Ikiwa wanandoa wanapatana na changamoto za uzalishaji, ni vyema kukumbuka kuwa hawako peke yao, mbali kuna wanandoa wengine wengi wanaokumbana na changamoto sawa. Utasa ni kawaida zaidi kuliko unavyodhania.
Moja kati ya wanandoa sita hutatizika na changamoto hii na utafiti unadhihirisha kuwa moja kati ya visa vitatu huwa kufuatia matatizo ya utasa katika wachumba wa kiume. Wakati ambapo utasa hauna tiba wakati mwingi, kuna baadhi ya vitu ambavyo unaweza fanya kuboresha nafasi zako za kutunga mimba. Uzalishaji unaweza kuboreshwa kutumia lishe bora na kuimarisha mitindo ya maisha.
Utasa wa kiume

Uzalishaji ni uwezo wa mwanamme kumpa mwanamke mimba.
Utasa wa kiume ni pale ambapo mwanamme hana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito. Mara nyingi huathiriwa na ubora wa seli zake za manii. Utasa unahusishwa na utendaji wa kingono ama ubora wa manii.
- Hamu ya kufanya ngono. Matamanio ya mtu kufanya mapenzi
- Idadi ya manii. Nambari ya maii bora ama kukolea kwa seli za manii
- Mwendo wa manii. Uwezo wa manii kuogelea
- Viwango vya testosterone. Kichocheo cha kiume cha ngongo kinauwezo wa kuathiri utasa
Mara nyingi, utasa huwa na vyanzo vingi na huweza kuathiriwa na geni, afya kwa ujumla, magonjwa, na lishe. Mtindo wa maisha wenye afya ni muhimu. Baadhi ya vyakula huwa na manufaa ya uzalishaji vikilinganishwa na vingine.
Baadhi ya njia za kuboresha kiwango cha manii na kuimarisha uzalishaji katika wanaume.
Fanya mazoezi mara kwa mara
Mazoezi yana manufaa mengi, na mbali na kuboresha afya yako, yanasaidia kuimarisha viwango vya vichocheo vya ngono( testosterone) na kuboresha uwezo wa uzalishaji. Kulingana na utafiti, wanaume wanaofanya mazoezi mara kwa mara huwa na viwango vya juu zaidi vya kichocheo cha ngono ikilinganishwa na wasio fanya mazoezi.
Pata vitamin C tosha
Vitamin C ina uwezo wa kuboresha kinga mwilini. Inasaidia pia katika kuimarisha uzalishaji katika wanaume. Vitamin C pia huimarisha kiwango cha manii na mwendo wake huku ikipunguza seli za manii zilizo haribika.

Pumzika na upunguze mawazo mengi
Mawazo mengi huathiri uwezo wa mwanamme kufanya mapenzi na kutosheleka. Na hivi kuathiri uzalishaji wa mwanamke. Mwanamme anapokuwa na mawazo mengi, anaweza kufanya mazoezi, kutembea ama kuzungumza na watu.
Pata vitamini D tosha
Vitamini D ni muhimu kwa uzalishaji wa kiume na kike. Ina boresha viwango vya kichocheo cha testosterone. Kulingana na utafiti, wanaume wasiokuwa na viwango tosha vya vitamini huwa na viwango vya chini vya testosterone.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Vyakula 8 Vinavyo Ua Manii Ambavyo Wanaume Wanapaswa Kujitenga Navyo!