Utosi Wa Mtoto Ni Nini Na Hatari Zinazo Husika Na Sehemu Hii Ni Zipi?

Utosi Wa Mtoto Ni Nini Na Hatari Zinazo Husika Na Sehemu Hii Ni Zipi?

Utosi wa mtoto ni sehemu nyeti zaidi ya mwili wake na unapaswa kuwa makini unapo mshika.

Kwa sasa kwani una mtoto mdogo, huenda ukashangaa kuhusu sehemu laini kwenye kichwa cha mtoto wako; na kwa nini unapaswa kuwa makini na sehemu hii. Huenda ukawa umesikia kuwa sehemu laini ni muhimu sana na kuishika ovyo huenda ikasababisha matatizo kwa mtoto. Kwa hivyo, tuna angazia utosi wa mtoto na hatari zake.

Kabla tuangazie hatari zinazo husika na sehemu hi laini ya mtotom, kuna haja ya kuelewa kwa nini kichwa cha mtoto huwa laini anapo zaliwa na majukumu ya upande huu wa mwili.

what's a soft spot

Utosi wa mtoto na hatari zake: Jukumu la sehemu hii

Sehemu laini inayo fahamika kama utosi wa mtoto unaonyesha mahali ambapo skull haija fungana kabisa baada ya kujifungua. Sehemu hizi zinajulikana kama fontanels. Huenda ikakufurahisha kujua kuwa mtoto wako ana sehemu moja laini juu ya kichwa chake na nyingine nyuma ya kichwa chake na kufanya sehemu mbili laini kwenye kichwa chake kidogo.

Kazi ya sehemu laini kwenye kichwa cha mtoto wako

what's a soft spot

  • Ubongo wa mtoto wako utaendelea kukua baada ya kuzaliwa, kwa hivyo sehemu hizi laini zitakubalisha ubongo kukua kwa kasi hata baada ya mtoto kuzaliwa.
  • Kichwa cha mtoto kinaweza kupita kwa kizazi cha mama mtoto anapo zaliwa kwa sababu sehemu laini inaifanya skull iweze kubadili muundo na kupita.
Mambo ya kusisimua kuhusu fontanel ya mtoto

soft spot

Wataalum wa Neonatal kuwa sehemu iliyo na muundo wa almasi iliyoko kwenye sehemu ya juu ya kichwa inaweza kuwa na upana wa inchi 2. Utaratibu wa kufungana huanza mtoto anapo fikisha umri wa miezi sita na kumaliza kufungana anapokuwa miezi 18.

Kama tulivyo taja hapo awali, kuna sehemu ya pili laini nyuma ya kichwa; kwa hivyo unapaswa kujua kuhusu utosi wa mtoto na hatari zake. Sehemu laini iliyo nyuma ya kichwa cha mtoto ni vigumu kupata; ina muundo wa pembe tatu na upana wa inchi nusu.

Fontanel ya mtoto wako mara kwa mara itapiga wakati sawa na mpigo wake wa roho, kwa hivyo haupaswi kuwa na shaka unapo ona hili likifanyika.

Daktari Tia Hubbard, mtaalum mkuu wa afya ya watoto katika Chuo Kikuu cha California katika San Diego Medical Center, ana washauri wazazi wasiwe na shaka, na kuwa sehemu hizi laini huwa ngumu kuliko unavyo fikiri.

"Inapaswa kuwa laini kwa sababu inakubalisha ukuaji wa kasi wa ubongo unaofanyika katika mwaka wa kwanza wa maisha. Ila, unaweza igusa, sio nyeti vile," aliiambia WebMD.

Sehemu hii laini ina vitu vya kipekee vya kuifunika. Na zina linda ubongo wa mtoto wako unao endelea kukua.

Kulinda sehemu nyeti ya mtoto wako kutokana na hatari

Sehemu laini ya mtoto wako ina pande ya ulinzi; ila hata safu hii ikiwa, ni vyema kwa mzazi na mlezi wa mtoto kuepuka kutingisha mtoto sana. Hakikisha kuwa hakuna anaye igonga fontanel ya mtoto, hata watoto wengine.

Fontanelle ni nini? Jinsi ya kujua wakati ambapo kuna kasoro

utosi wa mtoto na hatari zake

Iwapo sehemu hii imerudi upande wa ndani, huenda hii ikawa ishara kuwa mtoto wako anakosa maji tosha mwilini, hakikisha kuwa umempeleka mtoto hospitalini apate matibabu.

Ukigundua kuwa fontanel ya mtoto wako ime vimba, huenda kukawa na shinikizo nyingi kwenye ubongo wa mtoto wako. Hali hii huenda ikawa hatari sana kwenye maisha yake, bila kukawia, hakikisha kuwa umemwona daktari.

Baadhi ya watoto huenda wakainamisha kichwa chao upande mmoja mara kwa mara, na hii huenda ikasababishwa na tatizo walio nayo. Ili kuhakikisha kuwa mtoto wako hana hali ya torticollis, unapaswa kumpeleka hospitalini apimwe na mtaalum wa watoto. Katika visa vingi, madaktari hutibu hali hii kwa kutumia tiba ya kifizikia; kunyoosha misuli yake na kusaidia mtoto kubadili wanvyo weka kichwa.

Katika mojawapo ya visa visivyo kawaida, mtoto huenda akapata hali ya craniosynostosis. Hali hii ndipo safu moja ama zaidi kwenye kichwa cha mtoto zinashikana. Ni hatari na huenda ikabadili shepu ya kichwa cha mtoto; kwa sababu ubongo unakua na huenda ukaharibika shepu kwa kukosa nafasi tosha. Wataalum wa matibabu wana shauri upasuaji kutenganisha safu hizi zilizo shikana.

Kichwa ni sehemu nyeti ya mwili wa mtoto, na kwa hivyo unapaswa kuwa makini sana unapo ishika. Sehemu hii laini itajifunga yenyewe bila tatizo lolote; ila ni muhimu kuhakikisha kuwa hakuna kitu kinacho isumbua. Ukigundua kuwa kuna kitu kisicho cha kawaida kuhusu fontanel ya mtoto wako, tafadhali mjulishe daktari wako bila kukawia.

Kumbukumbu: What to Expect

WebMD

Soma pia: Je, Ni Maziwa Gani Bora Kwa Mtoto Mchanga?

Written by

Risper Nyakio