Kwa nini utengano katika uhusiano huwaumiza wanaume kwa njia tofauti?
Imani zilizoko kuhusu kutengana baada ya kuwa katika uhusiano ni kuwa wanawake huumia zaidi ikilinganishwa na wanaume ambao huhisi uchungu muda baada ya utengano kufanyika.

Kulingana na utafiti, wanawake huumia zaidi, kifizikia na kihisia baada ya utengano. Hata hivyo, wanawake huweza kupona na kuendelea na maisha yao. Kwa upande mwingine, wanaume huendelea na maisha yao na kamwe hawaponi. Jambo linalohusishwa na biolojia ya wanaume.
Tofauti na imani kuwa wanaume hawaathiriwi na utengano katika uhusiano, utafiti wa hivi karibuni unadhibitisha jambo tofauti. Wanaume huathiriwa na utengano katika uhusiano. Muda baada ya kutengana, mwanamke huathiriwa zaidi kihisia na kifizikia. Ila, mwanamke huwa na watu zaidi wa kuzungumzia yaliyompata nao. Kwa njia hii, mwanamke anahisi uchungu na kuonyesha hisia zake hadi anapohisi kuwa ako katika hali bora na kuendelea na maisha yake.
Wanaume wanapoachwa mara nyingi huchukua mvinyo kama njia ya kukabiliana na hisia zao za yaliyowapata. Anapoendelea na maisha yake, atahisi uchungu anapokumbuka alichopoteza na ugumu wa kupata mtu sawa.
Wanaume hukabiliana na hisia zao kwa njia tofauti

Wanaume wamekua katika jamii ambapo mwanamme kuonyesha hisia zake inaonekana kuwa ishara ya dhaifu. Kwa sababu hii, wanaume huficha hisia zao. Kujaribu kuficha hisia zao huwafanya watafute njia mbadala za kuonyesha wanachohisi kama kulewa. Huenda ikaonekana kana kwamba wanaume hawaathiriwi na utengano, lakini ukweli ni kuwa wanaathiriwa kwa njia sawa ama zaidi.
Wanaume hawazungumzii matatizo yao
Wanaume huwa vigumu kuomba usaidizi wanapokumbwa na tatizo. Tofauti na wanawake ambao hawatapoteza muda kuzungumza na marafiki wao. Wanaume hawataki kuonewa huruma, mara nyingi watajiwekea kinachowatatiza.
Wanaume hukana kinachofanyika kwanza

Ili kuishi na makosa yao, wanaume hukana walichokifanya kilichosababisha tukio la utengano. Badala yake, wao huwapa wachumba wao lawama. Baada ya kutengana, huwa na hasira na wachumba wao. Baada ya muda, wataanza kufikiria kuhusu makosa yao na walichofanya na kujuta.
Mwanamme anapokabiliana na hisia baada ya utengano katika uhusiano, inakuwa rahisi kwake kuendelea na maisha kwa njia yenye afya. Tofauti na anapoficha hisia zake.
Chanzo: Science Daily
Soma Pia: Ishara 5 za Kujua Iwapo Mwanamme Anakuthamini Katika Uhusiano