitenga na shughuli anazo fanya na kujitayarisha kulala.

Epuka kula vyakula vizito kabla ya kulala. Kula chakula chepesi kuna saidia mtoto wako kupata usingizi. Mhimize kusugua meno kabla ya kulala.
Kuvalia nguo maalum kunaweza kuwa sehemu ya utaratibu wa kulala. Na wakati, mtoto wako atahusisha kuvalia mavazi hayo na kulala. Pia, hakikisha kuwa mnaweka vifaa vyote vya kielektroniki mbali.
- Shughuli za wakati wa kulala
Kufanya mambo kama vile kuimba, hadithi ya usiku ama kuomba. Baada ya hapo, usingoje mtoto wako alale, mfunikie na uhakikishe kuwa kila kitu kiko sawa kisha umtakie usiku mwanana.
Utaratibu wa kulala kwa watu wazima
Weka wakati ambao unaweza fuata na ujipe muda wa dakika 20-30 kabla ya kuenda kulala. Ili uweze kujitayarisha kabla ya kuingia kwenye kitanda.
Weka vifaa vyote vya kielektroniki mbali. Ikiwa kuna kitu ambacho kinaweza katiza utaratibu wako wa usiku, ni simu yako. Hakikisha unaizima dakika 30 kabla ya kulala.
Kunywa pombe kabla ya kulala huenda ikaonekana kama kitu kizuri. Pombe ina katiza usingizi wako. Hii ni kwa sababu inakufanya utoe jasho na kung'orota. Pia, inaweza kulazimisha kuamka mara chache kwenda msalani.
Kuepuka kuwa na tumbo iliyo jaa. Kula angalau masaa matatu ama manne kabla ya kwenda kulala. Kwa njia hii chakula kina wakati tosha wa kuchakatwa. Lakini ukihisi njaa kabla ya kulala, unaweza kula kitu chepesi kama vile mboga ama tunda.
Chochote unacho amua kufanya kabla ya wakati wako wa kulala, hakikisha kuwa unapumzika. Unaweza amua kusoma kitabu, kuoga kwa maji moto ama kuvalia mavazi ya kulala unayo yapenda zaidi. Pia, unaweza omba ama kutafakari.
Heathline
Soma Pia: Sababu Zinazo Mfanya Mtoto Wako Kucheka Akiwa Amelala